Mamelodi Sundowns wako Overrated

Mamelodi Sundowns wako Overrated

Baada ya kupata goli la kuongoza hao Mamelodi wakakosa umakini na kufikiri kwamba mpira umeisha wakaanza ubishoo na matokeo yake ndio yakatokea ya kutokea.

Walijisahau kwamba walikuwa wanacheza na bingwa mtetezi, sasa itabidi wajipange tena upya kwa msimu ujao maanake hamna namna.
 
Matokeo yao sio makubwa kama sifa zao.

Mfano leo wametolewa na waydad kwenye caf champions league .

Timu yenye sifa kama mamelodi haipaswi kuwa inatolewa tolewa kila msimu.
Wanaupiga mwingi sana ila tatizo lao ni kupoteza focus kwenye knockout stages mfano ni zile red card mbili walizopata first leg
 
Tulipokuwa tukilisema hili wengi waliona labda tuna wivu na hao wasauz

Ila kiukweli kabisa Mamelod Sundowns wapo overated sana kuliko uhalisia yaani ukisikia sifa wanazoipa unaweza fikiri ni tomu bora pengine kuliko hata Al Ahly au Wydad Casablanca kumbe ni timu ambayo fainali ya mwisho klabu bingwa waliiona 2016 miaka 7 huko iliyopita
 
Matokeo yao sio makubwa kama sifa zao.

Mfano leo wametolewa na waydad kwenye caf champions league .

Timu yenye sifa kama mamelodi haipaswi kuwa inatolewa tolewa kila msimu.
Unataka kusemaje kuhusu Wydad? Yaani una underrate timu moja ili ku justify mawazo yako kuhusu Timu nyingine. Tafuta hoja nyingine.
 
Tatizo haukuwa unajiamini, kosa lako lilikuwa ni lipi?
Mamelodi hawana bahati tu, ila mpira kama mpira nimewavulia kofia wana umwaga wa kutosha,, mpira mchezo wa wazi sote tunaona, jamaa wapewe maua yao.. Na ninaposema hawana bahati ndio kama hivyo wanaongoza beki wao anakuja anajifunga.
 
Mamelodi hawana bahati tu, ila mpira kama mpira nimewavulia kofia wana umwaga wa kutosha,, mpira mchezo wa wazi sote tunaona, jamaa wapewe maua yao.. Na ninaposema hawana bahati ndio kama hivyo wanaongoza beki wao anakuja anajifunga.
Mamelod wa mwaka huu hana tofauti na yule wa misimu mitano ya CAFCL iliyopita, hizi ndio hatua zake ambazo huwa anaishia. Msimu uliopita aliyolewa kijinga na Atletico Petroleos hapohapo kwao kwa kudraw kama alivyofanya jana.

Hakuwa na la nyongeza.
 
Mamelodi hawana bahati tu, ila mpira kama mpira nimewavulia kofia wana umwaga wa kutosha,, mpira mchezo wa wazi sote tunaona, jamaa wapewe maua yao.. Na ninaposema hawana bahati ndio kama hivyo wanaongoza beki wao anakuja anajifunga.
Hapana sikubaliani na ww timu za south africa hazina mpira wa kutumia nguvu kutaka kitu, wanapenda mpira wa show game yaan badala ya kutoa pasi moja mchezaji atapiga chenga atataka kupiga tobo kufinya vitu ambavyo mnaweza kucheza kama timu imeshashinda goal za kutosha ndo mnaanza mambo hayo
Gemu ile ilikuwa inamalizika kipindi cha kwanza maana walipata nafasi nne za kumaliza gemu lkn wakaleta ustaa na mbwembe hivyo mwaarabu alikuwa ameshajaa upepo na alikuwa amekubali lkn wakazidisha mbwembwe na mwisho mwarabu akatulia akarudi na akawatoa easy
 

Habari wakuu

Awali ya yote ningependa ku-declare interest kuwa nawataka Masandawana. Twende kwenye mada, imezuka mijadala mingi sana mitandaoni hususani kwa baadhi ya wachambuzi wakisema kuwa Mamelodi sundowns sio timu ya kuomba kukutana nayo. Wengine wakaenda mbali zaidi kusema kuwa ndio timu hatari zaidi.

Binafsi naheshimu ubora wa Mamelodi, nilipata wasaa wa kutizama game zao mbili tatu hususani ile game yao ambayo walimpiga Al ahly hamsa pale Africa kusini. Naomba niseme tu kwamba Mamelodi wako Overrated mno.

Nadhani ni kwa sababu ya kumnyanyapaa Al ahly ndicho kinachofanya watu wamzungumzie kiutofauti, ambapo obviously hajaanza leo toka kitambo al ahly anapotua Johannesburg basi Hamsa zina muhusu.

Lakini ni ukweli usiopingika kuwa al ahly pia msimu huu hayupo vizuri, kinacho mbeba ni uzoefu tu ila hana timu, nisingeshangaa angepigwa nje ndani na mnyama simba kama angepangwa group moja.

Turudi sasa kwenye mada yetu, Mamelodi sundowns pamoja na kuwa Overrated sana bado hana mpira wa kutisha, nachelea kusema kuwa hata Raja CA ni maji marefu kwa Mamelodi. Kingine nilichokiona kwa Mamelodi ni aina yao ya uchezaji ambao uko very identical na uchezaji wa simba yani pira biriani a.k.a Sambaloketo.

Hivyo ikitokea timu hizi mbili zikakutana, basi Africa na Dunia kiujumla itashuhudia mechi ya karne, yani historical match, hivyo niwatoe hofu wanasimba wenzangu ambao mmeanza kutishika na maneno ya waganga njaa kuhusu Mamelodi sundowns.

Binafsi sintoshangaa kabisa kama simba akimtoa Sundowns kwenye hatua ya Robo fainali au hatua yoyote tutakayo kutana nae.

Nguvu moja [emoji881]

Uzi wa zamani ila una ukweli mwingi
 
Back
Top Bottom