JOHNGERVAS
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 1,487
- 2,599
Ubwabwa tu ndio watarekebishaCHAUMMA watarekebisha usihofu
kuna hawa wanaouza asubuh na had saa tatu inakuwa bado yaani ukihitaji uende kuanzia saa tano.Inategemea na mahali ulipo hapo dar, Kuna maeneo mbona huduma Kama supu ni 24/7 watu wanakesha.
Bongo ya ajabu sana kweli. alafu mtu kama huyo unakuta anatumia na maji ya mwmaposa eti apate wateja wengi wakati asubuh wateja kibao anawapoteza kwa uzembeBaadae wachina waki-take over wanaanza kulalamika
ni hatari sanaNa bado wanawasema watu wa Tanga kufungua biashara saa mbili
Hii ni kweli kabisa dar ukitaka bidhaa nunua jioni asubuhi ni shida kupata huduma labda usafiri
Na mtori/supu/makange/mapupu na vyote vitakaa sawaUbwabwa tu ndio watarekebisha
najua, ila kuna sehemu zile wanaofungua asubuhi ila asubuh yenyewe ni majangaKuna sehemu nyingine hapa Dar ni hakuna kulala.
Tanzania japo umaskini tumeletewa na ccm lakini sisi wenyewe bado ni shida nadhani vichwani kuna Makamasi na wala sio Ubongo.Au ndizi tayari lakini Supu bado kuna Jambo moja nashindwa Kuelewa hivi kama Mtu unauza Kifungua Kinywa na hadi saa tatu hujamaliza, nyie watu wa DSM huwa kwenu chai munakunywa saa ngapi?
HIvi ndio wafanyabiashara wetu wamekosa kabisa maarifa na kuendana na Muda?
Hapo ndio utaipenda Mbagala๐๐Kuna sehemu nyingine hapa Dar ni hakuna kulala.
Naungana na weweSHALLOM.
Nipo Dar kwa muda Kidogo ila kuna kitu kinanishangaza sana hasa kwa Dar maeneo ya wilaya ya Ubungo na maeneo mengine kuhusiana na suala zima la Uuzaji wa Vyakula hasa nyakati za asubuhi.
Ukipita Maeneo mengi wanayouzia KIfungua Kinywa kama Supu au mtori na n.k unakutana na Vituko sana Unafika sehemu inaweza kuwa ni saa tatu Asubuhi unaambiwa Supu bado, Au supu tayari lakini Chapati/ndizi bado.
Au ndizi tayari lakini Supu bado kuna Jambo moja nashindwa Kuelewa hivi kama Mtu unauza Kifungua Kinywa na hadi saa tatu hujamaliza, nyie watu wa DSM huwa kwenu chai munakunywa saa ngapi?
HIvi ndio wafanyabiashara wetu wamekosa kabisa maarifa na kuendana na Muda?
Imagine mtu umeamka zako na hangover usubiri supu hadi saa tano/
Au unawahi kwenda kwenye mishe mishe zako usubiri chai hadi saa tano?
Na ajabu mteja anapondoka kwa sababu ya Kukosa Huduma wala hawaonyeshi Kujutia chochote nikama wanafurahi kwamba Umeondoka.
Jambo la Mwisho hata ukienda Kula utaletewa baadhi ya Vitu vingine utaambiwa hamna labda ndizi/limao, pilipili nk utaambiwa mara zimeisha au bado hazijaandaliwa.
Kwa kumalziia unashangaa unaagiza tu hii Chai ya kawaida unaambiwa imeisha, hivi kuwasha Gas au kuchemsha chai inahitaji hata dakika Tano?
DSM maisha ya wafanyabiashara wengi ni kama wahudumu au wasaidizi wanaowaweka ni kam wanataka mshahara ila hawataki kazi unaenda bar unaomba Kuletewa kinywaji kinaisha unafukuza nzi nusu saa ndio unamuona mhudumu anjipitisha tena, na wakati mwingine unamuagiza kama naye humuagizii anaitosa meza yako hajali unachoingizia ofisi kwamba ndio kitakuwa mashahara wake.
Nirudi Dodoma sasa maana asubuh nikipita chako ni chako nakula supu na bia kadhaa ndio naenda kazini, pale mhudumu akikuletea kinywaji dakika tatu zikiisha anapita tena kukuulizia kama unaongeza. Anakuuliza na je unapenda huduma pendwa/ ee huduma ile yetu
Yaani umelipa Supu elfu 5 unaambiwa pili pili bado haijaletwa au Ndimu zimeisha jana๐๐๐๐Jambo la Mwisho hata ukienda Kula utaletewa baadhi ya Vitu vingine utaambiwa hamna labda ndizi/limao, pilipili nk utaambiwa mara zimeisha au bado hazijaandaliwa.
Rudia kauli yangu, " Kuna sehemu na sehemu" kama upo jijini dar es salaam hili unalosema sio kweli labda kama ni pembezoni mwa mji, Dar kubwa mkuu.kuna hawa wanaouza asubuh na had saa tatu inakuwa bado yaani ukihitaji uende kuanzia saa tano.