Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam

Ukweli ni kwamba DP world imepanga kuhuisha ajira zote za Bandari ili kuanza upya. Kitakachotokea ni hichi:
1. DP world itaajiri upya wafanyakazi (muhimu na wachache?) kutokea TPA.

2. Wafanyakazi watakao ajiriwa na DP world watapangiwa majukumu mapya na mishahara mipya. (Huenda yale marupuru ya holela yasiwepo tena)

3. Wafanyakazi wengine wote ambao hawataajiriwa na DP world watabakia TPA lakini wataondolewa bandari ya Dar na mwisho wa siku watachukuliwa na serikali kuhamishiwa taasisi nyingine za serikali.
 
Hii ndio inaitwa Counter attack ya DP world, kuanzia April Mosi ajira za watumishi wa bandari zitakuwa katika mtazamo mpya kabisa, kuna dalili za kilio kwa baadhi ya watu.

Yaani jengo moja lenye vyumba 10 vya ofisi lina wafagizi zaidi ya saba, wenye mishahara ya kuanzia 1m kwa mwezi na bado chafu halafu muarabu aache hivyo hivyo, watapukutishwa wote hapo, halafu kampuni za usafi zitapewa tender ya kuhakikisha usafi hapo.
 
TPA inauhakikishia Umma kwamba, itaendelea kuwathamini Watumishi wake ambao ni rasilimali muhimu zaidi katika Mamlaka na katika utekelezaji wa zoezi hili, maslahi ya pande zote husika yatazingatiwa kikamilifu kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.
porojo tu hizi. Bila kufanya kitu kikubwa nchi hii inaangamia
 
Watabanwa kinoma aisee ,walivyozoea bata hatari sana ,sehemu nyeti wanaondolewa kote .
 

Kuna sehemu wameandika, "kwani TPA ina mpango wa kuboresha bandari zake ktk maeneo mbalimbali nchini" maana yake watatawanywa ktk bandari zingine[emoji16][emoji16]
 
Kuna sehemu wameandika, "kwani TPA ina mpango wa kuboresha bandari zake ktk maeneo mbalimbali nchini" maana yake watatawanywa ktk bandari zingine[emoji16][emoji16]
Hao wafanyakazi watakao bahatika kubakia TPA watatupwa huko mikoani wakapauke vibaya. Muarabu hana muda wa kucheka cheka na kima mweusi.
 
😆 mtaalam wangu we wa masuala ya uchumi na fedha
Hii nchi ukisema uifatilie itakupasua moyo + ubongo tu

Ova
 
DP world ni kampuni binafsi, watumishi wa TPA ni watumishi wa Umma hivyo hapo kuna kubadilisha ajira kutoka kuwa mtumishi wa umma na kuwa mtumishi wa private. Hivyo ni lazima watumishi waridhie kuondoka TPA kwenda DP World na walipwe stahili zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi wa umma
 
Hapa ni janja ya TPA. Wafanyakazi watakaochagua kubaki TPA ina maana wengi watasambazwa Mikoani mfano Musoma, Mbaba Bay, Kyela, Mwanza, Ukerewe, Kemondo n.k na kama maisha yako yote ni Dar basi uchaguzi wako ni kuacha kazi. Watakaopenda kufanya kazi na DP World hata hawa DP World watakuwa na hiari ya kuendelea nao au kuachana nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…