Theolojia haimtaji Lilith na huyu Shetani anatajwa tu kama Shetani.
Mara baada ya kukifuta kile kizazi dunia ilibaki tupu na ukiwa, maana yake hakukuwa na kiumbe hai chochote kilichobakia, na hapo ndipo Roho wa Mungu ikabidi ashikilie kipindi hicho cha mpito.
Shetani hakuachwa atambe kama wengi wanavyodhani, ila wanadamu ndio walimpa upenyo wa kuingia huku kwetu, kawaida ya Mungu huvijaribu viumbe vyake vyote alivyovyipa utashi wa kuchagua jema na baya.
Na lake ni zuri tu, ni ili viumbe vyake vionyeshe upendo na utiifu kwa Mungu wao kama vikipewa nafasi ya kupewa kuasi, maana yake ni kuwa pasipo uhuru wa kuasi maana yake hakuna freewill.
Adam alipewa mtihani huo kumpima utiifu wake, bahati mbaya sana akalamba F.
Theolojia inadai kuwa baada ya kuona amechemka, akapanga kujiua, lakini Mungu akamzuia, lakini aliendelea kufanya majaribio kama matatu hivi ya kujiondoa uhai kwani alijua madhara aliyoyaleta kwa kizazi chake baada yake.
Ndipo ikabidi Mungu kupitia Neno(kama aivyokuwa anajulikana siku hizo) kutoa ahadi ya kuja kumuokoa baada ya siku kubwa 5500.
Adamu akajua ni siku 5500 za kibinadamu, kumbe ilikuwa ni miaka 5500.
Na baada ya miaka hiyo 5500, Neno akaja kama mtoto mdogo kwa jina la Yesu na akaja kufanya kama alivyofanya.
Kwa nini Shetani aache kutamba??
Shetani amekuwa na kawaida ya kuendeleza uasi kwa uumbaji wa Mungu toka huko mbinguni mpaka huku duniani, sasa hukumu yake ilikwishatolewa, ila moja ya maajabu ya Mungu ni kutokutekeleza hukumu zake hata kama ameshahukumu.
Huwa Mungu ana tabia ya kutoa muda fulani kwa waliohukumiwa, kabla ya hukumu zao kutekelezwa.
Mfano Adamu aihukumiwa kufa mara baada ya kula tunda, lakini hukumu ilikuja kutimia Adamu akiwa na miaka kama 930 hivi, hivyo hivyo kwa Kaini na wengineo.
Shetani naye ameshahukumiwa, kinachompa kiburi shetani ni ujinga wa wanadamu kuendelea kumfuata huko kuzimu ili awape nguvu(kumbuka Shetani alikuwa malaika wa ngazi ya Kerubi na alikuwa ametiwa mafuta, au ana upako wake).
Na huo upako wake ambao wanadamu wanautafuta ndio unaompa access ya kuja huku uraiani, wanamfuata awape upako wa kuwa maarufu kupitia jamii za siri kama freemasonry, kuwapa upako wa kuwa matajiri, kuwapa upako wa kiutawala kupitia makafara, kuwapa upako wa ulinzi kupitia sarakasi zote za giza.
Kama mwanadamu akiamua kuachana na shetani , shetani hawezi kutamba duniani.
Dunia iliumbwa kwa ajili ya wanadamu na si mashetani, sisi ndio wenye vihere here vya kumkaribisha humu duniani, na kwa kuwa ni king'ang'anizi akishakuja kuondoka ni shughuli kweli kweli.