Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Inaandikwa kwamba, basi Bwana Mungu akasema. NA TUUMBE MTU kwa mfano wetu. Hapa Bwana Mungu hakuwa pekeyake... Kulikuwa na mamlaka kamili ya kiroho juu mbinguni yaliyokuwa yanaongozwa na Mungu mwenyewe.
Tafsiri nyingine ni kwamba tayari huko mbinguni kulikuwa na maisha mengine ya kiroho mpaka walipojadiliana kuumba mtu mwenyewe mwili wa nyama.
Uumbaji mwingine wote wa vitu na wanyama viliumbwa na Mungu mwenyewe. Kwa uweza wake mkuu wa kutamka tu na ikawa. Ilipofika kwenye kuumba MTU ndio cabinet ya mbingu ikahusishwa!
Kwanini kwenye uumbaji wa MTU Mungu hakufanya maamuzi binafsi Kama kwa wanyama mimea na vingine vyote? Kuna ufunuo wa ajabu hapa. Ni kwa vile alitaka awepo mtu kwa mfano WAO.
Shetani anatajwa kama malaika mkuu. Kivyeo vya kisasa unaweza kusema katibu mkuu, waziri mkuu ama msaidizi mkuu. Huyu kwa asilimia 95 hufahamu yote ya mkuu wake wa kazi kwakuwa ndio kama mtendaji mkuu.
Kwenye uumbaji Mungu aliumba kila kimoja na kinyume chake. N mpaka wakati huu Hakukuwa na kitu kinaitwa dhambi japo kabla ya uumbaji nchi ilikuwa kiza tena totoro kiwa (ukiwa) na vilindi vya maji vikiwa vimetuama juu ya uso wa dunia.
Ni kwenye uumbaji pekee wa Adam ndio Mungu aliishirikisha Mamlaka yake (shetani?) Vingine vyote alifanya mwenyewe. Na hata alipoona Adam yu mpweke bustanini. Kwa mamlaka yake binafsi akamtengenenezea Adam msaidizi (Hawa/Eva?)
Kwanini hapa haikushirikisha cabinet yake? Je, lilith ndio shetani mwenyewe? Nini kilimuudhi shetani mpaka kuamua kwenda kumdanganya msaidizi wa Adam ale tunda la mti wa kati? Mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Je, ni kwa vile hakushirikishwa kwenye kumtengeneza? Wivu? Kisasi? Kwanini hakumwendea Adam? Au kwakuwa aliasi mbinguni na kufukuzwa?
Na baada ya hapo dhambi ikaingia ulimwenguni na shetani akapewa ufalme wa giza. Ndio hapa kinyume cha mbingu kinakamilisha uumbaji wote kiroho.
Je, huu ulikuwa unabii au mpango wa Mungu? Kwanini shetani ana role kubwa sana kwenye dhana nzima ya kukengeuka kwa dunia, Adam na upili wa kiumbaji?
Tutafakari kwa pamoja, inawezekana kabisa shetani tumdhaniaye na nyoka tumwonaye ni vitu vingine kabisa tofauti na uhalisia wa dhana nzima ya Eden, uumbaji, uasi, tunda la mti wa kati nk