Mambo yanayomfanya Rais Samia kupendwa sana na Watanzania

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
319
Reaction score
755
Wataalam wa mambo tunajua kuna vigezo vingi vinavyozingatiwa ili kutolewa tuzo ya Amani ya Nobel. Yanayowekwa hapa ni baadhi tu ya mambo yanayomfanya Rais Samia kupendwa sana na watanzania kama kiongozi mwenye kujali watu wake na mwenye weledi mkubwa wa kiuongozi;

1. Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha 6. Mikopo kwa wanafunzi wote wenye vigezo kwaajili ya kupata elimu ya Juu katika Vyuo vikuu vya Umma na Binafsi.

2. Ujenzi wa madarasa 15,000 kuwawezesha wanafunzi wote 907,803 waliopaswa kuanza masomo ya sekondari kuanza masomo kwa wakati mmoja.

3. Kupandisha mshahara kwa asilimia 23.3 kwa watumishi kuanzia wale wa kima cha chini. Kuongeza posho kwa zaidi ya asilimia 100.

4. Kupandisha madaraja watumishi wa umma wenye sifa, kulipa malimbikizo ya madeni kwa watumishi na kulipa madeni yote halali kwa wazabuni.

5. Kuondoa kodi katika mahitaji muhimu ya wakulima, dhana na vifaa vinavyo athiri moja kwa moja mnyororo wa thamani katika maeneo ya kilimo, ufugaji na uvuvi.

6. Kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mbalimbali Duniani na Taasisi zenye umuhimu kwa ustawi wa Tanzania.

7. Kuimarisha Sekta binafsi hususani katika biashara na uwekezaji na kutangaza vivutio vya utalii kwa namna ya kipekee Duniani.

8. Kutoa fedha katika miradi yote muhimu na kuanzisha miradi mipya ya maendeleo inayogusa malengo ya muda mrefu na mfupi ya Taifa.

9. Kuboresha huduma za jamii na kuchochea utekelezaji wa mipango endelevu kwa kasi kubwa. Miradi katika huduma za Maji, Afya, Elimu, Kilimo n.k

10. Kutoa vibali vya ajira kwa kila Taasisi yenye uhitaji, kuwawezesha vijana na wajasiriamali katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuwatambua wale wanaochipukia katika eneo la ubunifu na Teknolojia (startups).

Kwa hakika, Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi aliyeweka rekodi ya kipekee Barani Afrika kwa kutekeleza adhma yake ya kuona wananchi wanakuwa na maisha bora. Mungu ambariki ili aendelee kuwatumikia watanzania kwa upendo na aweze kufikia adhma yake kwa 100%.
 
Nampongeza na kumshukuru mama yetu kipenzi rais wa awamu ya sita wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kutuwezesha watanzania kula chakula cha mchana bila kusikia mlio wa risasi wala bomu, kiukweli mama anaupiga mwingi[emoji16][emoji1787]
 
Tunampenda sa100 kama tunavyo yapenda mafiii
 
Kilimo kupewa kipaombele
Ushauri wangu waambie waajiri wako wakulipie na nssf maana kazi unayoifanya kupaka rangi maiti sio ndogo, kuna wenzio walikua walipwa buku saba per day enzi za mwenda zake walifanya sana fujo humu jukwaani ila sasa ivi ni zilipendwa wamepauka kama kipande cha muhogo
 
Ni ajabu uliye hai unaongozwa na maiti..

Hivyo vyote ninavyo mkuu labda utaje vingine..

On top of that Kongeza bajeti kwenye Wizara zooote unazozijua wewe..

Mwisho kuondoa kabisa kilio cha Wabunge Kuhusu Tarura, yaani hutosikia tena kwamba Tarura imekosa pesa.
 
IMG_2368.jpg

Ni kweli
 
Wataalam wa mambo tunajua kuna vigezo vingi vinavyozingatiwa ili kutolewa tuzo ya Amani ya Nobel. Yanayowekwa hapa ni baadhi tu ya mambo yanayomfanya Rais Samia kupendwa sana na watanzania kama kiongozi mwenye kujali watu wake na mwenye weledi mkubwa wa kiuongozi;

1. Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha 6. Mikopo kwa wanafunzi wote wenye vigezo kwaajili ya kupata elimu ya Juu katika Vyuo vikuu vya Umma na Binafsi.

2. Ujenzi wa madarasa 15,000 kuwawezesha wanafunzi wote 907,803 waliopaswa kuanza masomo ya sekondari kuanza masomo kwa wakati mmoja.

3. Kupandisha mshahara kwa asilimia 23.3 kwa watumishi kuanzia wale wa kima cha chini. Kuongeza posho kwa zaidi ya asilimia 100.

4. Kupandisha madaraja watumishi wa umma wenye sifa, kulipa malimbikizo ya madeni kwa watumishi na kulipa madeni yote halali kwa wazabuni.

5. Kuondoa kodi katika mahitaji muhimu ya wakulima, dhana na vifaa vinavyo athiri moja kwa moja mnyororo wa thamani katika maeneo ya kilimo, ufugaji na uvuvi.

6. Kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mbalimbali Duniani na Taasisi zenye umuhimu kwa ustawi wa Tanzania.

7. Kuimarisha Sekta binafsi hususani katika biashara na uwekezaji na kutangaza vivutio vya utalii kwa namna ya kipekee Duniani.

8. Kutoa fedha katika miradi yote muhimu na kuanzisha miradi mipya ya maendeleo inayogusa malengo ya muda mrefu na mfupi ya Taifa.

9. Kuboresha huduma za jamii na kuchochea utekelezaji wa mipango endelevu kwa kasi kubwa. Miradi katika huduma za Maji, Afya, Elimu, Kilimo n.k

10. Kutoa vibali vya ajira kwa kila Taasisi yenye uhitaji, kuwawezesha vijana na wajasiriamali katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuwatambua wale wanaochipukia katika eneo la ubunifu na Teknolojia (startups).

Kwa hakika, Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi aliyeweka rekodi ya kipekee Barani Afrika kwa kutekeleza adhma yake ya kuona wananchi wanakuwa na maisha bora. Mungu ambariki ili aendelee kuwatumikia watanzania kwa upendo na aweze kufikia adhma yake kwa 100%.
Ndo tatizo la kuandika ukiwa bleed, Hao unaosema Watanzania wanampenda Samia ni wateule wake wanamsifia kwa kujipendekeza. Njoo mitaani uliza Watanzania kumi kama wanampenda Samia, hutompata hata mmoja anayempenda
 
Sijui kwanini moyo wangu unakua mzito sana kumpongeza ila wakimpongeza wengi inatosha pia, sio lazima tufanane
 
Back
Top Bottom