Mambosasa: Tumempuuza Mwamakula na kumuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana

Huyo askofu uchwara kaamua kutumia hii njia ili kujiongezea umaarufu kanisani kwake ili kapu lijae

Pongezi kwa jeshi la polisi kumshughulikia na kumpuuza
Anamzidi Gwajima kwa huo uchwara? Binafsi namuunga mkono huyo Askofu Mwamakula kwa ujasiri wake wa kuwasemea Mamilioni ya Watanzania waliochoshwa na utawala kandamizi na wa kidikteta, kibabe, kikatili, kifisadi,kibaguzi ma wa kidhalimu unao fanywa na CCM.

Wala hahitaji umaarufu wowote! Zaidi anaonekana tu kama Mtu Shujaa machoni kwa Watanzania wengi Wazalendo na Wapenda Mabadiliko ya kweli ya kisiasa na kiuchumi nchini. Ni kweli tunahitaji Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ili tuone kama kweli nyinyi mi CCM mnapendwa na Watanzania, au mnashinda tu Uchaguzi kwa hila na ghiliba.
 
Tumempuuza na kumwachia kwa dhamana. Kupuuza ni kwamba wamemuona mpuuzi au Hana maana sasa mpuuzi ana dhamana? Huyu ana mawili ni kumwachia bila masharti au kumuweka ndani, Bahati nzuri sio mvaa kanzu maana angesota gerezani hadi tukamsahau maana bila soni angetangazwa ni Alshabab
 
Silo hawezi toa kauli kama hizi anajitambua, licha ya kuzimika kufanya mambo ya ajabu!
 
Sasa mlinda katiba asitake kusikia kitu cha kikatiba kwa misingi ipi? Sasa si wakatoe mapendekezo kuwa katiba imezingua hapo
 
Huyo askofu uchwara kaamua kutumia hii njia ili kujiongezea umaarufu kanisani kwake ili kapu lijae

Pongezi kwa jeshi la polisi kumshughulikia na kumpuuza
Wamuache tu aandamane. Hajui anapotoka wala anapokwenda
 

wanatafuta mbinu za kuwa IGP ndiyo maigizo yote haya
 
Hivi mkienda kupekua watu nyumbani mnadhani mtakuta nini huo mfumo mlioiga ni mbaya kuwahi kutokea vitu ambavyo havieleweki mnavizingatia kweli mnaacha kupambana na Corona/ umasikini unaotuzunguka mpo busy na kauli za mtandaoni...
 
Huyu Mzee ana hitilagu
 
unajua nchi hii watu mpaka watumwe ndio wafanye ujinga wao! jamani mambosasa kumpekua askofu unatafuta nini, biblia, joho lake au msalaba! sababu katiba mpya muhimu sana!
 
Huu uandishi wa kurudia-rudia kichwa cha habri huwa unanibore sana. Naamini wana taaluma ya uandishi ndivyo hufundishana huko vyuoni mwao lakini inakuwa kero kwa msomaji kwani unakuta paragraph zote nne ni kichwa cha habari kinarudiwa miwsho wa siku habari yenyewe fupi kama njugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…