Achana na hii nadharia ni ya uongo.Gerezani wanahesabu usiku na mchana kama siku 2. So miaka miwili ni kama mwaka hivi
Siyo 1/3?Gerezani hawahesabu usiku na mchana, mfungwa anapofungwa anatumikia 2/3 ya kifungo chake, sio Tanzania tu, Duniani kote iko hivyo, Kama umehukumiwa miaka 30, utatumikia miaka 20 tu
Shukrani mkuu, uko sahihi, nimerekebisha tayari mkuuSiyo 1/3?
HahahaPole sana,kwavile ulifugwa kwa hasira zako na siyo kwa kuonewa naona sasa umejifunza,kisasi kizuri ni kutumia uchawi maana hakuna kesi wala ushaidi.
Kwa lugha nyepesi ni kama kifo kinavyokuja tu.Jela tumejengewa wanaume.
Siku ya kuingia itaanza kama siku nyingine bila hata dalili
Mwamba tatizo ngome ukiingia kama kupotea unapotea kweli usichukulie simple!!!Mkubwa uoga wa kwenda gerezani umewafanya wengi kupata umaskini wa kuwatosha
Kwahiyo alipojaa mtegoni ulimkisi ma K ya kutoshaKatika maisha ya utafutaji huwa tunapitia mambo mengi sana vikwazo,dhuluma,wivu, na mambo kadha wa kadha. Leo nitaeleza mambo mawili yanayotufanya/yatakayotufanya tujikute mwibani,ngombe au ukipenda sema gerezani. Hasira. Hasia za kutofurahia jambo fulani,mhemuko unasababisha kutokubaliana na jambo fulani mwaka jana January ya 2021 nilikua namalizia kupona majeraha niliyoyapata porini.Kuna rafiki yangu nlimkopesha zaidi ya milioni moja na laki nne aliposkia naumwa alimwambia msela wangu mwingine bora nife hakuja kabsaa kunisalimia nilipopata nafuu kumcheki kwenye cm hapokei nkaplot revenge akaingia mtegoni nikafanikiwa. Nakumbuka nlimjeruhi sana ikabidi awahishe ICU Mount Meru.Nilitorokea Manyara ila nilikamatwa nkarudishwa Chuga ghafla nkajikuta Kisongo rumande kesi ikatajwa bahat jamaa afya ikazidi imarika ila msala familia yake ina mwanasheria kesi ikasikilizwa mfululizo nkala miaka miwili na faini nkajikuta na gwanda za orange Kisongo miezi mitatu nkahamishiwa Tanga maweni msoto wa pale siwezi kuelezea wandugu.Marafiki walinisusa maza alipata presha na sukari baada ya kuja kunisalimia hakurudi tena.Ndugu zangu tupunguze hasira tujiepushe na wana wasiowaaminifu watatugharimu. Tamaa. Kupenda kuwa na vingi iwe halali au sio halali pesa,mali na mengine.Asilimia kubwa ya waliofugwa tamaa zimewaponza wengi hawakubali wanasema wamesingiziwa ila ukisikiliza kisa unaelewa jamaa ana makosa.Tamaa zimefanya wengi wafugwe vifungo virefu na kufanya familia zao ziishi kwa shida.Kuna jamaa alinihadithia kwamba alikua na rafik zake wawil waliua mtu wakampa lak mbil afiche bunduki ile iliyohusika kuua walipokamatwa wauaji kubanwa bunduki ipo wapi wakaenda na mapai kwake jamaa wale walihukumiwa kunyongwa kwakua yeye alishiriki kuficha bunduki akapewa miaka 20 na kushiriki kuficha mauaji akapewa miaka 5 jumla 25 kwa tamaa ya laki mbili tu yupo maweni hadi kesho jamaa kakata tamaa sana mawazo daily kazi hawez kufanya kila siku shambani au kwenye kokoto lazma achezee fimbo za nyapara. Ndugu zangu nawasihi tumuombe Mungu atuepeshe na tamaa hivi tunavyovimiliki kihalali tuviendeleze tutaishia Kisongo,Maweni, Songwe na Kitai tutasulubika sana.Siku unaingia gerezani utakutana na upekuzi usioelezeka utajipa moyo utatoka kesho ila wiki mwezi,mwaka vitaisha ukiwa na orange zako na kipara jumlisha kaz mlima na msosi mbovu mara moja kwa siku utafanya wazazi na ndugu zako waugue kisa wewe.Nashukuru Mungu nimetoka maza npo nae na chalii yangu ndio naishi nao sasa hivi mchumba wangu alinikimbia ila fresh maza na mwanangu wananitosha kwa sasa hadi mbeleni nitaamua mengine nlipotea njia ila nmerudi kwenye njia sikati tamaa nitaishi upya ila nitakua na marafik wachache mno wana sio wana wakuuuu. Asanteni na karibuni kwa mengine mengi.
