Mimi naamini mkulu ana "LIST" mpaka ya mawaziri atakaowachagua ameiandaa. Kuna watu ambao hawapo bungeni wala hawajawahi kuwa na mawazo ya kuwa wabunge, wataambiwa wakachukue "FORM" wagombee (ambao hatuwategemei). Na pia sura zilizokuwepo bungeni nyingi hazirudi (acha wajifanye wanasifia kila kitu, wajipange kufa njaa mtaani - watashangaa watakavyokatwa majina yao).
Bunge lijalo kama mkulu atachukua nchi basi litakua la vibaraka wake tu, ambao ameshawapanga. Hawa wana lumumba waliokuwa bungeni wajiandae kutafuta "AJIRA MTAANI".
Bunge litapitia "OVERHAUL REPLACEMENT" ya hali ya juu, haijawahi kutokea. Kila mtu atakaeingia bungeni safari hii sura zitakua ni "MPYA" itakua kazi yao ni "KUSIFIA NA KUTUKUZA TU". Na wengi watakua ni "VITENGO MAALUM (Watu Wasiojulikana)".
CCM mjipange na mpangike, maana bado hamjatibiwa "WENDAWAZIMU VICHWANI". Muda wenu kushughulikiwa sasa akili ziwakae sawa, na mtakumbuka maneno ya "BERNAD CAMILUS MEMBE" ya kukatwa mkia.