Mwanzo 1:2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Kwa Sura hii inamaanisha’ Roho Mtakatifu’ alikuwepo wakati wa uumbaji
Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mastari wa 26 ametaja utatu mtakatifu na mstari wa 27 unamaanisha ni Mungu pekee ndie aliumba mwanadamu.
Mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
* kwa hiyo Mungu mwenyewe ndio alimuumba Binadamu