Mamlaka naomba iunde kikosi maalumu kichunguze tukio la kupotea kwa Askari Emmanuelle Govella

Mamlaka naomba iunde kikosi maalumu kichunguze tukio la kupotea kwa Askari Emmanuelle Govella

Haieleweki ndugu yangu kwanza Sisi majirani tuliowengi miezi yote hatukuweza kujua kama jamaa ni askari mpaka ulipovunjwa mlango wake na kukuta uniform Tena alikuwa na nyota Mbili wenzake walisema alikuwa mkuu wa kituo Cha mtumba mji wa kiserikali nafkiri hakutaka watu wamjue kama ni askari.
Kwa hiyo Uniforms alikuwa anazivalia wapi?
 
Au ni miongoni mwa walioratibu zoezi la Lissu
 
Kwa hiyo Uniforms alikuwa anazivalia wapi?
Askari wengi sikuhizi hawavalii uniform nyumba za kupanga huwa wanaenda kuvalia kituoni shifti ikianza

Ila sasa sijajua wakifua wanaanika wapi? Au ni mwendo wa laundry shop tu
 
Kama aliingia kwenye anga za watu wakala kichwa utajuaje maaskari wa Tanzania wanajifanyaga sometimes miungu watu sasa ukikutana na watu wa Kanda Maalum wanakuua na wanakulawiti vilevile , dhuluma na dhambi zao ndio zinawatafuna hawatakaa salama, Babu yangu alishawahi kusema ukiona umekosa kazi ukawa sijui polisi sijui mkamata nini ujue basi tena huna maana kwenye jamii
Babu yako genius

Kazi ya polisi ni kazi ya laana tupu.

Sitoshauri mwanangu aende huko afadhali jeshini ila sio polisi

Hao watu tangu enzi Yesu walikuwa wamejaa milaana ya kudhulumu watu haki zao rushwa na Mambo kedekede.

Sikiliza kuna mtu anaitwa Zirro anavyoongea utaelewa uwa polisi ni wapuuzi wapuuzi tu
 
Mh rais nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupa Afya njema na kuweza kutekeleza vyema majukumu yako ya kitaifa,mh rais Nina ombi maalum kwako kama mwananchi wako ambaye nimeguswa Sana na tukio la kupotea kwa askari polisi Emmanuelle Govella wa kituo kidogo cha mtumba mji wa kiserikali hapa Dodoma.

Mimi ni jirani hapa Nkuhungu Dodoma na Nyumba ambayo polisi huyu alikuwa amepanga siku ambayo ndugu wa huyo polisi walifika na polisi wa kituo Cha kati dodoma kuvunja mlango ili kujua kwanini askari huyo hapatikani muda mrefu nilikuwepo karibu.

Ilikuwa kati ya tarehe 19| 20 mwezi huu wa saba baada ya kuingia ndani walikuta simu ikiwa na laini zake zote Mbili lakini pia walikuta wallet yake ikiwa na vitambulisho vyake vyote mpaka kadi ya benki pamoja na fedha tasrimu sikujua kiasi gani, namba yake 0768243998 inaonyesha alikuwa hewani mala mwisho ni tarehe 26june hata ukiangalia WhatsApp inaonyesha hivyo mpaka siku wanabomoa kwake zilisha pita siku 24 Sasa Kuna maswali najiuliza ni kweli kwamba askari anapotea ZAIDI ya wiki 3 bila wenzake kujua?

Ombi langu kwako MH RAIS uunde kikosi maalum kichunguze upoteaji wa askari huyu Emmanuel govella Mpaka Leo hii nakutumia maombi haya ni takribani mwezi mmoja na siku 5 askari huyu hajaonekana ,nakutakia majukumu mema na Mwenyezi Mungu akutangulie.
Mungu amsaidie huko aliko sijui kakumbana na dhahma gani..lakin naona kuna maajabu hapo simu iwe hewan kwa siku zaid ya kumi tena hadi wasap? Au kuna alikua na hiyo simu alikua anasikilizia? Hiyo simu haikua na paswd? Kuna ujumbe wowote unaonyesha alichat kwa hizo siku?
 
Nowadays kuna ma askar kanzu wamefuga mizuzu na Wana sigda kama waswali sunaaa....

Ukionyeshwa hata huwazanii. Wala nini....save the date.
Nilishawahi kukutana nao,alitusimamisha kwenye gari kukagua maana gari yetu ilititia kidogo
 
kwa maelezo hayo,alikuwa anaishi double life,kuna jambo alikuwa anaficha na hatimaye wahusika wakfanikiwa kufungua codes
 
Unajitoa mwenyewe, unadhani Askari officer WA nyota mbili anawezaje kupotea kienyeji hivo, zingatia maelezo hapo juu alikuwa mkuu wa Kituo fulani,alikuwa hapendelei kuvaa uniform akienda kazini badala yake alikuwa akibeba begi jeusi mgongoni, jiulize Kwa nini alikuwa anaficha identity? Defenitly was an agent undercover, jiulize Askari wa level officer commanding station anawezaje kupotea polisi wasitoe tamko mpaka ndg zake ndo wamtafute? Anzia hapo kujiuliza kama alivuruga mission huyo ndo umsahau, formula ni moja tu kwamba if the law doesn't work, Eliminate.
Ukimya wa mwajiri wake umebeba ujumbe ....
 
Babu yako genius

Kazi ya polisi ni kazi ya laana tupu.

Sitoshauri mwanangu aende huko afadhali jeshini ila sio polisi

Hao watu tangu enzi Yesu walikuwa wamejaa milaana ya kudhulumu watu haki zao rushwa na Mambo kedekede.

Sikiliza kuna mtu anaitwa Zirro anavyoongea utaelewa uwa polisi ni wapuuzi wapuuzi tu
Umasikini ndio laana kubwa,wekeza nguvu huko kuuondoa.

Mungu alivyo wa ajabu,mwanao wa kike ataolewa na polisi,na ndiye pekee atakuwa anakutunza.
 
Hakika mkuu Kuna watu wanawaza ujinga wa siasa za maji taka muda wote wanafkiri kila mtu anahitaji masiasa siasa mtu kapotea badala ya kuchangia namna nini kifanyike yaani ni ccm v/s chadema+chuki basi ni upuuzi tu.

Ben saanane yuko wapi?
 
Back
Top Bottom