MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Maendeleo huja na changamoto zake. Ni kweli kama tungeweza kuendesha bandari zetu wenyewe kwa ufanisi basi kusingekuwa na haja ya DP World. Tatizo lilianza kwa hao wafanyakazi wa TPA na uongozi wao. Walioajiriwa ni wengi lakini karibu wote wanachowaza ni upigaji. Hata sisi tulio nje ya ajira za TPA wengi wetu tulikuwa tukitamani kupata ajira hapo ili tupige. Kimsingi hela nyingi za umma zilikuwa zinaishia kwenye matumbo ya watu wa TPA. Ni kawaida kuona mtumishi wa TPA ndani ya miaka michache akimiliki mali za mamilioni kirahisi. DP World ndo mwarobaini.
Mimi ninashauri watumishi wabaki TPA na kumalizana na TPA kuhusu stahiki zao na wakubali tu kiroho safi aidha kuacha kazi au kupangiwa kwingine. Kwa upuuzi walio nao wasijaribu kwenda DP World kwa sababu watadumu kwa muda mfupi kabla ya kufukuzwa. DP World atabaki na watu smart tu na wenye maadili.