Mamlaka ya kiroho ndani ya mbingu - je, yalikuwa na pande mbili?

Mamlaka ya kiroho ndani ya mbingu - je, yalikuwa na pande mbili?

Mkuu zurri nina swali kidogo naomba ufafanuzi kwanini umesema SHETANI WA KIJINI?

pili, uyo Azazuri/Aba ndiye yule AZAZEL ambaye ni moja ya malaika 200 wanaotajwa katika kitabu cha HENOKO??


Kwanza nimeandika SHETANI WA KIJINI, kuweka utafauti na kumtambulisha kiumbe aliyekuwa anazungumziwa hapo.

Anayezungumziwa hapo ni jini ambaye ni muasi,mwanye jina Azazir/ Aba Sajida.

Ama kuhusu huyu nineae mzungumzia kwamba ndie AZAZEL hilo sijui.
 
@zurri iko vizuri ila umefupisha mno maelezo ukiweza ingia deep kidogo... Hasa kwenye suala la shetani jini kuumbwa kwa moto... Je jini na shetani jini wana tofauti gani?


Swali zuri hilo tunalijibu kwa mtindo huu "Si kila jini ni shetani"

Vile vile sifa ya shetani hata binadamu anakuwa nayo yaani binadamu anaweza kusifika kwa sifa ya "SHETANI",yaani sifa za kuasi na kuwashawishi wengine wafanye maovu.
 
Swali zuri hilo tunalijibu kwa mtindo huu "Si kila jini ni shetani"

Vile vile sifa ya shetani hata binadamu anakuwa nayo yaani binadamu anaweza kusifika kwa sifa ya "SHETANI",yaani sifa za kuasi na kuwashawishi wengine wafanye maovu.
Asante sana
 
"One of the truly bad effects of religion is that it teaches us that it is a virtue to be satisfied with not understanding.”
Then it become a burden... Very heavy to carry.,...!!!
 
Ninacho kupendea Mshana, mara nyingi hua unaleta HOJA fikirishi, well done brother.
Nichangie name ninavyo fahamu kidogo kuhusu hu uzi uliouleta; Ukisoma Biblia shetani (kabla ya kutupwa duniani alikua akiitwa Kerubi) hakua mkuu wa malaika kama watu wanavyo jaribu kufikiri, alikua mkuu wa Idara ya UIMBAJI, huko mbinguni inaitwa idara ya kusifu na kuabudu na Michael/Mikaeli yeye ni mkuu wa vita wakati Gabriel yeye ni mkuu wa kutoa habari; ukisoma kitabu cha Daniel nafikiri sura ya 7, malaika mmojawapo aliyetumwa kumletea habari Nabii Daniel anamwambia hivi Daniel, "....Ewe Daniel unaye pendwa sana...., maombi yako yalisikiwa tokea siku ile ulipo OMBA lakini yule mkuu wa UAJEMI alimzuia aliyetumwa nae Mikaeli mmojawapo wa wakuu..." hilo neno mmojawapo wa wakuu lina maana kwamba huko mbinguni wakuu wapo wengi! Again, hatuna hakika ni lini shetani alitupwa duniani, je ni baada ya uumbaji au kabla ya uumbaji!? No body knows kwasababu kwanini huyu huyu shetani alimuijia HAWA pale bustanini na kumdanganya!? LEt su wait from the Bible scholar to explain more

Hapa naona swala la uimbaji likiwa limeanza zamani asili ikiwa mbinguni na Kiongozi wa Kwaya baadae akatoswa, waimbaji wa nyimbo za kidunia unakuta mtu anasauti maridhawa tamu hadi unapagawa.

Sijui kuna connection na ule msemo wa "Sauti ya kumtoa nyoka pangoni" Nyoka kama kwaya Master!!!
 
Hapa naona swala la uimbaji likiwa limeanza zamani asili ikiwa mbinguni na Kiongozi wa Kwaya baadae akatoswa, waimbaji wa nyimbo za kidunia unakuta mtu anasauti maridhawa tamu hadi unapagawa. Sijui kuna connection na ule msemo wa "Sauti ya kumtoa nyoka pangoni" Nyoka kama kwaya Master!!!
Mmh... 😳 😳 😳 😳
 
hivi maandiko yanayodai shetani sijui alitupwa toka mbinguni huwa yanatokea wapi?
mwenye andiko atusaidie hapa
 
Najiuliza bandiko hili malidhawa sijaona mchango wake kiranga
 
!
!
Hold On.. .. Kwa Hiyo Dunia Ilishakuwapo Ila Ilikuwa Kiwa Na Tupu? Kwamba Kuanzia Chini Hadi Kuleee Juu Ni Maji Maji Na Giza? Vipi Jua Lilikuwepo Kabla?
 
