Mambo yaliyotakiwa kuzingatiwa kabla ya “Royal Tour”

Mambo yaliyotakiwa kuzingatiwa kabla ya “Royal Tour”

jmushi1

Platinum Member
Joined
Nov 2, 2007
Posts
26,329
Reaction score
25,263
Wanajamvi,

Nimeona niseme hili bila kuwa “bias”. Kwa maslahi ya Taifa letu na wananchi wake kwa ujumla.

Kwasababu sitaki kuwa “negative” kuhusiana na jitihada za serikali hii ya “awamu ya sita”, ningependa kuweka wazi hii “disclaimer”

Kwamba nakubaliana na jitihada za kutangaza Taifa letu kwenye utalii na uwekezaji. Lakini pia nina ushauri. Na huu unatokana na uhalisia uliopo.

Uhalisia ninaouzungumzia, ni kuhusu “target market” yetu. Kwamba sasa tunawaonyesha “documentary” kuhusu vivutio vyetu, pamoja na mazingira stahiki ya uwekezaji kwenye Taifa letu.

Watalii walio wengi na wawekezaji, huwa wana “rely” ama kutegemea “informations” kutoka serikalini mwao. Mosi, ni kuhusu sehemu/Taifa husika. Na pili wananchi wake na usalama wa wageni nk.

Mfano kwa wamarekani, wengi hutizama ama kupata taarifa za huko wanakoenda, kwa kupitia https://travel.state.gov ambapo kuna taarifa rasmi kutoka serikalini mwao, kuhusiana na Taifa husika.

Naomba niweke taarifa za serikali ya marekani kuhusiana na safari za kuja Tanzania. Kwamba watakaoamuwa kuja Tanzania, watarajie nini. Either kuja kwenye utalii ama uwekezaji. Naomba ni “paste and copy” kutoka kwenye “website” hiyo ya serikali ya marekani kuhusiana na tahadhari ama “precautions” za kuchukua wakati unasafiri kuja Tanzania kwa nia yoyote ile. Iwe utalii au hata uwekezaji. Almuradi unakuja Tanzania.

Sisi tupo kwenye “level 2” ya “Travel advisory levels”, ambapo hiyo “level” yetu inatamka wazi kwamba “exercise increased caution”, ikiwa na maana kwamba ni lazima uchukuwe umakini wa hali ya juu.

Binafsi sijaona “big deal” kihivyo. Maana nyingi ya hizo “cautions”, zinahusika na “same sex relationships”, yani wakija huku kama wana tabia za kishoga, au kama ni mashoga, basi wasijiachie na kuonyesha wazi wazi hadharani.

Hilo mimi wala sipingi. Siwezi kufanya hivyo kutokana na utamaduni wetu sisi ulivyo. Lakini, lengo langu, ni kwamba yalitakiwa kujadiliwa. Haswa ambayo ni mengine zaidi ya hilo la ushoga. Kuna mengine mengi ambayo ni vyema serikali yetu na ile ya marekani wangeyajadili sambamba na hili la kuwataka waje kutalii na kuwekeza nchini mwetu…kwamba, je mnatuchukuliaje sisi watanzania wakati ambapo tunawataka muje kutizama vivutio na uwekezaji?

Je ni kweli yaliyowekwa kwenye serikali yao kutuhusu sisi ni ya kweli? Je pamoja na sisi ku “promote” waje kwa kupitia uzinduzi wetu wa “The roya tour”, wanawaeleza nini wananchi wao kuhusiana na Taifa la Tanzania na watu wake?

Naomba niweke kipengele cha “country summary”, ambapo wameweka kwa kifupi. Lakini ninaweka pia “link” ili msomaji uweze kujisomea wewe mwenyewe.

“Country Summary: Violent crime, such as assault, sexual assault, robberies, mugging, and carjacking, is common. Local police may lack the resources to respond effectively to serious crime.”

Kwenye “country summary”, ambapo wengi wa raia hao wa marekani lazima wasome, kuna ukakasi. Je serikali yetu inakubaliana na maelezo hayo? Kwamba hayo madhambi mfano “sexual assault”, “violent crimes” nk ni mambo ya kawaida hapa Tanzania? Haya ni maswali tulitakiwa tujiulize na pia yalitakiwa yawekwe mezani wakati wa vikao kati yetu na serikali ya marekani. Ambapo, kama nilivyomsikia mh Rais, vilihusu kurudisha mahusiano yetu na wamarekani kuwa mazuri. Na hivyo kuwa ni mojawapo ya sababu za kutangaza movie ya “the royal tour”

Naomba niweke “link” ili mwanajamvi ujisomee wewe mwenyewe na pengine kutoa maoni yako kuhusu hili jambo.

