Lakini pia ikumbukwe Mwanadamu aliumbwa baada ya uasi kuwa umeshatokea, na baada pia ya shetani kutupwa pande za mwisho za shimo, wengine hupaita kuzimu, wengine abyss, wengine Sheol, bottomless pit,wengine underworld, Lakini pia ikumbukwe kuzimu ipo tena ni halisi na ipo hapa duniani,na milango ya maingilio ipo pia hapa duniani kwetu.
Lakini kuzimu sio juu ya uso wa dunia bali ni chini au underworld ndipo alipotupiwa huyu kiumbe na huko ndio kuna enzi yake ya utawala au unaweza sema headquarters za wote walioshindwa vita ile, ndio yakawa makao yao mapya na ndio maana kwenda kuzimu wakati mwingine huelezewa kama kushuka shimoni, ndio maana huwezi sikia akashuka kuelekea mbinguni maana penyewe ni juu au akapaa kuelekea kuzimu maana kule ni shimoni, na hapo hatujui labda huenda ile force waliotupwa nayo ndio ilisababisha hilo shimo au tayari lilikuwepo kwa ajili yao hilo bado sijajua ila ninachoelewa kabla ya wanadamu na vitu tunavyoviona sasa duniani kuwepo kulikuwa na uumbaji mwingine wa viumbe wazuri sana waliombwa kwa magimba ya moto ndio waliokuwa wakikaa duniani sijasema kutawala dunia nimesema kukaa duniani.
Na hao ndio waliokuwepo hadi siku Nyota ya asubuhi inaanguka, sasa hapo hatujui kama wao pia walidanganywa wakaasi au kwa sababu ya hasira ya Mungu baada ya kumtupa chini mpinzani wake akaamua kuufutulia mbali huo uumbaji mzuri wa mwanzo kwa kuwa tayari ulikuwa umenajisika na uwepo wa viumbe waasi katika sehemu ya makazi yao na hivyo kupafanya pawe najisi na hivyo Mungu kupaharibu na viumbe vyote vilivyokuwepo na kupagharikisha kwa maji na kupafanya ukiwa na giza kwa ajili ya wivu wa hasira yake na utakatifu wake, rejelea kisa cha sodoma na gomora na pia kisa cha nuhu utaweza kuelewa nini nilikuwa nakimaanisha jinsi gani Mungu alikuwa anashughulika na uasi na unajisi wa viumbe.
Na ndio maana ukisoma biblia yako vizuri kwenye mwanzo kabisa wa uumbaji utagundua vitu hivi kuwa, dunia ilikuwepo tena ilikuwa imefunikwa kwa maji mengi sana, (vilindi)kwa hiyo na maji yalikuwepo na giza lilikuwa limeufunikiza uso wa nchi, na giza lilikuwepo tayari na roho ya Bwana ikatulia juu ya uso wa maji, ili kuanza uumbaji mwingine, hii inatufundisha kuwa Mwanadamu sio kiumbe wa kwanza kuishi duniani walikuwepo viumbe wengine wazuri waliombwa kwa magimba ya moto sijasema malaika maana malaika walikuwa mbinguni sio duniani, nimesema viumbe ila sijajua ni viumbe gani ila ni viumbe sio wa udongo ambao baada ya shetani kuangukia makao yao aliwaponza wao pia wakafutiliwa mbali na sehemu yao ya makazi kufanywa giza na ukiwa kwa kipindi ambacho hatujui ni kwa muda gani ilikuwa hivyo mpaka azimio la uumbaji mpya lilipotangazwa.
Na shetani alipokuwa shimoni ndio na yeye akaweka azimio lake ,akaweka azimio hili :
"Isaya 14:12-14.
[13]Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
[14]Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.".
Baada ya azimio hilo kwa sababu ya uchungu wa kushindwa vita na hasara iliyopatikana kwa jeshi lake ya kufukuzwa wote mahali pa raha na furaha (mbinguni) na kuamishiwa shimoni, mahali pa giza na ukiwa kuwa fungu lao, azimio lao lingine likawa ni kuharibu kila alichotengeneza yule Mungu wa haki, kwa kuwa yeye binafsi hawamuwezi tena ki vita, kwa hiyo njia pekee ya kumfanya aonje na yeye joto la jiwe ni kuharibu kazi zake zote njema alizokuwa amefanya,alizokuwa anaendelea kufanya na atakazozifanya kwa baadae, Na ndipo baada ya Mungu wa haki kutambua Nia hii ovu ya kiumbe wake huyu muasi alieshindwa kwenye jaribio la mapinduzi ya kiutawala,na yeye pia katika hekima yake ya kiungu akaamua kuleta tena miradi yake tena ya kiutawala duniani ambapo huyu kiumbe anaishi chini yake (underworld), ingawa ni katika sayari hiyo moja.
Lakini Cha kushangaza alitaka this time awepo mtu wa kuiangalia na kuisimamia hii miradi yaani kwa maana nyingine mtawala wa miradi ya Mungu duniani(Koloni la mbinguni) huku Mungu mwenyewe akiwa amestarehe kwenye kiti chake cha enzi akiendelea kupokea ibada na utukufu na heshima yake kama Mungu, lakini huyu atakakayekuwa mtawala badala ya Mungu duniani lazima aweze kuwa na nguvu za kutawala na kutiisha na kuamrisha chochote katika eneo la utawala wake, kuilinda na kuitetea enzi yake kama tu vile Mungu anavyolinda na kuitetea enzi yake dhidi ya chochote kinachoipinga, kwa hiyo kwa namna yoyote tunategemea kitakachoumbwa hakitakuwa dhaifu au kinyonge, kitakuwa na uwezo kama wa kiungu ingawa sio Mungu lakini lazima awe katika mfano wa Mungu ili aweze kutimiza majukumu hayo ya kiutawala.
Maana malaika wana nguvu ndio hatukatai, lakini wao sio mfano wa Mungu na majukumu ya kiutawala hayawahusu, wao ni watumishi waaminifu na watakatifu tu kutimiza kila kitakachoamriwa kutoka kwenye kiti cha enzi na sio zaidi ya hapo, ila huyu mwingine alitaka aache majukumu ya utumishi aingie kwenye utawala na hayo ndio yaliyomkuta,na ndio likaja azimio la kumfanya mtu kwa mfanano wa Muumbaji mwenye enzi, je mtu huyu atafanikiwa kuilinda milki yake ya utawala(dunia) aliyopewa ki uhalali kabisa? Je ana nguvu kweli za kuitetea kama Mungu alivyoitetea ya kwake (mbingu)?, Itajulikana? Tutaendelea ndugu zangu naomba kuwasilisha kwa sasa [emoji3526][emoji120].
Zaburi 115:15-16
[15]Na mbarikiwe ninyi na BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi.
[16]Mbingu ni mbingu za BWANA, Bali nchi amewapa wanadamu.
Kwenu wana jamii, Mshana Jr.