Mamlaka ya kiroho ndani ya mbingu - je, yalikuwa na pande mbili?

Mamlaka ya kiroho ndani ya mbingu - je, yalikuwa na pande mbili?

Naona uzi huu unakona kona nyingi sana.

Naomba niulize swali kwako Mshana Jr ni lini shetani alitupwa duniani?

Huwa unanadharia unazozijua ambazo kimsingi hata biblia haijazitaja.
 
Mshana Jr umeandika mambo ya kufikirika sana humu mkuu. Mbaya zaidi your biasness is transparent. Umeandika ukiwa tayari una imani yako - Yesu ni Mungu na Utatu Mtakatifu. Kosa.
Asante kwa mtazamo na mchango.... Ngoja tusikie na wengine wanasemaje
 
Naona uzi huu unakona kona nyingi sana.

Naomba niulize swali kwako Mshana Jr ni lini shetani alitupwa duniani?

Huwa unanadharia unazozijua ambazo kimsingi hata biblia haijazitaja.
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Ezekiel Ezekiel
28 :13 - 19
13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.
14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.
16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.
17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.
19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele

Nadhani umepata picha halisi ya shetan kutupwa kutoka mbinguni
 
Ukisoma simulizi hilo bila mahaba ya kiitikadi

Hutoshindwa kutambua kuwa shetani ndiye Mungu mwenye

Kulingana na hilo simulizi_ mwanadamu alikuwa anaishi kama hayawani akiwa bustanini(Eden) nimejuaje.?

Ni baada tu ya kula Tunda akaanza kuhisi Yu uchi..!? Ikiwa na maana akajitambua..!?

Umungu ukawaingia Adamu na hawa kama walivyo ambiwa na anayeitwa shetani..!? Kumbe naye mkweli eenh.[emoji39]

Hivyo kama waliweza kujitambua baada ya kula Tunda inaonesha hapo kabla mwanzoni walikuwa malofa bila ubishi

Kwa mantiki hii ni kwamba shetani huyo kwao alikuwa ni msaada wa kuwatoa kifungoni(uzwazwa)

Na si kama Adui kama wanavyoaminishwa watu wengi wanaolishwa maana kupitia masomo ya mwengine

Maana yake bora ni lipi.!?

Kati ya kuishi milele kama hayawani_ au kwa muda mfupi ila ukijitambua...!?

Mpaka hapa ni kwamba Uyo anayeitwa Adamu hakukosea kufanya maamuzi[emoji818]

Na ukiwa huru katika tafakari hutoshindwa pia kutambua kuwa ilikuwa ni makusudi la aliyeanzisha huo uhai katika pahala hapo

Ni kama igizo jengine la mind evolution (level 1 to 2) kwa huyo kiumbe anayeitwa Adamu

Ila katika hila ya huyo Mungu kujiita shetani....[emoji3][emoji16]

Ngoja niishie hapa nisije nikakera wengi
Ni kwanini yote haya yalitokea?
Je yalipangwa yatokee?
Je ni unabii?
Je kuna kitu kiliingilia mahali?
 
Ukisoma kwa umakini Mwanzo sura ya kwanza mstari wa kwanza utagudundua kuwa kulikuwa na maisha kabla ya uumbaji huu wa dunia ya sasa uliopo.

Na baadhi ya theolojia za Kikristo zinataja kuwa Mungu kabla ya kumuumba Adam na kizazi chake aliwahi kuumba kizazi kingine, ila kilijivuruga sana, hivyo akaamua kukifutilia mbali na hivyo kupelekea nchi kuwa giza na ukiwa na Roho Mtakatifu akapewa jukumu a kuishikilia dunia kwa muda mpaka pale Uumbaji mpya utakapofanyika.

Kwa muktadha wa theolojia hiyo ni kuwa mara baada ya Mungu kutaka kurudisha uumbaji upya kutokana na uumbaji wa kwanza kufutiliwa mbali, ilibidi kukaa kikao mbinguni kupitisha maazimio ya kumuumba mwanadamu wa sasa na kizazi chake, na hili lilileta mvutano sana.
Wengi wa malaika na viumbe vya mbinguni vilipinga wazo hili kwa hoja kuwa so long as Shetani bado yupo, haina maana ya kuleta upya kizizi kingine maana yatatokea yale yale ya kizazi cha kwanza.

