Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam

Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam

Kimsingi TPA hana mamlaka kwenye bandari kwa sasa na kama angekuwa ana mamlaka kama tulivyo ambiwa hawa wafanyakazi walitakiwa kukabidhiwa kwa DPW! Lakini kimsingi hawa wafanyakazi ni kama wamefukuzwa kazi TPA na ndio maana wanapewa option ya kinachoitwa kuajiriwa maana yake watapewa mikataba mipya na yenye masharti mapya na watapimwa kwa vigezo na hakutakuwa na kufanya kazi bila kufukuzwa kazi hivyo wale watakao ajiriwa na DPW wajiandae kuchapa kazi kweli kweli ……!

Kiufupi watakao baki TPA wengi wao watahamishiwa kwenye ofisi za serikali na mashirika mengine na pia watapelekwa kwenye vibandari vidogo vidogo…..!

Kwa watanzania walivyo na mambo ya hovyo,uvivu ,ujinga nawashauri wabaki TPA….
Watakaochagua Dp wataangukia Pua hawatafikisha 30 years kwenye ajira
 
Unajua kuna gati ngapi pale bandarini!?
Sehemu iliyo baki ni ya wavuvi tu, hata ile aliyo kuwa nayo tics ambayo ilipewa kampuni haileweki ni janja tu za kumshikia dp word.
Hakuna gati inayo baki, na sgr ikikamilika mpaka mwanza na kigoma nazo atachukua
WACHUKUE TU. TUTAFANYAJE SASA! NCHI IMEJAA MACHAWA TUPIU NA VYUO VINAZALISHA MACHAWA TU. WAJUKUU ZETU WATAPAMBANIA UHURU WA RASILIMALI ZAO ZILIZOUZWA NA BABU ZAO WAJINGAWAJINGA.
 
Hawa wafanyakazi hawakupaswa kupewa jukumu la kuchagua TPA au DP World. Nionavyo mimi ilitakiwa TPA kukabidhi wafanya kazi wote waliokuwa chini ya TPA kwa DP world, Muundo wa TPA uvunjwe na ubaki uongozi wa TPA kusimamia tu uendeshaji wa DP world na kuhakikisha hawa DP World hawatanyanyasa wafanyakazi na kuhakikisha malipo yao yanfuata makubaliano ya mkataba, na kuhakikisha mkataba wenyewe unaenda kama ulivyopangwa.

Sasa TPA inabaki kufanya nini ilkiwa DP World anapewa Bandari ya Dar es Salaam na zingine na za maziwa yote, kama sikukosea mkataba ulikuwa unasemaje.

TPH iji disolve yenyewe, wafanyakazi wote waende kule DP World kwa mama Kizimkazi.

Tanzania kama inalaana dah , tunaanzisha tatizo na kuanza kupambana nalo dah
 
Hii kitu ngumu sana...mambo haya ni kama msiba tu, ukiwa kwa jirani mzuri..ukikukuta duh....
Mi siku mkataba wangu umeisha, sikulala vizuri wiki nzima nawaza tu
 
Wasi
Hawa wafanyakazi hawakupaswa kupewa jukumu la kuchagua TPA au DP World. Nionavyo mimi ilitakiwa TPA kukabidhi wafanya kazi wote waliokuwa chini ya TPA kwa DP world, Muundo wa TPA uvunjwe na ubaki uongozi wa TPA kusimamia tu uendeshaji wa DP world na kuhakikisha hawa DP World hawatanyanyasa wafanyakazi na kuhakikisha malipo yao yanfuata makubaliano ya mkataba, na kuhakikisha mkataba wenyewe unaenda kama ulivyopangwa.

Sasa TPA inabaki kufanya nini ilkiwa DP World anapewa Bandari ya Dar es Salaam na zingine na za maziwa yote, kama sikukosea mkataba ulikuwa unasemaje.

TPH iji disolve yenyewe, wafanyakazi wote waende kule DP World kwa mama Kizimkazi.
Wasijichanganye TPA wakavunja Muundo wao ili kuwakabidhi wafanyakazi kwa DP-W. Watu wanaopew dhamana kufuatilia haki za wafanyakazi huwa hawatekelezi wajibu wao

maana wakienda kufuatilia, wamiliki wa miladi,viwanda au makampuni, huwa wanapozwa kwa kupewa vijifedha ili wasitekeleze wajibu wao au kuwachukulia hatua waajiri, Tunayaona Mengi sana huku viwandani kwa wahindi,wachina NK.
 
Gati no. 0 mpk no. 7 ? Mbona kama magati yanaongezeka?
Kiufupi wamepewa maeneo ya tanzania bara ya bandari na nchi kavu…hadi mizigo ya SGR na ile reli ni yao tulivyokuwa tunajadili ule mkataba wa hovyo mlituona wajinga sana…..
 
Attachments

  • IMG_2095.jpeg
    IMG_2095.jpeg
    386.4 KB · Views: 4
Wasi

Wasijichanganye TPA wakavunja Muundo wao ili kuwakabidhi wafanyakazi kwa DP-W. Watu wanaopew dhamana kufuatilia haki za wafanyakazi huwa hawatekelezi wajibu wao

maana wakienda kufuatilia, wamiliki wa miladi,viwanda au makampuni, huwa wanapozwa kwa kupewa vijifedha ili wasitekeleze wajibu wao au kuwachukulia hatua waajiri, Tunayaona Mengi sana huku viwandani kwa wahindi,wachina NK.
Sasa wasipouvunja muundo wao na wao wakawa na wafnyakazi wao na DP World ikawa na wafanya kazi wake inapoteza taswira tuliyoambiwa wakati DP World walipokuwa watutongoza. Walisema HAKUNA MFANYAKAZI ATAPOTEZA AJIRA WALA STAHIKI ZAKE, BALI ZITABOREKA NA KUBORESHWA.

