Mambo yaliyokuwa yanakuudhi nyumbani ulipokuwa mdogo...

Baba alikuwa ananikera.
Akirudi kazini ananiamsha nikamnunulie dawa pharmacy.
kuna wakati nikienda kununua Dawa.kama kuna sehemu kuna kibaraza nalala.mpaka anakuja kunifata mwenyewe.
 
Mm nilikuwa nachukia kuamshwa asubuhi niwahi namba shuleni eti walimu wa field wakali mwaaàaaa
mimi tulikuwa tunashindana kuwahi shule ya msingi na rafiki yangu siku moja nikawahi kulala saa moja nikashtuka baadae kidogo kwa kuwa nilikuwa nishavaa sale ya shule kabisa nikavaa viatu huyo nikawaacha hom wamelala mi nikasepa,
ashukuliwe yule mlevi aliyeniludisha mpaka nyumbani,ilikuwa saa tano usiku ye ndo katoka bar.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mpunga ukianza kuchanua, mi na dogo tunaenda kushinda pori kufukuza ndege wasile mpunga. Kilichokuwa nlkinauzi mbuga yetu iko mbali sana halafu katikati ya pori, woga plus kushinda unaongea na ndege ilikuwa mbaya sana. Ai heti zati momenti
 
Nikifika kutoka shule nakuta wamekula ugali wote, alafu naambiwa ''mboga ipo songa ugali wako ule au kama umeshiba subiria usiku''...kwa asira nawasha jiko alafu napakua mboga nyingiiii...labda wawe wamenipakulia mboga ndo inakuwa ponapona yao
 
undertwentyboy bado mdogo tu...
 
niletee kitunguuu-- unaleta
niletee nyanya-- unaleta
niletee kisu-- unaleta
niletee maji-- unaleta
hujakaa sawa
niletee mwiko-- unaleta
hujapumzika unasikia
hebu niletee chumvi
hadi hicho chakula kiive umeshatembea zaidi ya km 10 kufata vitu tu.

Tehtehtehteh..........
Nilikuwa sipendi kutumwa kwenda kusaga unga mashineni
 
Mimi nilikuwa naambiwa UTAKULA MIGUU YAKO!
Hiyo maza alikuwa ananiambia kama amenipa kazi alafu nimeenda kuzurura sijaifanya...na kama ni usiku mshua yupo napewa kichapo ,alafu naambiwa nikaoge then nikalale bila kula...lakini maza usiku ananionea huruma ananiletea msosi room...NAMPENDA SANA MAMA
 
This is so touching
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…