Mambo yanayomfanya Rais Samia kupendwa sana na Watanzania

Mambo yanayomfanya Rais Samia kupendwa sana na Watanzania

Bangi ni mbaya ila akili zako ni mbaya zaidi. Yaani ushuzi huo ndo umpe mtu tuzo ya nobel! Hii nchi ina mataahira sana na nakubaliana na utafiti kuwa watanzania wengi wanatatizo la afya ya akili.
Taka ngumu hii
 
Wataalam wa mambo tunajua kuna vigezo vingi vinavyozingatiwa ili kutolewa tuzo ya Amani ya Nobel. Yanayowekwa hapa ni baadhi tu ya mambo yanayomfanya Rais Samia kupendwa sana na watanzania kama kiongozi mwenye kujali watu wake na mwenye weledi mkubwa wa kiuongozi;

1. Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha 6. Mikopo kwa wanafunzi wote wenye vigezo kwaajili ya kupata elimu ya Juu katika Vyuo vikuu vya Umma na Binafsi.

2. Ujenzi wa madarasa 15,000 kuwawezesha wanafunzi wote 907,803 waliopaswa kuanza masomo ya sekondari kuanza masomo kwa wakati mmoja.

3. Kupandisha mshahara kwa asilimia 23.3 kwa watumishi kuanzia wale wa kima cha chini. Kuongeza posho kwa zaidi ya asilimia 100.

4. Kupandisha madaraja watumishi wa umma wenye sifa, kulipa malimbikizo ya madeni kwa watumishi na kulipa madeni yote halali kwa wazabuni.

5. Kuondoa kodi katika mahitaji muhimu ya wakulima, dhana na vifaa vinavyo athiri moja kwa moja mnyororo wa thamani katika maeneo ya kilimo, ufugaji na uvuvi.

6. Kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mbalimbali Duniani na Taasisi zenye umuhimu kwa ustawi wa Tanzania.

7. Kuimarisha Sekta binafsi hususani katika biashara na uwekezaji na kutangaza vivutio vya utalii kwa namna ya kipekee Duniani.

8. Kutoa fedha katika miradi yote muhimu na kuanzisha miradi mipya ya maendeleo inayogusa malengo ya muda mrefu na mfupi ya Taifa.

9. Kuboresha huduma za jamii na kuchochea utekelezaji wa mipango endelevu kwa kasi kubwa. Miradi katika huduma za Maji, Afya, Elimu, Kilimo n.k

10. Kutoa vibali vya ajira kwa kila Taasisi yenye uhitaji, kuwawezesha vijana na wajasiriamali katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuwatambua wale wanaochipukia katika eneo la ubunifu na Teknolojia (startups).

Kwa hakika, Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi aliyeweka rekodi ya kipekee Barani Afrika kwa kutekeleza adhma yake ya kuona wananchi wanakuwa na maisha bora. Mungu ambariki ili aendelee kuwatumikia watanzania kwa upendo na aweze kufikia adhma yake kwa 100%.
Nadhani wewe ni miongoni mwa walamba asali.

1. Wachimba madini wadogo wadogo wote wamenyang'anywa maeneo yao
2. Kikokotoo
3. Tozo
4. Safari za nje ya nchi kila uchao ikiwa ni pa1 na kwenda Dubai kumsalimia mjomba

Bado unasema Watanzania wanampenda Mtemi Hangaya!!!!!!!
 
Hadi Heche Mwenyewe kakiri Leo kwenye big ajenda kumkubari mh.Rais na kasema amewahi mpongeza mara kadhaa,sasa kenge kwenye msafara wa Mamba ndio wanasumbua.
 
Sio kwamba Rais Samia anapendwa sana bali AMESUSWA na kupotezewa...hakuna jipya!!! In short labda upendo wa kulazimishia
 
Hadi Heche Mwenyewe kakiri Leo kwenye big ajenda kumkubari mh.Rais na kasema amewahi mpongeza mara kadhaa,sasa kenge kwenye msafara wa Mamba ndio wanasumbua.
Sasa Heche ndiye nani....kwamba alivomkubali basi wote tumkubali....nani hajui heche amelambishwa.......??
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Ukishiba mataputapu ndio akili zinakuwa namna hii
Kamfufue uzikwe wewe. Tunataka uhuru na haki siyo kupora korosho, Kuua, kupogana risasi, kupotezana na kubambikiana mikesi.
Mungu fundi sana
 
Back
Top Bottom