Lakini theolojia hiyo haisemi kwa nini Mungu pamoja na hoja nzuri ya malaika zake aliamua kumuumba Adamu japo alijua kabisa kuwa angeyarudia makosa yale yale ya watangulizi wake.

Ikumbukwe pia kuwa Mungu amekuwa na kawaida ya kukaa vikao na malaika wake, kama inavyoonekana kwenye Biblia.

Mfano , wakati Mungu anataka kumuhukumu Mfalme katili sana wa Israel aliyejulikana kama Ahabu kilikaa kikao na majadiliano yakawepo ya jinsi ya kumdanganya Mfalme aende vitani ili auwawe ili neno la nabii Eliya litimie, habari hii inapatikana katika 1Wafalme 22:19-23.

Pia wakati Ayubu anaundiwa zengwe ili kujaribiwa kwa majipu yale kiliwahi kukaa kikao Mbinguni na inaonekana Shetani alipeleka hoja zake Mbinguni japo za uchongezi ili kumshitaki Ayubu ajaribiwe.

Pia kimewahi kukaa kikao kati ya Mungu na Wajumbe wake cha nani atumwe kuja duniani kuwaokoa wanadamu, wajumbe kwa kujua uzito wa kazi mbele yao walikaa kimya, ndipo Yesu akasema nitume mimi.

Pia kwenye kitabu cha Ufunuo 5:1 inaonekana kulikuwa kikao mbinguni kati ya Mungu na wajumbe wake cha kuangalia ni nani aliyekuwa na uwezo wa kufungua document moja iliyokuwa ina siri nzito sana, na wajumbe wote wakakosa qualifications , mpaka Yesu mwenyewe alipoamua kufungua document hiyo.

Kimsingi suala la vikao mbinguni ni la kawaida sana, tatizo linakuwa ni moja tu kuwa wajumbe wa vikao huwa hawatajwi, anatajwa mwenyekiti wa kikikao pekee ambaye ni Mungu, na hii inatokana na mfumo wa utawala wa Kimbingu kuwa wa Kifalme.
Kawaida ya mfalme ni kubeba sifa zote hata kama watendaji wake ndio wamefanya maana mamlaka ya kiutendaji ya watendaji hao inatoka kwa Mfalme mwenyewe.

Kwa hiyo suala la uumbaji wa Adamu lilikuwa ni mwendelezo wa vikao hivyo hivyo, tatizo ni kuwa wajumbe wa vikao hawakutajwa, ila ukisoma Bibia kwa umakini utagundua kuwa waliokuwa wanazungumza katika kikao hicho walikuwa na cheo cha Uungu.

Kibiblia wenye cheo cha Uungu kwa mbinguni wako watatu, Mungu Baba, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu.
Kwa duniani cheo cha Uungu kipo kwa Shetani(Yesu alimuita Mungu wa dunia hii), Musa pia aliwahi kupewa cheo hicho, akawa kama Mungu kwa Farao na Haruni kuwa Nabii wake.

Kwa mantiki hiyo, kama kikao kile cha uumbaji kilikaa mbinguni bila shaka walikuwa watatu waliokaa ambao ni Mungu Baba, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu.

Na hapo ndipo inapokuja kauli ya tumfanye mtu kwa sura yetu na mfano wetu.
Mungu hana tofauti na hili jiwe letu! Sifa zao zinaendana kabisa
 
.
words-for-witches-necromancy-cauldron-5674-84e7a6a3788f9ff95e49425ed12edd0a@2x.jpg
 
Inaandikwa kwamba..... Basi Bwana Mungu akasema... NA TUUMBE MTU kwa mfano wetu.. Hapa Bwana Mungu hakuwa pekeyake... Kulikuwa na mamlaka kamili ya kiroho juu mbinguni yaliyokuwa yanaongozwa na Mungu mwenyewe

Tafsiri nyingine ni kwamba tayari huko mbinguni kulikuwa na maisha mengine ya kiroho mpaka walipojadiliana kuumba mtu mwenyewe mwili wa nyama

Uumbaji mwingine wote wa vitu na wanyama viliumbwa na Mungu mwenyewe... Kwa uweza wake mkuu wa kutamka tu na ikawa.... Ilipofika kwenye kuumba MTU ndio cabinet ya mbingu ikahusishwa!

