Mamelodi yaondolewa hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika na Wiliete

Mamelodi yaondolewa hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika na Wiliete

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wametolewa katika mashindano hayo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Wiliete SC ya Angola katika mchezo wa marudiano wa hatua ya pili ya awali, uliochezwa Oktoba 23, 2026.

MAMELOD 2.jpg
Matokeo hayo yanaifanya Wiliete kusonga mbele kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare tasa. Sundowns sasa imekosa nafasi ya kutetea taji lake, huku Wiliete ikifuzu hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Wiliete SC.webp
Mamelodi Sundowns walitwaa ubingwa wa CAF Champions League mwaka 2016 na 2026. Ubngwa wao wa pili waliutwaa Mei 24, 2026, baada ya kuifunga AS FAR ya Morocco kwa jumla ya mabao 2-1.

1792792862367.png
Yanga SC, wamefuzu hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, Oktoba 21, 2026, baada ya kuifunga CFFA ya Madagascar kwa jumla ya mabao 8-1.

Timu tano tayari zimefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) msimu wa 2026/27, huku timu nyingine zikitarajiwa kujiunga nazo baada ya hatua ya mwisho ya mchujo kukamilika. Timu hizo ni:

1. Young Africans (Yanga SC)
2. Petro de Luanda
3. Orlando Pirates
4. Wiliete SC
5. MC Alger

1792793665521.png

Huku Simba SC, ikitarajiwa kucheza na 15 de Agosto ya Equatorial Guinea Oktoba 25, 2026 mechi ya marudio baada ya mechi iliyochezwa Jumatano, Oktoba 21, 2026, katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Na Simba kushinda kwa mabao 6-1.

1792792928336.png

Kwa viwango walivyoonesha Kulwa na Doto, unaona Simba na Yanga zinaweza kutamba Afrika 2026 bila Al Ahly na Mamelodi Sundowns?
 
Yanga na Simba badonsana kushindana Afrika na kuwa na imani kurudisha kokbe nyumbani, tukubali tu kwamba timu zetu hizi zimwshuka kidogo kiwango kwa misimu hii miwili...

Ingekuwa vile vikosi vya hapo nyuma ndio vinakutana na mazingira haya ya sasa, kidogo tungekuwa na matumaini ya timu mojawapo kukimbiza...
 
Si ndio anaanzia hatua ya pili...

Ulitaka apewe qualification ya moja kwa moja makundi?

Ndio. Sababu yeye ni bingwa, ilitakiwa apewe kigezo cha ubingwa alitetee kombe.
 
Back
Top Bottom