Katika maisha ya utafutaji huwa tunapitia mambo mengi sana vikwazo,dhuluma,wivu, na mambo kadha wa kadha. Leo nitaeleza mambo mawili yanayotufanya/yatakayotufanya tujikute mwibani,ngombe au ukipenda sema gerezani. Hasira. Hasia za kutofurahia jambo fulani,mhemuko unasababisha kutokubaliana na jambo fulani mwaka jana January ya 2021 nilikua namalizia kupona majeraha niliyoyapata porini.Kuna rafiki yangu nlimkopesha zaidi ya milioni moja na laki nne aliposkia naumwa alimwambia msela wangu mwingine bora nife hakuja kabsaa kunisalimia nilipopata nafuu kumcheki kwenye cm hapokei nkaplot revenge akaingia mtegoni nikafanikiwa. Nakumbuka nlimjeruhi sana ikabidi awahishe ICU Mount Meru.Nilitorokea Manyara ila nilikamatwa nkarudishwa Chuga ghafla nkajikuta Kisongo rumande kesi ikatajwa bahat jamaa afya ikazidi imarika ila msala familia yake ina mwanasheria kesi ikasikilizwa mfululizo nkala miaka miwili na faini nkajikuta na gwanda za orange Kisongo miezi mitatu nkahamishiwa Tanga maweni msoto wa pale siwezi kuelezea wandugu.Marafiki walinisusa maza alipata presha na sukari baada ya kuja kunisalimia hakurudi tena.Ndugu zangu tupunguze hasira tujiepushe na wana wasiowaaminifu watatugharimu. Tamaa. Kupenda kuwa na vingi iwe halali au sio halali pesa,mali na mengine.Asilimia kubwa ya waliofugwa tamaa zimewaponza wengi hawakubali wanasema wamesingiziwa ila ukisikiliza kisa unaelewa jamaa ana makosa.Tamaa zimefanya wengi wafugwe vifungo virefu na kufanya familia zao ziishi kwa shida.Kuna jamaa alinihadithia kwamba alikua na rafik zake wawil waliua mtu wakampa lak mbil afiche bunduki ile iliyohusika kuua walipokamatwa wauaji kubanwa bunduki ipo wapi wakaenda na mapai kwake jamaa wale walihukumiwa kunyongwa kwakua yeye alishiriki kuficha bunduki akapewa miaka 20 na kushiriki kuficha mauaji akapewa miaka 5 jumla 25 kwa tamaa ya laki mbili tu yupo maweni hadi kesho jamaa kakata tamaa sana mawazo daily kazi hawez kufanya kila siku shambani au kwenye kokoto lazma achezee fimbo za nyapara. Ndugu zangu nawasihi tumuombe Mungu atuepeshe na tamaa hivi tunavyovimiliki kihalali tuviendeleze tutaishia Kisongo,Maweni, Songwe na Kitai tutasulubika sana.Siku unaingia gerezani utakutana na upekuzi usioelezeka utajipa moyo utatoka kesho ila wiki mwezi,mwaka vitaisha ukiwa na orange zako na kipara jumlisha kaz mlima na msosi mbovu mara moja kwa siku utafanya wazazi na ndugu zako waugue kisa wewe.Nashukuru Mungu nimetoka maza npo nae na chalii yangu ndio naishi nao sasa hivi mchumba wangu alinikimbia ila fresh maza na mwanangu wananitosha kwa sasa hadi mbeleni nitaamua mengine nlipotea njia ila nmerudi kwenye njia sikati tamaa nitaishi upya ila nitakua na marafik wachache mno wana sio wana wakuuuu. Asanteni na karibuni kwa mengine mengi.