Kwanini kwenye uumbaji wa MTU Mungu hakufanya maamuzi binafsi Kama kwa wanyama mimea na vingine vyote? Kuna ufunuo wa ajabu hapa... Ni kwa vile alitaka awepo mtu kwa mfano WAO

Shetani anatajwa kama malaika mkuu... K vyeo vya kisasa unaweza kusema katibu mkuu, waziri mkuu ama msaidizi mkuu..... Huyu kwa asilimia 95 hufahamu yote ya mkuu wake wa kazi kwakuwa ndio kama mtendaji mkuu
Kwenye uumbaji Mungu aliumba kila kimoja na kinyume chake... N mpaka wakati huu Hakukuwa na kitu kinaitwa dhambi japo kabla ya uumbaji nchi ilikuwa kiza tena totoro kiwa(ukiwa) na vilindi vya maji vikiwa vimetuama juu ya uso wa dunia...

Ni kwenye uumbaji pekee wa Adam ndio Mungu aliishirikisha Mamlaka yake (shetani?) Vingine vyote alifanya mwenyewe.... Na hata alipoona Adam yu mpweke bustanini... Kwa mamlaka yake binafsi akamtengenenezea Adam msaidizi (Hawa/Eva?)

Kwanini hapa haikushirikisha cabinet yake? Je lilith ndio shetani mwenyewe? Nini kilimuudhi shetani mpaka kuamua kwenda kumdanganya msaidizi wa Adam ale tunda la mti wa kati? Mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Je ni kwa vile hakushirikishwa kwenye kumtengeneza? Wivu? Kisasi? Kwanini hakumwendea Adam? Au kwakuwa aliasi mbinguni na kufukuzwa?

Na baada ya hapo dhambi ikaingia ulimwenguni na shetani akapewa ufalme wa giza.... Ndio hapa kinyume cha mbingu kinakamilisha uumbaji wote kiroho....

Je huu ulikuwa unabii au mpango wa Mungu? Kwanini shetani ana role kubwa sana kwenye dhana nzima ya kukengeuka kwa dunia, Adam na upili wa kiumbaji?

Tutafakari kwa pamoja... Inawezekana kabisa shetani tumdhaniaye na nyoka tumwonaye ni vitu vingine kabisa tofauti na uhalisia wa dhana nzima ya Eden, uumbaji, uasi, tunda la mti wa kati nk
Kazi zote za utendaji wa Mungu ziko chini ya mamlaka ya Roho Mtakatifu. Unless mtu haamini juu ya utatu mtakatifu, yaani Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, huyo ndiye anayeweza kupinga hili, na akawa yuko sahihi kwa mtizamo wake. Kwa hiyo maongezi unayoongelea hapa yalikuwa ni ya hao watatu.

Zaidi ni kuwa Yesu alikuja duniani kwa njia ya kuzaliwa na binadamu, lakini alikuwepo huko mbinguni kabla. Kumbuka kuwa kipindi wakati wale malaika wawili wanakuja kuchoma Sodoma na Gomora, Yesu pia alikuja pamoja nao, na anatajwa kwenye maandiko matakatifu kama Bwana.

Malaika ni kiumbe mtumishi wa Mungu ameumbwa kwa ajili ya kukulinda wewe, and you are senior to all the angels, kwa sababu wewe ni mwana wa Mungu wakati yeye ni mtumishi wa mwana wa Mungu. Uhusiano wako wewe na Malika ni kama ule wa Rais na BodyGuard wake, isipokuwa:

Mlinzi wako wewe inabidi awe ana ujuzi zaidi kuliko wewe, na ndiyo maana mlinzi wa Rais ana ujuzi kuliko Rais
Zaidi ni kuwa malaika wao hawafi na hawana dhamhi, ila sisi tuna dhambi na huwa tunakufa. Malaika ni viumbe aliowaumba Mungu na hivyo hawakuwahi kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye uumbaji!

