Mambo yanayonikasirisha Kanisani

kunapokua na ratiba lazima ifuatwe. Vinginevyo wasiweke ratiba hakuna atakayepigia kelele muda.

Kama wewe unaweka rules mwenyewe alafu hauzifuati utapata wapi uwezo wa kuniambia mimi nishike amri zako au za Mungu?
 
Kimsingi ratiba lazima iheshimiwe. Dunia imebadilika
Mkuu unakaza shingo tu kwa sababu ya kiburi na uzima ulio nao sasa,amini hivyo.

Mwaka 2020 may nilimshuhudia rafiki yangu akiwa ktk kitanda cha mauti pale Muhimbili alikuwa analia anamuahidi Mungu kwamba akichomoka ktk lililomsibu atamuabudu kwa namna isivyoelezeka na huyu alikuwa busy kweli na mambo ya dunia!


Kama wewe daktar au nurse au polisi unao uwezo wa ku-argue hivi but unatoka kanisani unaenda kunywa supu bar kisha unataka Ibada izingatie muda wako no bro hivi hatutafika tunapopiga magoti tufike.

Niamini mkuu!
 
Naunga mkono 100%. Mfano Kwaya nyingi zina kigagasi (egocentrism) mara nyingi huwa wanaambiwa na kuonywa waimbe zile nyimbo zinazofahamika na wengi na kama ni lazima basi wimbo mpya uwe ni 1 au 2 tu na wimbo huo urudiwe-rudiwe mara nyingi kadri iwezekanavyo ili na waumini wengine waujue.

Lakini wapi!! hawaambiliki.... Wata-surf kwenye Swahili music notes na kukusanya nyimbo mpya huko na kuziimba bila kujali kwamba wao wanachangia tu kukoleza Ibada ili washiriki waweze kushiriki kikamilifu(Active participation) na kwamba pale sio mahali/jukwaa la maonesho au mbwembwe.

Aidha nyimbo nyingine haziko kama ni sala na hivyo zinapigwa marufuku.
 
Na hili ni tatizo kubwa. Kwenye English Services kuna vitabu, utafuatilia nyimbo na kuimba na kushiriki ibada. Huku uswahilini wanajiimbia tu manyimbo yenyewe mabaya hayana ata ladha
 
I think hii ni kutokana na kasi ya mabadiliko ya dunia, well kama ikitokea

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwezekano wa kutokea ni mkubwa sana kwani mchakato wa kuleta mabadiliko ndani ya kanisa Katoliki umeshaanza ngazi za chini (Grassroot level) kwa kusambaza questionnaire (dodoso) litakalojazwa na waumini wake wote na wale wasio waamini wa kanisa hilo.

Aidha hali ya Kanisa hilo inazidi kuwa Tete kwani Kanisa na baadhi ya Wahudumu wake limekumbwa na kashfa nyingi.
 
Dini zimejengwa kwenye kutisha waumini wake ili waipate adhabu huko rohoni siku ya kufa..uzuri ni kwamba yote mazuri na mabaya huwapata wanao sali nawasio sali..hata maandiko yameweka wazi kuwa Mungu huwanyeshea mvua waovu na wasio waovu.

Live your life chamsingi ishi katika haki na utauwa pia dini iliyosafi ni ile inayosidia wahitaji katika uhitaji wao.

Tofauti na hapo endeleeni kulipa kodi ya koloni rome kila jpl mpelekapo sadaka..huku divai wakishindialia mapadri na kutoka vitambi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Huku unalalamika misa inachukua muda mrefu at the same time unataka upate nafasi ya kuuliza. Hivi wakiruhusu maswali Misa utachukua masaa mangapi
maswali matatu ya msingi hayawezi kuumiza muda
 
Na hili ni tatizo kubwa. Kwenye English Services kuna vitabu, utafuatilia nyimbo na kuimba na kushiriki ibada. Huku uswahilini wanajiimbia tu manyimbo yenyewe mabaya hayana ata ladha
Hawawasomi(they don't Study) wasikilizaji wa nyimbo zao na kutaka kujua reaction yao kwa nyimbo wanazoimba.

Wao ni mbele kwa mbele tu kana kwamba wasipoimba Misa/Ibada haitakuwepo.
 
kunapokua na ratiba lazima ifuatwe. Vinginevyo wasiweke ratiba hakuna atakayepigia kelele muda. Kama wewe unaweka rules mwenyewe alafu hauzifuati utapata wapi uwezo wa kuniambia mimi nishike amri zako au za Mungu?

Mkuu nina imani unao utashi wa kuelewa kitu kinaitwa ratiba na kitu kinaitwa dharura.

Usually maisha ya binadamu lazima awe na ratiba,Kikanisa na zaidi kiimani ratiba zimewekwa ili watu wapate muda wa kufanya yale yaliyo nje ya kumuabudu Mungu ktk ile siku maalumu (na siyo kwenda kufanya zile kazi ngumu ni kipindi hiki tu waamini tumekuwa viburi au sijui ndo ugumu wa maisha)

Lakini tukija kiimani hasa inapotokea dharura lazima tuelewe kwamba ratiba zetu na Mungu ni vitu viwili tofauti,let's say siku hiyo imepangwa kutolewa mahubiri na padre mwenye karama ya kitu fulani na lazima kwa sababu ni mara chache atakuja parokiani kwenu itabidi atumie muda mrefu kuhubiri ili kiu ya waamini iishe ktk situation kama hii kipi muhimu?

Utoke kanisani kwa sababu ratiba mliyojiwekea imevunjwa uache kusikiliza neno la Mungu uende ukakae nyumbani au bar huku umefura kwa hasira ukilalamika muda waliokupotezea kwenye Ibada?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…