ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 48,052
- 104,677
Wakuu,
Ni ajabu sana kuona miji midogo ndani ya majiji haina sehemu zenye utulivu kwa ajili ya watu kupumzika na kutembea, huku wakicheza na watoto wao, wakinywa soft drinks na bites, wakipiga picha na kupumzisha mafuvu yao.
Mji mdogo kama Mbezi-Kimara, kutwa ni shughuli za kiuchumi zinaendelea, kuanzia maduka makubwa hadi wanaopanga nyanya stand, huduma za usafirishaji hadi huduma zetu pendwa usiku wa manane maeneo tofauti kama kwa Gody, kwa Robert(Ngao Pub) na njia ya Kinyerezi.
Sasa kwa nini kusiwe na maeneo ya watu kupumzika, yatengenezwe vizuri, yahudumiwe kwa usafi yavutie wenyeji na wageni? Hizi open spaces nyingi zimegeuzwa maeneo ya biashara ndogondogo.
Watanzania nadhani hatuna huu utamaduni, tukitaka kutoka basi it's either tukutane bar, beach na wengine wetu guest😀, sio kila mtu anapenda kukutana bar. Lakini kuna namna tunaweza kujenga na kutengeneza maeneo mahususi watu wakakaa na kupumzika, kuongea, kupanga na kupangua mambo yao. Mbona hapo Zanzibar kuna sehemu zimejengwa vizuri tu, huku bara sisi tunashindwa nini?
Napendekeza eneo linalotizamana na Magufuli Stand, katikati ya barabara kuu na Stand kuu kuwe na recreation space, ijengwe vizuri, ivutie wageni na wenyeji, yaani sisi tunakuwa wala vumbi tu mda wote kweli? Sio Mbezi tu, sehemu zote za miji yetu zinahitaji kuwa na mandhari za kuvutia wageni na wenyeji, tuache uchafu jamani, miji yetu ni michafu sana, haivutii, inaongezea watu stress.
Kwani wenye nchi huwa hawasafiri wakaona wenzetu wanafanyaje huko kwao?