Shetani ni malaika
 
Maji, giza, kifo, vilikuwepo havikuumbwa
Hivi maji yalitoka wap? Maana hakuna sehemu inayo onesha kuumbwa kwa maji.
Na nchi( ardhi), giza vyote hivi uwepo hauja ainishwa moja kwa moja kweny biblia kwamba vilitokeaje. Sasa je vyote hivi nani aliviumba.
 
nahtaji kufaham kipi kilitangulia kati ya hvi? shetan kutupwa kwny mamlaka ya giza au shetan kumuongopea mwanamke? lakn pia nadhan aliamua kushirikisha cabinet yake juu ya uumbaji wa adam mana am sure ilihtaji skills kubwa zaid na pia ndo kwa mara ya kwanza ilibid aumbwe kiumbe kwa udongo na nyama, lakn hakuitaj sana msaada kumtengeneza mwanamke mana ilikua ni inshu ya kupga copy na kuweka jinsia tu,
Shetani alitangulia kutupwa kabla ya kuubwa kwa mwanadam. Na kilicho muuma zaidi ni ile kauli ya
Mwanzo 1:26

"Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."

Hii kauli ya kutawala ili muuma shetani kumbuka kakoswa utawala mbinguni kashushwa duniani napo anaenda kutawaliwa na binadam!!? Akaona nibora aturubuni ili na ss tuingie zambini lama yeye tusiweze kutawala kila kitu
 
Inaandikwa kwamba..... Basi Bwana Mungu akasema... NA TUUMBE MTU kwa mfano wetu.. Hapa Bwana Mungu hakuwa pekeyake... Kulikuwa na mamlaka kamili ya kiroho juu mbinguni yaliyokuwa yanaongozwa na Mungu mwenyewe
Tafsiri nyingine ni kwamba tayari huko mbinguni kulikuwa na maisha mengine ya kiroho mpaka walipojadiliana kuumba mtu mwenyewe mwili wa nyama
Uumbaji mwingine wote wa vitu na wanyama viliumbwa na Mungu mwenyewe... Kwa uweza wake mkuu wa kutamka tu na ikawa.... Ilipofika kwenye kuumba MTU ndio cabinet ya mbingu ikahusishwa!
Kwanini kwenye uumbaji wa MTU Mungu hakufanya maamuzi binafsi Kama kwa wanyama mimea na vingine vyote? Kuna ufunuo wa ajabu hapa... Ni kwa vile alitaka awepo mtu kwa mfano WAO
Shetani anatajwa kama malaika mkuu... K vyeo vya kisasa unaweza kusema katibu mkuu, waziri mkuu ama msaidizi mkuu..... Huyu kwa asilimia 95 hufahamu yote ya mkuu wake wa kazi kwakuwa ndio kama mtendaji mkuu
Kwenye uumbaji Mungu aliumba kila kimoja na kinyume chake... N mpaka wakati huu Hakukuwa na kitu kinaitwa dhambi japo kabla ya uumbaji nchi ilikuwa kiza tena totoro kiwa(ukiwa) na vilindi vya maji vikiwa vimetuama juu ya uso wa dunia...
Ni kwenye uumbaji pekee wa Adam ndio Mungu aliishirikisha Mamlaka yake (shetani?) Vingine vyote alifanya mwenyewe.... Na hata alipoona Adam yu mpweke bustanini... Kwa mamlaka yake binafsi akamtengenenezea Adam msaidizi (Hawa/Eva?)
Kwanini hapa haikushirikisha cabinet yake? Je lilith ndio shetani mwenyewe? Nini kilimuudhi shetani mpaka kuamua kwenda kumdanganya msaidizi wa Adam ale tunda la mti wa kati? Mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Je ni kwa vile hakushirikishwa kwenye kumtengeneza? Wivu? Kisasi? Kwanini hakumwendea Adam? Au kwakuwa aliasi mbinguni na kufukuzwa?
Na baada ya hapo dhambi ikaingia ulimwenguni na shetani akapewa ufalme wa giza.... Ndio hapa kinyume cha mbingu kinakamilisha uumbaji wote kiroho....
Je huu ulikuwa unabii au mpango wa Mungu? Kwanini shetani ana role kubwa sana kwenye dhana nzima ya kukengeuka kwa dunia, Adam na upili wa kiumbaji?

