Mambosasa ajibu maswali ya Rais Magufuli kuhusu kutekwa Mo Dewji

Kujua kitu cha kusema, wakati sahihi na namna ya kukisema ni taaluma muhimu sana.
Sasa kama kuna wakubwa zake anapopaita huko juu, si wao ndio wangejibu hizo tuhuma za mkuu? Vinginevyo kama aliulizwa yeye binafsi.
 
Yale Yale ya "maagizo kutoka juu"

Ila kamanda issue ilikuwa ni communication iliyojaa uwongo mweupe kabisa. ....hiyo ndio hasa hoja ya JP..... issue ya mafile ni nyingine kabisa.....
Unadhani watanzania wote ni wajinga hivo??...jibu swali
 
IMG_20181022_123841_381.jpg
tapatalk_1538484647045.jpeg
 
Siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuibua maswali juu ya tukio la kutekwa Mfanyabiashara Mohamed Dewji Kamanda wa Polisi Dar es salaam Lazaro Mambosasa amejitokeza na kusema yeye alishamaliza kazi yake.

Mambosasa amesema baada ya yeye kumaliza kazi yake alikabidhi kwa viongozi wake wa juu na kwa sasa wanaojua kinachoendelea ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ambaye anatakiwa kutoa taarifa za uchunguzi zilizowasilishwa kwake.

Mambosasa amesema, “kuhusu maelekezo ya Rais aliyoyatoa kuhusu kutekwa kwa Mo, maadamu aliyatoa mbele ya Mkuu wetu wa Jeshi la Polisi na DCI ambao walikuwepo, jalada hilo lilishafika kwao, huko ndiko wanakojua kinachoendelea".

“Mimi jukumu langu lilishakwisha kwa hiyo ni suala la maamuzi ya juu kuhusu hatua zilizofikiwa kwenye jalada hilo", ameongeza Kamanda Mambosasa.

Mapema juzi Ikulu akiwaapisha Makamshna wa juu wa Jeshi la Polisi, Rais Magufuli alisema, "Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali, tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa."
kuanzia baba mwenye nyumba wote wanafiki tu wanajuana
 
Mmmmh anamjibu amiri jeshi mkuu? Haya sawa
 
Kiofisi ni vizuri boss au junior kuwasiliana kiofisi kulikoni kujibizana au kutuhumiana hadharani .Naona kuna kitu hakiko sawa.Public sio ofisi.Mafaili yapo boss aandike junior ajibu.Haya mambo ya kuanikana hadharani na kujibizana hadharani kati ya mabosi na ma subordinate wao ni ukosefu wa nidhamu za kiofisi na lazima ukataliwe usiote mizizi . Taratibu za mawasiliano ya kiofisi yaheshimiwe na yatumike kwa wote mabosi na juniors.Kitu haliko sawa uliza kiofisi ujibiwe na junior kama kuna kitu hukioni sawa kiekezee kiofisi.Ndio maana vyuo vyote hufundisha business communication kwa kozi zote za sayansi na Arts ili zitumike zaidi
 
Back
Top Bottom