Mameneja wa bar, wamiliki wa majiko DSM muna shida gani?

Mleta mada umeongea ukweli, hili ni tatizo maeneo mengi Dar.
Juzi kati niliagiza mchemsho wa nyama ya kuku kwenye bar moja maeneo ya Tabata Balacuda nilisusa nikaondoka kimya kimya.
Niliagiza wakaniletea nyama ya kuku iliyopashwa kwenye supu ya utumbo..pumbavu zao wale!
 
Hahaha hii ni hatari sana
 
najua, ila kuna sehemu zile wanaofungua asubuhi ila asubuh yenyewe ni majanga
Sasa kwanini usiende hizo sehemu wanazofungua 24/7 wewe unakomaa kwenda hizo wanazofungua asubuhi??!! kila eneo na wateja wake.
Au unategemea ukienda kila siku asubuhi watabadilisha utaratibu ili wakidhi mahitaji yako??
 
Hapo mbuzi online tu kimara korogwe ni kwa mchagga ila mtori haupati hadi ifike saa 3 na kuendelea, achana na ujinga wa kufikiria ki kabila
 
Sasa kwanini usiende hizo sehemu wanazofungua 24/7 wewe unakomaa kwenda hizo wanazofungua asubuhi??!! kila eneo na wateja wake.
Au unategemea ukienda kila siku asubuhi watabadilisha utaratibu ili wakidhi mahitaji yako??
ndugu meneja acha uvivu amka mapema
 
Unakunywaje chai saa tano Dar? Labda moshi na arusha au mbeya.
 
Kumbe tupo wengi tunaopata huu usumbufu mfano kwa Madale Montana, Joy, Deez,Musu, Mbuzi Online halafu hata Goba mfano Texas, Trindad,Triple B, Plan B.
Wote ni hovyo tu poor customer care tena ukienda uko simple ndio vina nyodo balaa
Duh mkuu ebu taja makanisa watano unayoyafahamu!!?
 
Mbona sisi huku Masaki hakuna hio shida....
Nenda huu mgahawa wanafungua tokea saa 1:30 asubuhi, ila kwenye menu hawaandiki bei.....

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…