Mameneja wa bar, wamiliki wa majiko DSM muna shida gani?

Yaani umelipa Supu elfu 5 unaambiwa pili pili bado haijaletwa au Ndimu zimeisha jana😀😀😀😀
Kuna mahali nilikunywa supu wateja wanahitaji Pepsi na zipo zinaonekana kwenye friji ila unaambiwa mwenye funguo bado hajafika na hiyo ni saa nne! Yani mwenye bar hawezi kuwaamini watu wa jikoni awaachie ufunguo wawauzie watu soda! Ni upuuzi mtupu.
 
Kumbe tupo wengi tunaopata huu usumbufu mfano kwa Madale Montana, Joy, Deez,Musu, Mbuzi Online halafu hata Goba mfano Texas, Trindad,Triple B, Plan B.
Wote ni hovyo tu poor customer care tena ukienda uko simple ndio vina nyodo balaa
 
Kumbe tupo wengi tunaopata huu usumbufu mfano kwa Madale Montana, Joy, Deez,Musu, Mbuzi Online halafu hata Goba mfano Texas, Trindad,Triple B, Plan B.
Wote ni hovyo tu poor customer care tena ukienda uko simple ndio vina nyodo balaa
wanakuangalia kuanzia muonekana sio asee hatari sana
 
Pika kwako
 
Zamani kulikuwa na bar kinondoni kiria bar saa 12 na nusu supu tayari

Ova
Nilikuwa ninaitafuta hii comment.

Sipajui Kiria Bar, ila jina linasadifu kwamba boss ni Mchagga.

Siyo kwamba ninalisifia kabila langu, ila ninamaanisha kwamba Wachagga kwenye kazi tupo serious kuliko jamii nyingine.

Nimewahi kuwa na mzazi pale Hospitali ya Wilaya ya Ubungo.

Nilitoka asubuhi nikaanza kutafuta mtori kuanzia Baruti, ilipo Hospitali, nikaenda kuupatia pale Lego, Shekilango (Kwa Wachagga).

Nimeona mtoa mada kawasifia Chako ni Chako kwa kuwahi kuandaa supu. Jibu ni kwamba pale napo ni kwa Wachagga.
 
Kiria bar ilikuwa kila kitu kiko mapema


Ova
 
Nairobi saa kumi na moja asubuhi unapata mahindi ya kuchoma ugali wa moto nk...
Ndio maana hotel nyingi tu bongo zilikuwa zinaweka mameneja Wakenya kabla ya jiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…