Mambosasa: Tumempuuza Mwamakula na kumuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana

Hawa ni viongozi wa polisi akili zipo hivi!!
 
Aisee kuandamana kudai katiba mpya ni kuvunja sheria basi naandaa maandamano ya kutaka JPM aongezewe muda wa kukaa madarakani.
 
Hii ni lugha gani anatumia kiongozi huyu?

Kwani angesema tu, tumemwachia kwa dhamana angepungukiwa na nini?

Huu ndiyo hasa unaoitwa "ulevi wa madaraka"....

Jamaa anazungumza tu na amesahau kabisa kuwa " cheo ni dhamana" unacho leo kesho ni raia wa kawaida...

MamboSasa, unasubiriwa huku uraiani siku umetemeshwa cheo hicho na mgawa vyeo Yehova Mungu mtakatifu....
 
Kama alikuwa anahamasisha maandamano,nyumbani kwake walienda kupekua waandamananji!
Wakupuuzwa hapo ni Mambo ss
 
Kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ni kosa la jinai awamu hii???


Sio kosa kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, madai hayo sanaaa... hapo issue hamasisho la maandamano. Kitu maandamano polisi hawataki kusikia
 
Sio kosa kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, madai hayo sanaaa... hapo issue hamasisho la maandamano. Kitu maandamano polisi hawataki kusikia
Askofu ameyaita matembezi ya hiari sio maandamano hao wanaosema maandamano ni kwa kutafuta tu namna ili askofu aonekane kavunja sheria
 
Mnasema corona ipo serikali haichukui hatua,

Halafu muda huo huo mnataka kukusanya watu wakadai katiba mpya,

Au mikusanyiko wakati wa shughuli zenu tu ndio hakuna maambukizi??

Inashangaza Sana.
 
Hivi Jeshi la Polisi limekosa kabisa mtu sahihi wa kuongoza Kanda maalum Dar es salaam kuliko huyu mchumia tumbo anayewaza kumharibia IGP wake kila uchao ili ateuliwe yeye?
 
Umemkamata, mmemuweka ndani, mmeenda kumpekua nyumbani kwake, mkamuachia kwa dhamana, halafu jitu moja kubwa la mwili linahitimisha kwa kusema eti wamempuuza!!!
Nilishasema yule Babu Mamboosasasa kichwani kweupe..si ndo yule aliyekaa na Mo wakanywa chai baada ya kutekwa? Rais akamuumbua
 
Kumbe ile kauli waliyosema "tumemkamata mtu anayejiita askofu" haikua ya bahati mbaya na sasa wanasema "tumempuuza"....hawa wapuuzi hii kitu watakuja kulipa muda ukifika.
 
Chapter one ya Demokrasia inataka kuvumiliana katika kutoa mawazo au kauli.
Ukishindwa basics hizo za Demokrasia unaenda sehemu nyingine ya kutunisha misuri,yaani kinyume na umma.
Haya mambo ya kutaka kujua haki yako,au kutaka uwepo wa katiba mpya ni haki ya watawaliwa.
Lakini nina shaka kama baadhi ya viongozi wetu walipitia somo la urai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…