Mambosasa: Tumempuuza Mwamakula na kumuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana

Mambosasa: Tumempuuza Mwamakula na kumuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana

Mnasema corona ipo serikali haichukui hatua,

Halafu muda huo huo mnataka kukusanya watu wakadai katiba mpya,

Au mikusanyiko wakati wa shughuli zenu tu ndio hakuna maambukizi??

Inashangaza Sana.
Ndiyo maana alisema ni matembezi ya hiari ya kila kundi lisilozidi watu 20. Wewe unafikiri Askofu ni mjinga kama wanaCCM (TWAWEZA)?
 
Mambosasa mwili mkubwa akili za kuvalia suluali tu. Anaongee upuuzi tu. His days are numbered. Huwezi ukawa unaua, unatesa na unaonea halafu uwe na mwisho mzuri.
 
Hivi mkienda kupekua watu nyumbani mnadhani mtakuta nini huo mfumo mlioiga ni mbaya kuwahi kutokea vitu ambavyo havieleweki mnavizingatia kweli mnaacha kupambana na Corona/ umasikini unaotuzunguka mpo busy na kauli za mtandaoni...
Halafu wanajua kabisa kuwa yule ni askofu,hana silaha,wala hatumii bangi kwamba wangeikuta nyumbani kwake,zaidi ya biblia.

Wanatukamia sana kodi lakini wanaitumia Kodi yetu vibaya.
 
Baba Askofu, ukuu wa Mungu ukae nawe kwa sababu umehesabiwa pamoja na wenye hatia pasipo hatia.

Walaaniwe waliojipa mamlaka ya Mungu, wasiotaka kuhojiwa, kushauriwa, kukanywa wala kukosolewa. Wamejitengenezea Mungu wao wa sanamu, Mungu wa Tanzania, ndiye wanayemwabudu na kumwimbia nyimbo za sifa katika kila jambo, liwe jema au uchafu.

Bwana Mungu wetu iangamize mamlaka hii ya shetani na mawakala wake wote hata kizazi cha nne. Maana ni wewe pekee usiyehojiwa, usiyehitaji kushauriwa lakini unayeliliwa na kuombwa usiku na mchana, na unajibu wakati ufaao.
 
Ameni
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuachia kwa dhamana Askofu Emmaus Mwamakula wa kanisa la Uamsho la Moravian baada ya kufanya upekuzi nyumbani kwake.

Taarifa za kushikiliwa Mwamakula zilitolewa na polisi jana Jumatatu Februari 15, 2021 kupitia mtandao wa kijamiii kabla ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuthibitisha kumshikilia.

Akizungumza leo Jumanne Februari 16,2021 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema baada ya jeshi hilo kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake limemuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

“Tumempuuza na baada ya kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake, mchana huu tumemuachia kwa dhamana baada ya kutimiza masharti,” amesema.

Awali polisi walieleza kumshikilia kumshikilia Mwamakula kutokana na taarifa aliyoichapisha mtandaoni iliyokuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuandamana kushinikiza kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Mwananchi
Hivi Shetani huwa anampuuza Mungu au Mungu siku zote ndiyo humpuuza Shetani?
 
Masharti ya dhamana ya nn ilihali mmempuuza?
Mambosasa hajui maana ya kupuuza... tafuta neno musharafu hilo haliswii hapo!!
 
Uwezo wako wa kufiri ni mdogo sana kuhusu mitandao

Wewe ndio ume prove kwamba ni KIDU(Kiwango Duni) ,Polisi kila siku wanasema hawafanyii kazi habari za kwenye mitandao iweje Mambo sasa akarupuke na kwenda kumkata Askofu kwa habari za kwenye facebook?
 
Huyu kamanda aelewe kina maisha baada ya ukamanda wake kuisha. Hajatumia lugha ya staha eti " tumempuuza" yule ni kiongozi wa dini.
 
Kiintelijensia hakuna taarifa inayo puuzwa ilimradi tu inatishia uvunjifu wa amani (ambao ni jukumu la msingi la polisi).... Ingawa baada ya upelelezi wa awali unaweza kubaini uwezo wa utekelezaji wa kitisho cha uvunjifu wa amani wa mtuhumiwa kuwa si halisi.

Hapo ndio dhana ya kumpuuza huundwa ili kuarifu umma ambao uwenda walikuwa na nia au wazo la kushiriki, kuunga mkono au kuteleza wito wa kitisho au madai kughaili na kuupuuza uwezo wa mwamasishaji.

Ni issue ya kiusalama zaidi au kiintelijensia ambayo Kamanda Mambosasa ameibua na kuipandikiza kwa umma kwamba wapo macho na kila hatua na anaachiwa Baba Askofu kwa dhamana ambayo bila shaka itakuwa na sharti la kuwasili na kusaini kwenye kituo cha polisi kila siku ili kunyong'onyeza nia yake.

Ni swala la saikolojia ya kiusalama
 
Bora angekaa kimya tu kwa sababu anajidhalilisha mwenyewe kwa kudhani anamdhalilisha aliyewaweka bize kwa masaa kadhaa...

Mungu tunusuru watanzania.
 
Back
Top Bottom