!
!
Wakati Wanaumba Au Anaumwa Alikuwa Wapi? Mbingu Na Nchi. . . Kwamba Mungu Aliiedit Tu Dunia Au
 
Kuna facts nyingi ningekuwa na muda ningeandika kwa kirefu lakini moja ya chemsha bongo ambayo baadhi ya wanatheolojia wanasema ni kuwa pale Mungu anaposema na tuumbe mtu kwa sura na mfano WETU, haina maana kulikuwa na Miungu mitatu yenye sura moja bali lugha ya wingi iliyotumika ni ya kiuandishi ikiwakilisha tamaduni/tabia za jamii ya muandishi wa kitabu cha mwanzo.

Inasemekana lugha ya wingi ilitumika kuwakilisha ukuu au sifa kwa mtu/watu wakubwa. Kwa mfano hata huku uswahilini mtu anaweza kujisifia kwa kusema "watu kama SISI hatupandi daladala". Kitu kimoja kinachoitesa dunia ya leo ambacho Kanisa kilihofia miaka mingi ni direct translation of holy scriptures.

Imagine muhaya wa kamachumu ndio angekuwa mwandishi wa kitabu cha mwanzo alafu akiandike kwa kihaya alafu kitafsiriwe kwa lugha tofauti labda kihaya-kiswahili- English- Arab ili asome mtu aliye Iraq! Maandiko yanahitaji tahadhari kubwa sana.

Hiyo niliyoandika ni moja ya mantiki za wanatheolojia lakini binafsi nimesoma mitazamo mingi pia na ipo ambayo nakubaliana nayo kwa asilimia mia.
 
Kwa ufupi, wakati Adamu anaumbwa tayari Lucifer alikwishaasi na kutupwa duniani na malaika zake. Mungu alimuumba Adamu ili akaitawale dunia. Ukisoma mwanzo utaona Mungu anasema ana muumba Adamu ili akaitawale dunia.

Neno la Mungu ni sheria kwake ndio maana ni mtakatifu maana akisema neno linageuka sheria kwake na wala hasemi uongo. Hivyo kwavile Adamu alipewa nafsi huru na mamlaka ya kutawala dunia lakini akipewa sharti la kutokula moja ya mti, hiyo tayari ni sheria mbele za Mungu na wala hatengui kile alichosema.

Kwanza ndio maana shetani alipitia kwa eva ambaye si aliyepewa maagizo, na Eva aliumbwa kama msaidizi wa Adamu na tunaona tatizo lilianza pale tunda alipokula Adamu na si Eva!

Lakini pia kwavile Mungu akisema jambo linakuwa sheria automatically, Mungu hakwenda kumzuia shetani kumdanganya Adam na Eva sababu aliwaumba na nafsi huru na kuwapa mamlaka ya kutawala dunia. Hivyo Mungu kumzuia shetani angekuwa anavunja sheria yake mwenyewe maana yeye alishawapa mamlaka ya utawala kwa Adamu.

Ndio maana ili Mungu asivunje amri yake mwenyewe ilibidi aje duniani kwa kuvaa mwili kupitia Bikira Maria na kuwa mwanadamu ili aweze kutukomboa kutoka kwenye makosa ya Adamu......
 
Ukielewa utendaji kazi wa Mungu utaelewa vizuri mantiki ya Mungu kutumia wingi wakati wa kumuumba Adam. Nikiendelea ....utaona Mungu akivaa mwili wa Yesu ili aweze kututoa utumwani.

Yesu ni Mungu kweli na mtu kweli ndio maana anaitwa Yesu Kristo. Aliyekufa msalabani ni Yesu si Kristo! Aliyekwenda kumnyanganya shetani funguo za kuzimu ni Kristo si Yesu! Principle ya kushuka kuzimu ni lazima ufe, hivyo Yesu alikufa msalabani ili Kristo apate kibali cha kushuka kuzimu kumnyanganya shetani funguo.

Ndio maana Yesu alipofufuka na kupaa alisema nitawaachia msaidizi ....ambapo sasa Yesu aliyekuwa na mikono miwili, miguu miwili n.k hatakuwepo bali kutakuwa na kanisa ambalo ndio litakuwa mwili wa Kristo! The bible says the church is the body of Christ and not Jesus!

Imeeleweka walau ili mwanzo na habari zake zisomeke?
 
Back
Top Bottom