Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam

Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam

Ukweli ni kwamba DP world imepanga kuhuisha ajira zote za Bandari ili kuanza upya. Kitakachotokea ni hichi:
1. DP world itaajiri upya wafanyakazi (muhimu na wachache?) kutokea TPA.

2. Wafanyakazi watakao ajiriwa na DP world watapangiwa majukumu mapya na mishahara mipya. (Huenda yale marupuru ya holela yasiwepo tena)

3. Wafanyakazi wengine wote ambao hawataajiriwa na DP world watabakia TPA lakini wataondolewa bandari ya Dar na mwisho wa siku watachukuliwa na serikali kuhamishiwa taasisi nyingine za serikali.
 
Hii ndio inaitwa Counter attack ya DP world, kuanzia April Mosi ajira za watumishi wa bandari zitakuwa katika mtazamo mpya kabisa, kuna dalili za kilio kwa baadhi ya watu.

Yaani jengo moja lenye vyumba 10 vya ofisi lina wafagizi zaidi ya saba, wenye mishahara ya kuanzia 1m kwa mwezi na bado chafu halafu muarabu aache hivyo hivyo, watapukutishwa wote hapo, halafu kampuni za usafi zitapewa tender ya kuhakikisha usafi hapo.
 
TPA inauhakikishia Umma kwamba, itaendelea kuwathamini Watumishi wake ambao ni rasilimali muhimu zaidi katika Mamlaka na katika utekelezaji wa zoezi hili, maslahi ya pande zote husika yatazingatiwa kikamilifu kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.
porojo tu hizi. Bila kufanya kitu kikubwa nchi hii inaangamia
 
Hii ndio inaitwa Counter attack ya DP world, kuanzia April Mosi ajira za watumishi wa bandari zitakuwa katika mtazamo mpya kabisa, kuna dalili za kilio kwa baadhi ya watu.

Yaani jengo moja lenye vyumba 10 vya ofisi lina wafagizi zaidi ya saba, wenye mishahara ya kuanzia 1m kwa mwezi na bado chafu halafu muarabu aache hivyo hivyo, watapukutishwa wote hapo, halafu kampuni za usafi zitapewa tender ya kuhakikisha usafi hapo.
Watabanwa kinoma aisee ,walivyozoea bata hatari sana ,sehemu nyeti wanaondolewa kote .
 
Hawa wafanyakazi hawakupaswa kupewa jukumu la kuchagua TPA au DP World. Nionavyo mimi ilitakiwa TPA kukabidhi wafanya kazi wote waliokuwa chini ya TPA kwa DP world, Muundo wa TPA uvunjwe na ubaki uongozi wa TPA kusimamia tu uendeshaji wa DP world na kuhakikisha hawa DP World hawatanyanyasa wafanyakazi na kuhakikisha malipo yao yanfuata makubaliano ya mkataba, na kuhakikisha mkataba wenyewe unaenda kama ulivyopangwa.

Sasa TPA inabaki kufanya nini ilkiwa DP World anapewa Bandari ya Dar es Salaam na zingine na za maziwa yote, kama sikukosea mkataba ulikuwa unasemaje.

TPH iji disolve yenyewe, wafanyakazi wote waende kule DP World kwa mama Kizimkazi.

Kuna sehemu wameandika, "kwani TPA ina mpango wa kuboresha bandari zake ktk maeneo mbalimbali nchini" maana yake watatawanywa ktk bandari zingine[emoji16][emoji16]
 
Kuna sehemu wameandika, "kwani TPA ina mpango wa kuboresha bandari zake ktk maeneo mbalimbali nchini" maana yake watatawanywa ktk bandari zingine[emoji16][emoji16]
Hao wafanyakazi watakao bahatika kubakia TPA watatupwa huko mikoani wakapauke vibaya. Muarabu hana muda wa kucheka cheka na kima mweusi.
 
Tuliwakatalia Oman na China kama awataki mkataba wa miaka 33 bandari ya Bagamoyo uwekezaji wa $10 billion dollars.

Halafu tumeenda wapa Dubai miaka 30 kwa uwekezaji wa $500m huku wanachukua sehemu kubwa ya Dar port.

Haki ya mungu hii nchi, uwekezaji wa DP World ni kweli unatija na strategic lakini ndio miaka 30.

Excuse my language sijapata kuona nchi ina viongozi wasiojielewa kama Tanzania. Hiyo hela DP world si anarudisha chini ya miaka minne tu.
😆 mtaalam wangu we wa masuala ya uchumi na fedha
Hii nchi ukisema uifatilie itakupasua moyo + ubongo tu

Ova
 
DP world ni kampuni binafsi, watumishi wa TPA ni watumishi wa Umma hivyo hapo kuna kubadilisha ajira kutoka kuwa mtumishi wa umma na kuwa mtumishi wa private. Hivyo ni lazima watumishi waridhie kuondoka TPA kwenda DP World na walipwe stahili zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi wa umma
 
Hapa ni janja ya TPA. Wafanyakazi watakaochagua kubaki TPA ina maana wengi watasambazwa Mikoani mfano Musoma, Mbaba Bay, Kyela, Mwanza, Ukerewe, Kemondo n.k na kama maisha yako yote ni Dar basi uchaguzi wako ni kuacha kazi. Watakaopenda kufanya kazi na DP World hata hawa DP World watakuwa na hiari ya kuendelea nao au kuachana nao.
 
Back
Top Bottom