Mambo ya Msingi Sana katika maisha

Mambo ya Msingi Sana katika maisha

Hakika....wapo wawaonao ndugu zao ambao hawajafanikiwa kama hawana akili na kuekti wanampenda Mungu sana... kumbuka usipompenda ndugu yako unayemuona utampendaje Mungu usiyemuona... mnafiki wewe...kutokumjali ndugu yako ni kumchukia dhahiri....wapo wasiopenda hata kuwasiliana na ndugu zao na akijua una namba yake anabadilisha nyingine.... wanafiki wakubwa
Kwakweli ni heri ya Mchawi kuliko Mnafiki.
 
(1) Ukipiga mihayo (yawning), chafya au kukohoa, funika mdomo na pua kwa mikono yote miwili.

(2) Usiteme mate, kutapika, kupenga kamasi, wenzako wakiwa wanakula.

(3) Ukienda nyumbani kwa mtu, hususan rafiki, usitangaze madhaifu utakayoyaona. Mfano: Watoto wao wanashindia nguo zilizochanika.

(4) Rafiki yako unayeheshimiana naye, usiwe na namba ya simu ya mkewe ili kuepuka kutembea naye.

(5) Ukiacha kazi ofisini, usiwatukane former employers wako kwa maana katika maisha kuna leo na kesho.

(6) Ni vema ukapakua chakula kidogo kisha ukaongeza kuliko kupakua kingi alafu ukashindwa kukimaliza.

(7) Ukienda kwenye sherehe, hata kama wewe ni ndugu za karibu, usikae sehemu za VIP bila kukaribishwa. Ni aibu sana kuambiwa uondoke kwenye seat za VIP uende kwa wageni wa kawaida.

(8) Ukigundua spouse wa rafiki yako ana uhusiano wa nje ya ndoa, mfuate na mkanye ila usimwambie mumewe/mkewe.

(9) Mtu akikusaidia mara moja, usimgeuzi kitega uchumi cha kumuomba mara kwa mara. Kumbuka yeye pia ana majukumu yake binafsi.

(10) Ukiongea kwenye simu na mtu wa mbali sio vizuri kusema "fulani (Alex) nipo naye hapa ongea naye pia. Kama huyo Alex hajakuomba kuongea na mhusika basi kaa kimya.

(11) Ukipata mshahara mwisho wa mwezi, wape kidogo mfanya usafi pamoja na mpika chai hapo ofisini kwenu. Hao ndio informers na wanajua mengi ya hapo ofisini kwenu.

(12) Usiache kwenda likizo ya mapumziko kwa kuambiwa eti "tutakufidia kwa fedha hizo siku 28 za mapumziko". Afya yako ya akili ni kitu cha msingi sana.

(13) Ukienda ugenini kisha ukaachwa peke yako sebuleni, usishike chochote kama mwenyeji wako hayupo (ameenda kunununulia soda kwa mfano). Hata kama ni gazeti umelikuta hapo, subiri akirudi ndio umuombe.

ONGEZEA NA WEWE NDUGU YANGU......
Nimeipenda hii
 
14. Usiwadharau WanaCCM hata kama ni Chipukizi maana hao ndio WanaCCM wa Kesho ambao Watampangia nini cha kufanya mtoto wako.
 
Usianzishe mada nyengine na wenzio ndani ya thread yenye mada yake tayari.

Kufanya hivyo unatutibua wasomaji badala ya kupata majibu sahihi kuhusiana na thread husika tunaishia kupata chatting za kisenge ndani ya thread ya mtu.
Sawa boss. Asante kwa mchango wako.
 
Ukila kula kwa mkono wa kulia tu, usishike chai mkono wa kushoto na mkate kulia.
Safi sana mkuu. Alafu mkuu, kuna wale watu unakuta anakatakata vipande vya mkate kisha anatumbukiza ndani ya kikombe cha chai alafu anaanza kuchota kwa kijiko au vidole kisha anakula.

Aisee wanatia sana kinyaa..
 
Ukisalimiana na mtu ukiwa umekaa akikupa salam na mkono simama ndo umpe mkono pia (usi-shakehand) ukiwa umekaa
Yes. Hususan ukikutana na watu wa "High Class" kama wale ndugu zetu wa Oyster Bay pamoja na Masaki..
 
Ukila tafuna huku umefunga mdomo.

Ukila kula kwa mkono wa kulia tu, usishike chai mkono wa kushoto na mkate kulia.

Ukisalimiana na mtu ukiwa umekaa akikupa salam na mkono simama ndo umpe mkono pia (usi-shakehand) ukiwa umekaa
ANOTHER ONE: Ni vema kula na watoto meza moja ili kuweza kuwafundisha table manners..
 
Ukigundua spouse wa rafiki yako ana uhusiano wa nje ya ndoa, mfuate na mkanye ila usimwambie mumewe/mkewe.
Hii ngumu sana, kumkanya mtu hakumtoi usaliti.

Mwanamke au mwanaume anaesaliti agano la ndoa kavunja ndoa. Accountability acha wafanye ndani wao lakini ukweli mwamba ajue kua Shemeji ni mchafu
 
Kwa hiyo solution ni kukaa kimya as if you saw nothing. Au sio mkuu??
 
Back
Top Bottom