Tutafakari kwa pamoja... Inawezekana kabisa shetani tumdhaniaye na nyoka tumwonaye ni vitu vingine kabisa tofauti na uhalisia wa dhana nzima ya Eden, uumbaji, uasi, tunda la mti wa kati nk
Hakuna dhambi kumbwa kama wivu uongo huzaa zambi zote nyingine na hizo zambi ndo zambi pekee za shetani
 
Kwa uelewa wangu kwenye kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza vitu vilitengenezwa katika ulimwengu wa Roho (Created) ; kwenye sura ya pili inaelezea vitu jinsi vilivyotokea katika ulimwengu wa nyama( Formed)

Nikupe mfano, kwenye Mwanzo sura ya kwanza wanyama na mimea waliumbwa kwenye Ulimwengu wa kiroho (Created)- Mwanzo 1:24-25, kabla ya Binadamu ( Human Kind)- Mwanzo 1:27

Kwenye sura ya pili wakati wa vitu kuonekana katika Ulimwengu wa nyama ( Formation) Binadamu alianza - Mwanzo 2:7 kabla ya wanyama na mimea-Mwanzo 2:19 BWANA Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.

Kwa hiyo uumbaji wa sura ya Pili ni katika ulimwengu wa kimwili kiroho ulishafanyika kama sura ya kwanza inavyoeleza
Sikuwahi kuitazama Biblia kwa mtazamo huu katika uumbaji. Ahsante Mkuu umefungua ufahamu wangu eneo hilo
 
Kazi zote za utendaji wa Mungu ziko chini ya mamlaka ya Roho Mtakatifu. Unless mtu haamini juu ya utatu mtakatifu, yaani Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, huyo ndiye anayeweza kupinga hili, na akawa yuko sahihi kwa mtizamo wake. Kwa hiyo maongezi unayoongelea hapa yalikuwa ni ya hao watatu. Zaidi ni kuwa Yesu alikuja duniani kwa njia ya kuzaliwa na binadamu, lakini alikuwepo huko mbinguni kabla. Kumbuka kuwa kipindi wakati wale malaika wawili wanakuja kuchoma Sodoma na Gomora, Yesu pia alikuja pamoja nao, na anatajwa kwenye maandiko matakatifu kama Bwana. Malaika ni kiumbe mtumishi wa Mungu ameumbwa kwa ajili ya kukulinda wewe, and you are senior to all the angels, kwa sababu wewe ni mwana wa Mungu wakati yeye ni mtumishi wa mwana wa Mungu. Uhusiano wako wewe na Malika ni kama ule wa Rais na BodyGuard wake, isipokuwa:
Mlinzi wako wewe inabidi awe ana ujuzi zaidi kuliko wewe, na ndiyo maana mlinzi wa Rais ana ujuzi kuliko Rais
Zaidi ni kuwa malaika wao hawafi na hawana dhamhi, ila sisi tuna dhambi na huwa tunakufa. Malaika ni viumbe aliowaumba Mungu na hivyo hawakuwahi kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye uumbaji! Shetani ni malaika
Mlinzi wako wewe inabidi awe ana ujuzi zaidi kuliko wewe, na ndiyo maana mlinzi wa Rais ana ujuzi kuliko Rais

Zaidi ni kuwa malaika wao hawafi na hawana dhamhi, ila sisi tuna dhambi na huwa tunakufa. Malaika ni viumbe aliowaumba Mungu na hivyo hawakuwahi kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye uumbaji! Shetani ni malaika [emoji109][emoji109][emoji123][emoji123][emoji123][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Ndugu mshana nimesoma comments zote za wadau humu wengi wao huzungumzia hii dhana ya uumbaji kwa kuegemea upande wa biblia na quran ,kwani hatuwezi kuelezea hii dhana nje ya reference za bible na quran?
Tuna uwanja mdogo sana nje ya hiyo misahafu.. Na uwanja wenyewe ni kihistoria na kisayansi ambavyo ni kama vile viko mbali na uhalisia
 
Naona uzi huu unakona kona nyingi sana.

Naomba niulize swali kwako Mshana Jr ni lini shetani alitupwa duniani?

Huwa unanadharia unazozijua ambazo kimsingi hata biblia haijazitaja.
Shetani hajawahi kutupwa duniani, ni uongo, au misleading ya maandishi, mwenye aya alete tui analyse😄
 
Back
Top Bottom