Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee kuandamana kudai katiba mpya ni kuvunja sheria basi naandaa maandamano ya kutaka JPM aongezewe muda wa kukaa madarakani.Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuachia kwa dhamana Askofu Emmaus Mwamakula wa kanisa la Uamsho la Moravian baada ya kufanya upekuzi nyumbani kwake.
Taarifa za kushikiliwa Mwamakula zilitolewa na polisi jana Jumatatu Februari 15, 2021 kupitia mtandao wa kijamiii kabla ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuthibitisha kumshikilia.
Akizungumza leo Jumanne Februari 16,2021 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema baada ya jeshi hilo kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake limemuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
“Tumempuuza na baada ya kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake, mchana huu tumemuachia kwa dhamana baada ya kutimiza masharti,” amesema.
Awali polisi walieleza kumshikilia kumshikilia Mwamakula kutokana na taarifa aliyoichapisha mtandaoni iliyokuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuandamana kushinikiza kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.
Mwananchi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]View attachment 1703776
Hapo Mambosasa kajichanganya, au amechanganyikiwa. 🙈🙈🙈Mkuu Mambosasa kama umempuuza , masharti ya dhamana yamefuata nini?
kwanza kwa mtu mwenye makandokando kama Mambosasa kutuma mamluki wake kwenda kumpekua Mcha Mungu Mwamakula ni laana kwa nchiHapo Mambosasa kajichanganya, au amechanganyikiwa. 🙈🙈🙈
Kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ni kosa la jinai awamu hii???
Askofu ameyaita matembezi ya hiari sio maandamano hao wanaosema maandamano ni kwa kutafuta tu namna ili askofu aonekane kavunja sheriaSio kosa kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, madai hayo sanaaa... hapo issue hamasisho la maandamano. Kitu maandamano polisi hawataki kusikia
Nilishasema yule Babu Mamboosasasa kichwani kweupe..si ndo yule aliyekaa na Mo wakanywa chai baada ya kutekwa? Rais akamuumbuaUmemkamata, mmemuweka ndani, mmeenda kumpekua nyumbani kwake, mkamuachia kwa dhamana, halafu jitu moja kubwa la mwili linahitimisha kwa kusema eti wamempuuza!!!
Mkuu Mambosasa kama umempuuza , masharti ya dhamana yamefuata nini?
Uchwara wewe hapo Lumumba usiyejitambua!Huyo askofu uchwara kaamua kutumia hii njia ili kujiongezea umaarufu kanisani kwake ili kapu lijae
Pongezi kwa jeshi la polisi kumshughulikia na kumpuuza
Mambosasa , kwani mmempuuza mmemkuta na kondom?“Tumempuuza na baada ya kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake, mchana huu tumemuachia kwa dhamana baada ya kutimiza masharti,” amesema.
Haka kaaskofu kakimatwa unalalamika, kakiachiwa vile vile unalalamika; wewe vipi wewe?Mkuu Mambosasa kama umempuuza , masharti ya dhamana yamefuata nini?