Mambosasa ajibu maswali ya Rais Magufuli kuhusu kutekwa Mo Dewji

Mambosasa ajibu maswali ya Rais Magufuli kuhusu kutekwa Mo Dewji

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuibua maswali juu ya tukio la kutekwa Mfanyabiashara Mohamed Dewji Kamanda wa Polisi Dar es salaam Lazaro Mambosasa amejitokeza na kusema yeye alishamaliza kazi yake.


Mambosasa amesema baada ya yeye kumaliza kazi yake alikabidhi kwa viongozi wake wa juu na kwa sasa wanaojua kinachoendelea ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ambaye anatakiwa kutoa taarifa za uchunguzi zilizowasilishwa kwake.

Mambosasa amesema, “kuhusu maelekezo ya Rais aliyoyatoa kuhusu kutekwa kwa Mo, maadamu aliyatoa mbele ya Mkuu wetu wa Jeshi la Polisi na DCI ambao walikuwepo, jalada hilo lilishafika kwao, huko ndiko wanakojua kinachoendelea".

“Mimi jukumu langu lilishakwisha kwa hiyo ni suala la maamuzi ya juu kuhusu hatua zilizofikiwa kwenye jalada hilo", ameongeza Kamanda Mambosasa.

Mapema juzi Ikulu akiwaapisha Makamshna wa juu wa Jeshi la Polisi, Rais Magufuli alisema, "Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali, tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa."
 
Kwetu sisi wataalam wa Lugha na itifaki za Kiserikali, kauli ya mambo sasa ni utovu wa nidhamu si tu kwa Mkuu wa nchi Bali kwa Amiri Jeshi Mkuu.

Mambo sasa alipaswa kusema "maneno yaliyosemwa na Mkuu ya nchi si ya kupuuzwa bali yanapasa kitutafakarisha kama kuna sehemu tumekosea au tulikosea tujisahihishe". Hiyo ingekuwa kauli ya Afisa wa Jeshi kwa amiri Jeshi Mkuu.

Otherwise Mambosasa anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki, tusubiri tuone!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juu kabisa si ni kwa amiri jeshi mkuu? Atoe majibu sasa kama kila kitu kipo kwake.
Halafu yeye si ana vyanzo lukuki vya kupata habari? Ya nini kusubiri kama sisi akina Pepsin tunaotegemea JF?
 
😂😂😂 kale ka wimbo kaccm sasa kumekucha jogoo limewikaaaaaa...
 
Kwa hiyo rais hayupo informed? By the way kuna mambo ambayo Mambosasa hajaya ongelea ambayo rais aliya lalamikia.
1. Mazingira ya upatikanaji ya mtekwaji
2. Mambosasa kuonekana anakunywa chai na mtekwaji.
 
Back
Top Bottom