Mamlaka inayotoka kwa Mungu ni Ile inayotenda Haki na kulinda utu wa watu wake

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Ijumaa Kareem!

1. Mara nyingi watu waovu hutumia maandiko kupotosha Jambo Fulani au kuhalalisha uovu Fulani.

2. Sio Kila mamlaka inatoka kwa Mungu.

3. Zipo Mamlaka za kihalifu ambazo chimbuko lake ni Shetani(roho chafu)..

4. Mtu yeyote anayekuambia Mamlaka zote zinatoka kwa Mungu kaa ukijua ni mshirika wa uovu.

5. Mamlaka inayoheshimiwa na inastahili kuheshimiwa ni Mamlaka inayotoka kwa Mungu ambayo maelekezo yake huwa ya HAKI na kulinda Utu wa binadamu. Kinyume na hapo ni kumheshimu shetani. Yaani kuwa mtumishi wa Shetani.

6. Unapoambiwa usiabudu miungu mingine au kuabudu sanamu tafsiri yake ni kuheshimu na kusujudia mamlaka isiyotoka kwa Mungu.

7. Wengi huamini kwenda kanisani au msikitini ni kuabudu. Wakati sivyo.
Ibada ni matendo ya heshima katika Jambo Fulani.
Ukiheshinu waovu na uovu huko ni kuabudu na kusujudia mashetani na sanamu.

8. Maandiko yanasema usivisujudie wala kuvitumikia. Mamlaka yoyote isiyotenda Haki na inayoharibu utu wa binadamu hautakiwi kuiheshimu, kuitumikia na kuisikiliza.
Ni kumsikiliza shetani

9. Watu wema wenye akili. Kamwe hawawezi kusujudia na kuabudu watu waovu wasiofuata njia za haki. Bila kujali watu hao wanaitwa kwa majina gani, hadhi gani, cheo gani na hali gani.

Kufikia hapo sina la ziada.

Nawatakia maandalizi mema ya sabato.

TaikonMaster
Kwa sasa, Mhungula. Kahama
 

Msimamo wako haueleweki
 
Kma huyu wetu ndio shetani mwenywe,!

Mtu umepata 98% ila umejizungushia ukuta wa jeshi na bunduki kwa kuogopa 2%!
 
Kama ndo hivyo bas hakuna mamlaka hata moja inayotoka kwa Mungu hapa Dunia
 
Weka hitimisho lako likae vizuri. Kwani unaogopa nini?

Unashindwa nini kuhitimisha kwa kusema: Mamlaka ya serikali ya Tanzania ya sasa chini ya Samia Suluhu Hassan haijatoka kwa Mungu, bali imewekwa na shetani. Ipo kwa muda tu kwa sababu Mungu ameiruhusu iwepo kwa makusudi maalumu

Hii ni kweli kabisa kwa kuwa Mungu Yehova hawapi watu fulani mamlaka ya kiserikali kwa njia ya kuharibu (manipulate) na kuiba uchaguzi wote na kuua watu wanaopinga wizi huo wa kura

Samia Suluhu Hassan na serikali yake yote ni imeingia kwa gharama za damu za watu. Muuaji ni shetani lakini Mungu wetu ni Mungu atunzaye uhai wa watu wake kwa wivu mkubwa.

LAKINI KUNA UKWELI MWINGINE MUHIMU TOKA KWA MUNGU MWENYEWE: Kwamba, nyakati fulani Mungu huruhusu serikali za kishetani kama hii yetu chini ya Samia Suluhu Hassan kuwepo kwa mpango na kwa kusudi maalumu kwa watu wa Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…