Sasa Jiulize, Ikiwa wafanyakazi wote wakaamua kubaki TPA, DP World inabidi aajiri wafanyakazi wapya, sasa hao wafanyakazi wa TPA watafanya kazi gani na wapi?
 
Wamepewa gati nane (8) tu katika Bandari ya Dar es Salaam. Gatio namba 0-7.
TPA bado inaendelea kusimamia gati zingine na bandari zingine.
Soma hiyo barua tena na tena, na tena na ukiona huelewi muulize na mwingine asome tena. Labda useme mwandishi wa hiyo barua kakosea, au ulete mkataba uliosainiwa ambao walisema utakuwa SIRI.
 
Kimsingi TPA hana mamlaka kwenye bandari kwa sasa na kama angekuwa ana mamlaka kama tulivyo ambiwa hawa wafanyakazi walitakiwa kukabidhiwa kwa DPW! Lakini kimsingi hawa wafanyakazi ni kama wamefukuzwa kazi TPA na ndio maana wanapewa option ya kinachoitwa kuajiriwa maana yake watapewa mikataba mipya na yenye masharti mapya na watapimwa kwa vigezo na hakutakuwa na kufanya kazi bila kufukuzwa kazi hivyo wale watakao ajiriwa na DPW wajiandae kuchapa kazi kweli kweli ……!

Kiufupi watakao baki TPA wengi wao watahamishiwa kwenye ofisi za serikali na mashirika mengine na pia watapelekwa kwenye vibandari vidogo vidogo…..!

Kwa watanzania walivyo na mambo ya hovyo,uvivu ,ujinga nawashauri wabaki TPA….
Nakuelewa, Lakini hawa TPA watakuwa ama WALITUDANGANYA au WAMEKIUKA WALICHOTUAMBIA. Walisema Hakuna mtanzania anayefanya kazi TPA atakosa ajira au kufukuzwa kwa sababu ya ujio wa DP World.

Na kwa mtizamo wangu hawa TPA walitakiwa wawaamishe wafanyakazi wao wote na mikataba yao ya awali ya TPA kwenda DP World. Na DP World alipaswa awapokee na kuwapa majukumu kulingana na mpangilio wake wa kazi na sio vinginevyo. TPA ambayo ndiye msimamizi wa ajira zao alipaswa kuhakikisha hilo takwa linatekelezeka na sio vinginevyo, kupewa option ya kuchagua ni kuingizana mkenge.

Inakuwaje nikichagua kutoka TPA na kwenda DP World nikafika kule DP World akasema sina qualification za kutosha au uwezo wa kufanya kazi naye, na kunifukuza? Apo lawama anabeba nani? TPA au Dp World?

TPA na serikali waache kulaghai watu na waweke mambo wazi, na hao wafanyakazi watulize akili ningekuwa mimi ni bora nibaki na TPA tumalizane kwanza, tulipwe malipo yetu na stahiki zote za wao TPA kukatisha ajira yetu. Kisha nitaenda DP World kuomba kujaribu zali nikipata sawa nikikosa sawa, vinginevyo ni kuwanyima raia haki zao.
 
Kuna sehemu wameandika, "kwani TPA ina mpango wa kuboresha bandari zake ktk maeneo mbalimbali nchini" maana yake watatawanywa ktk bandari zingine[emoji16][emoji16]
Lakini unakumbuka ulimkataba ulisema DP World watapewa Bandari zote za Bahari na maziwa yote. Na sababu ya hao DP World kupewa Kusimamia hiyo bandari si nikwasababu ya hao TPA kushindwa kuendesha? Sasa hiyo nguvu wanaitoa wapi tena ya kuboresha na kuendesha hizo bandari? Huo ni ubabaishaji, na hautakiwi.

Njia sahihi ni kutafuta muafaka kisheria. Ama Iwastaafishe kwa kuwalipa stahiki zote mpaka mwisho wa ajira zao na usumbufu wa kukatisha mkataba wao, au uwahamishie huko DP World bila masharti na ihakikishe DP World hato kiuka makubaliano yake na serikali, likiwemo kuwahakikishia hakuna atakayepoteza ajira yake.
 
Jambo lolote likielezwq na lisieleweke, likahitaji ufafanuzi, maana yake Halieleweki kwasababu halina mantiki.

Lakini tulisema mnapigwa madalali. Sasa .....
1) acha kazi ukafanyiw3 interview DP world na ushindwe urudi mtaqni
2) baki TPA upelekwe bandari ya Lindi, Chato, na bwawa la nyumbq ya m7ngu.....maana hamnagq qkili daaad3ki
 
Takataka,, Hii Nchi Hata Mtoto wa Miaka Kumi Anaweza kuongoza na akauza Chochote anachotaka. Ukiona mwekezaji anasaidiwa na Wenye Nguvu jua Hamna kitu hapo
 
Ndio tatizo la kuongozwa na kiongozi mbumbumbu. Kiukweli Bandari ya Dar es salaam ilikuwa sio ya kuichia kirahisi hivyo kwa muwekezaji tena kwa mkataba wa kijinga namba ile.

Tena hiyo miaka 30 wameweka tu geresha baada ya kelele kuzidi yaani ni mzigo kwa taifa kuwa na kiongozi ambae hana future,

Ila kwa wafanyakazi wa TPA nawapa pole sana maana ni pigo zito na vitambi vishaanza kuwashuka sii kwa maokoto mliokuwa mnapiga hapo .Now mtaanza kuishi ndani ya mshahara sio tena kupiga madili
 
Back
Top Bottom