Hawahesabu usiku na mchana bali Jeshi la Magereza limepewa mamlaka ya kupunguza 1/3 ya kifungo kwa kila mfungwa mwenye namba zinazohesabika,,hapa namaanisha kwamba wafungwa wa maisha na kunyongwa punguzo hilo haliwahusu!!! Hivyo dhana kwamba wanahesabu usiku na mchana siyo kweli!!! Kwamfano mtu aliyehukumiwa miaka 10 ikiondolewa 1/3 ya kifungo hicho inabaki kama miaka 7Gerezani wanahesabu usiku na mchana kama siku 2. So miaka miwili ni kama mwaka hivi
Ni 1/3Siyo 1/3?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kama kweli aisee ,umeongea kitu fulan nahisi nimejifunza kituPole sana,kwavile ulifugwa kwa hasira zako na siyo kwa kuonewa naona sasa umejifunza,kisasi kizuri ni kutumia uchawi maana hakuna kesi wala ushaidi.
Pole sana mwamba, hii dunia tu dahDuh pole sana! Yaani me nimekaa mahabusu ya Korogwe magereza miezi miwili kwa kesi ya kuvamiwa kwenye lindo na mali kuibiwa, yaan nilitengwa na ndugu jamaa na marafiki.....ila yote ni yote magereza sio sehem nzuri, tuishi kwa amani na upendo uraiani....wana sio watu
Pole sana mwambaMimi mwaka 2015 nilikua narud home majira ya saa 8 usiku nilitoka kuchek mechi nikakatiza nje kwenye yard moja ya magari walinzi wa pale wakaniweka mtu kati wakinituhumu mm ni mwizi, lakini mm binafsi tangu nizaliwe sijawahi kuiba mali ya mtu.
Nilijitetea lakin jamaa wakaning'angania nilikuja kugundua wale walinzi waliibiwa usiku wakiwa wamelala Sasa kwakua walikua wamefanya uzembe ikabidi watege nje ya geti na wamkamate mtu yeyote atakae katiza ndo nikawa nimeangukiwa na jumba bovu, maboss wao walikuja usiku wakapiga simu polisi nikaja kuchukuliwa lakini niliwatamkia wale walinzi kuwa "hii mnayo nifanyia ni dhulma na hata mioyo yenu inatambua ukweli kuwa Mimi siyo mwizi ila mmeniangushia jumba bovu tu Mungu yupo"
Yale maneno yaliwagusa sana had wale polisi waliokuja kunichukua, kwenye gar wakanihoji nikwasimulia jinsi nilivyotengenezewa mazingira wakaelewa lakin wakaniambia dogo sis tupo kazin ila usijali ukweli utabainika nikatupwa lockup kesho yake mahakamani
Nilikaa mahabusu gerezani wiki mbili mwsho wa siku nilikuja kugundulika sina hatia nikaachiwa nikasema yote kheri siyo kila anaeenda jela ana hatia.