Kama ni kweli kuna mabadiliko kwenye serikali ya awamu hii, mabadiliko ambayo mama Samia alisema ndiyo yanayopelekea sisi kurudisha mahusiano yetu na marekani kuwa mazuri, basi wangewasisitizia wayapitie hayo. Ili raia wao wasipate ukakasi wanapotaka kuja huku. Bila kujali kwamba wanaokuja huku siyo lazima wawe ni mashoga au wenye ku sapoti tabia hizo.

Mkuu , hongera kwa uchambuzi makini pia nina jambo la kukumbusha.

Huyu mama mwenyewe alisema kuna "magaidi" walikwishakamatwa tangu 2020 na Mbowe ana kesi ya kujibu.

Ajabu ni kuwa Mbowe aliachiliwa bila kizuizi ila hili suala litamtesa sana huyu mama sababu hakuna mahali alikuja kujitokeza kusema hatua walizochukuliwa hawa magaidi waliokamatwa mwaka 2020.

Kwa Mbowe ni dhahiri hata mtoto wa miaka 10 anajua hakua hata na harufu ya ugaidi hata chembe.

Mama ajitokeze aseme sasa ugaidi upo au umeisha?
 
Mkuu , hongera kwa uchambuzi makini pia nina jambo la kukumbusha.

Huyu mwenyewe alisema kuna "magaidi" walikwishakamatwa tangu 2020 na Mbowe ana kesi ya kujibu...
Well said.
 
Mkuu , hongera kwa uchambuzi makini pia nina jambo la kukumbusha.

Huyu mama mwenyewe alisema kuna "magaidi" walikwishakamatwa tangu 2020 na Mbowe ana kesi ya kujibu.

Ajabu ni kuwa Mbowe aliachiliwa bila kizuizi ila hili suala litamtesa sana huyu mama sababu hakuna mahali alikuja kujitokeza kusema hatua walizochukuliwa hawa magaidi waliokamatwa mwaka 2020.

Kwa Mbowe ni dhahiri hata mtoto wa miaka 10 anajua hakua hata na harufu ya ugaidi hata chembe.

Mama ajitokeze aseme sasa ugaidi upo au umeisha?

Acha siasa kwenye mambo serious ya kitaifa
 
Wanajamvi,

Nimeona niseme hili bila kuwa “bias”. Kwa maslahi ya Taifa letu na wananchi wake kwa ujumla...
Binafsi nadhan hilo ni jambo dogo kwa wana wa Marekani kwa sababu popote walipo duniani wako protected na serikali yao na ndiyo kazi za mabalozi na CIA hivyo wengi hawatazami hizo taarifa zao ambapo kimsingi kwenye nchi zilizoendelea kama marekani hizo violent crimes ni kawaida kubwa linaloogopwa na violent extremism ambapo kwetu haipo na kama nchi na movies yetu inaendelea kusisitiza ukarimu na umakini kwa wageni nadhani litasaidia kuondoa hiyo notion.
 
Nataka nikujibu, lakini kwanza naomba nikuulize swali, Je umeshawahi kuishi Marekani?
 
Hiyo ni improvement hata hivyo maana tulikua level 4 . lakini baada ya kupiga kelele naona wameona watuondoe huko. Hali ilikua hii.

Screenshot_20220413-232427.png
 
Bwamdogo umeongea mantiki sana.
Anayekuja hoyee in makongoro voice👊👍👍👍
 
Pitia pia huu uzi.

Wanajamvi,

Nimeona niseme hili bila kuwa “bias”. Kwa maslahi ya Taifa letu na wananchi wake kwa ujumla.

Kwasababu sitaki kuwa “negative” kuhusiana na jitihada za serikali hii ya “awamu ya sita”, ningependa kuweka wazi hii “disclaimer”....
The royal tour ni travel documentary ya mwandishi habari wa kimarekani siyo yetu. Sisi mama aliweka muda mwingi sana wa kazi bila kuelewa background yake. Angeangalia viongozi wenzake wa Rwanda, Israel, Poland, Mexico na Equador walifanya nini walipomkaribishwa mwandishi huyo. Kuna wapiga debe wengie hapa wameshupaa kama kweli ile ni sinema ya mama.

Kuhus kuvutia utalii, serikali inabidi ishughulikiea madhaifu hayo uliyoona ambayo kiukweli kama ulivyosema ndiyo wamarekani wanayoangalia kwa ujumla kabla hawajapanga kwenda kuzurura duniani.
 
Back
Top Bottom