MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
- Thread starter
- #81
kunapokua na ratiba lazima ifuatwe. Vinginevyo wasiweke ratiba hakuna atakayepigia kelele muda.Sioni bado mantiki ya muumini wa imani yoyote kukaza shingo kutaka Ibada izingatie muda!
Kiumbe binadamu Mungu amekuzawadia zawadi ya pumzi siku 6 bila kukutoza chochote na halijakupata lolote baya lakini unashindwa kukaa mahali pamoja palipoamuliwa kumuabudu na kumsifu kwa angalao masaa matano?
Wengine wanalalamika sadaka (sitazungumzia nje ya Kanisa Catholic) ila naamini utoaji na matumizi ktk Kanisa yapo wazi sana,mfano;inatangazwa mchango wa pili ni kwa ajili ya maendelo ya Kanisa,haitegemewi leo majengo ya Kanisa yamepata hitilafu ya umeme wasubiri mpaka waumini washtuliwe ktk Ibada kwamba kuna mchango wa kuchangia marekebisho ya wiring au mfumo wa maji!
Ajabu wengi wanaolalamika wana watoto wawili+ wanasomesha shule za 1.5ml per kichwa,wakiwa watatu ni 4.5mil huyu ni muumini anapiga magoti kumuomba Mungu ampe mwanae akili lakini muumini huyu huyu anashindwa kutoa sadaka 10K kwa ajili ya maendelo ya pale anapopigia magoti Mungu amsikie mwisho mtoto akifeli anaona Mungu wa Catholic hana jipya anaenda kulipa 100,000/= kumuona kuhani Musa Mbezi amuombee kwa Mungu wake.
Mimi nasema sitaona aibu au yeyote asijisikie hatia kutoa sadaka as long as nilipotoa mara ya kwanza sikufilisika na nitatoa kadiri kipato kinavyoongezeka Imani siyo kubembelezana
Kama wewe unaweka rules mwenyewe alafu hauzifuati utapata wapi uwezo wa kuniambia mimi nishike amri zako au za Mungu?