Mambo yaliyokuwa yanakuudhi nyumbani ulipokuwa mdogo...

GREAT NAME

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2016
Posts
1,078
Reaction score
1,718
Mimi nilikuwa nakereka kwa mambo haya:

1: Kurudi home mchana nakuta madha anachambua mboga halafua ananiambia nikawashe jiko na inabidi nirudie shule,

2: Anapita home msichana tunayesoma naye darasa moja hata sijamwongelesha, madha anaongea kwa sauti ya juu 'We hivi leo si ndio zamu yako kuosha vyombo’

Duuuh, nilikuwa nakasirika vibaya! Wewe je?
 
Kuchota maji huku mie nataka kucheza rede, na ile mwenzio anakupitia umsindikize sokoni, mama anakukatazs
 
niletee kitunguuu-- unaleta
niletee nyanya-- unaleta
niletee kisu-- unaleta
niletee maji-- unaleta
hujakaa sawa
niletee mwiko-- unaleta
hujapumzika unasikia
hebu niletee chumvi
hadi hicho chakula kiive umeshatembea zaidi ya km 10 kufata vitu tu.
 
Mie nilikuwa nachukia mama yangu alikuwa ana tabia kwa mfano kama tunatembea naye njiani, akikutana na mtu pale alipokuwa anaanza kunitambulisha "HUYU NI MWANANGU WA 3 KUMZAA ANAITWA...."
Kuna siku alikuwa ametupanga mimi na ndugu zangu baada ya kutoka church, siku alisalisha padre mgeni, basi akaanza zake "PADRE HAWA NI WANANGU, WA KWANZA NI HUYU, WA PILI NI HUYU WA TATU NI HUY...." mie hapo hapo nikatoka nduki kukimbia kuelekea home, wakati bado angali anatutambulisha kwa father mgeni, alivyorudi nyumbani akanikuta, kilichonipata....... ngoja kwanza nitamalizia kesho

Yote kwa yote R.I.P mama yangu kipenzi
 
RIP mama Nahuja
 
kazi yangu ilikuwaga kufagia uwanja wa mbele ya nyumba kila asubuhi, sasa najicheleweshaga kila siku mpka wenzangu wanapita mchaka mchaka me bado nafagia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…