Mamelodi Sundowns wako Overrated

Okay so unadhani Mamelodi hawjalitambua hilo kila mwaka watakua wanarudia makosa yale yale?

Kuhusu kujifunza kwa makosa yao. Hilo jibu wanalo wenyewe.

Mimi point yangu ni simba ana nafasi kubwa ya kupita kama akipangiwa Mamelodi robo fainali.

Ila Simba huyu huyu ana nafasi ndogo sana ya kupita kama Akipangiwa Esperence ama Waydad Casablanca.

Sababu kuu hizo timu ni hatari kuliko mamelodi. Record zao Caf zinajieleza kwa uwazi. Na rekodi za mamelodi caf zinajieleza kwa uwazi
 


Nenda katazame mechi zote mbili za mwaka huu 2023 zilizochezwa caf kati
Mamelodi vs Al hilal ya sudan.

Ya kwanza south africa

Na ya pili sudan

Jiulize Al Hilal na simba wana tofauti gani kiuwezo.
 
Esperes Tunis vS Simba.
 
Tumekuuliza hao Masandawana wenye mbinu za maana, ndani ya hii misimu mitano ya CAFCL waliwahi kuvuka robo fainali?

Kama hawakuvuka huoni kama unawapa ukubwa ambao kimsingi hawana?
 
Simba angekua anacheza huo mpira unao usema angekua kafika final hata moja kumbuka mara mbili katolewa ni timu za SA (Orlando pirates na Kaizer Chiefs) wala sio Northern huko kabla ya kujigamba kumtoa Mamelodi ungejiuliza kwanini Simba hua anaishia robo?
 
Niambie hio nafasi kubwa kwa Simba kumfunga Mamelodi umei determine vipi? sababu kama ni clubs ranking Mamelodi wapo juu, statistics wapo juu wewe ulisha wahi hata kutoa draw na Al Ahly pale Cairo? tuachieni ujinga
Ile tu kuishia robo fainali misimu mitano mfululizo hatua ambayo hata Simba Sc anaifikia, itoshe kukufahamisha kwamba mnawakuza for nothing.
 
Mimi ni Simba lialia ila kiukweli wale jamaa ukiwaangalia wanajua Kuna mtu anaitwa Maema ,Mailula na Peter wale jamaa ndo injini pale kwa huu mpira wanaocheza labda Raja kidogo msimu huu ndo wako sawa ila jamaa wako far beyond us.
Ilikuwaje wakawa wanaishi robo fainali kwa misimu mitano mfululizo?

Haohao mwaka jana walitolewa na Petroleos, ilikuwaje?
 
Hata msimu uliopita mlidai yupo kwenye kiwango cha juu mpaka pale alipotolewa.
 
Unataka tujiulize kwanini Simba Sc huwa anaishia robo, ila hautaki Mamelod wadharauliwe kwa kuishia kwao robo fainali misimu mitano mfululizo.

Huoni kama upo biased?
 

Simba ndio uwezo wake ulivyo. Sio kama anaishia robo kwa bahati mbaya.

Na hata mamelodi tunamsema ni afadhali kwa simba sababu ndie kiwango chake kilivyo. Simba akisema asikutane na mamelodi ujue simba anaenda kukutana na Esperence ama wydad casablanca ambayo ni maji marefu zaidi ya mamelodi.

Mamelodi ndie mnyongee mnyongee katika timu zinazopaswa kupambana na simba robo fainali.

Hata timu ya taifa Tanzania tukiambiwa tuchague tucheze na Congo ama Morocco. Tutachagua Congo sababu hajatuzidi uwezo sana. Hatuna uwezo sawa na Congo ila tunaweza kushindana nae kuliko tukicheza na Morocco
 
Manara alikuwa sahihi sana, anyway ni mawazo yako na sina budi kuyaheshimu..
 
Na simba katwaa mara ngapi?
 
Brother acha ushabiki kuwa realistic Simba hana uwezo wa Ku battle na Mamelodi Sundowns labda itokee tu maajabu ambayo kwenye football yapo lakini kwa quality, experience, technical bench hizi timu ni mbigu na aridhi
Wewe ni shabiki wa timu gani mkuu ?..
 
Ile tu kuishia robo fainali misimu mitano mfululizo hatua ambayo hata Simba Sc anaifikia, itoshe kukufahamisha kwamba mnawakuza for nothing.
Hawakuzwi ila uwezo unaongea at least wao wana kombe
 
Nenda katazame mechi zote mbili za mwaka huu 2023 zilizochezwa caf kati
Mamelodi vs Al hilal ya sudan.

Ya kwanza south africa

Na ya pili sudan

Jiulize Al Hilal na simba wana tofauti gani kiuwezo.
A very lame comparison. Hapa tunawalinganisha Mamelodi na Simba, sio Mamelodi na Al Hilal.

Lakini pia hata tukiamua kufanya hivyo unavyotaka, kwani hukuona malalamiko kwamba Mamelodi wanafanya match fixing kwa kuwalegezea Al hilal makusudi ili Al Ahly atoke?

Ikitokea Mamelodi akapangiwa Simba, basi ni do or die kind of a match kwa Mamelodi. Usitegemee wacheze kama walivyocheza na Al Hilal kwenye makundi ambapo wao tayari walikua na uhakika wa kufuzu!

Inahitaji kiwango cha juu sana cha kujitoa fahamu kuwaweka Mamelodi hawa, na Hii simba kwenye level moja!
 
Umeandika personal feelings ndugu yangu ila naomba siku moja ukae uangalie mechi zote walizocheza CAFCL Huu msimu afu uje uedit thread
Hakuna cha ku-edit mkuu, ndo uhalisia Mamelodi wako Overrated sana ukilinganisha na wanacho kionesha uwanjani, ni mara 10 ungeniambia Raja CA
 
Niambie hio nafasi kubwa kwa Simba kumfunga Mamelodi umei determine vipi? sababu kama ni clubs ranking Mamelodi wapo juu, statistics wapo juu wewe ulisha wahi hata kutoa draw na Al Ahly pale Cairo? tuachieni ujinga
Al ahly ya mwaka huu umeiona au unaongea tu kwa historia ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…