[emoji3588] Human beings ni mnyama kama wanyamapori wowote ila tuna kakitu kidogo kina tutofautisha lakini Kuna wakati tunafanana kabisa
[emoji3588] Huwezi kujua ni dakika ngapi mtu anabadilika au hakuna kipimo duniani Cha kupima mtu anaweza nini tofauti na kufuatilia mienendo ya mabadiliko ya tabia yake. Kwa mtu anayefamya kitu Cha gafla huwashtua watu " Hivi kweli ni Fulani kafanyaa? Siamini"
[emoji3588] Mamlaka zinafanya kazi yake ya kitaalamu ya venting tena kwa kufuatilia mienendo yake yote ya nyuma na kufaulu saafi kabisa lakini, huwezi kujua ni katika point gani tabia ya mtu itabadilika, ama kwa hasira ( provocation) ama kwa ulevi wowote uwe wa madaawa ,pombe au Madaraka ,au kurukwa na akili na kuibadilisha tabia yake au kuibua kitu kilicho ndani Sana kwake ambacho sio rahisi kukigundua kwa vetting.
[emoji3588] Ninamshukuru na kumpongeza Sana Mh. Raisi kwa kuchukua hatua za haraka za kuutengua uwaziri wake ili kumuondolea ministerial immunity na benefits kuviwezesha vyombo vya Dola kushugulikia kwa uhuru TUHUMA dhidi yake ambazo hazijathibitishwa na vilevile kuwa Raisi wa mfano wa kumuwadhibisha waziri ili kulinda image nzuri ya Baraza la mawaziri.
[emoji3588] Hapa Kuna mambo mengi ya kujifunza . Tukumbuke huyu alikuwa upinzani na kule alikuwa kama wenzake na sifa kedekede kuwa ni kamanda, na mkombozi mpaka alipotoka kwa vyeo hivyo. Amepata uongozi yametokea haya,, hizi bado ni tuhuma zinaweza kuthibitishwa au kubatilishwa pale ambapo atapewa haki ya kusikilizwa ( AUDI ALTERAM PARTEM) Lakini mfano ithibitishwe inatupa picha gani kwa Hawa wengine wanaotupigia kelele kuwa ni wakombozi wanasiasa na Wana harakati? Je! Walipata nafasi kumbe yaweza kutokea kama haya kumbe sio malaika
[emoji3588] Kwa upande mwingine unaweza kukuta katika hatua hizi za awali Sasa vyombo vya USALAMA vinaingiliwa na Wana harakati na wanasiasa kushinikiza nini Cha kufanya mtu anaweza kuwaza labda wale so called makamanda ,wakombozi wenzake wamefurahi kwa kuwa aliwatosa au kule alikoenda amechukuwa nafasi za wazawa waliokulia humo, au wanahatakati wamepata platform za kusukuma ajenda hayo ni mambo ya kuchukuliws kwa tahadhari katika hatua hizi
[emoji3588] Yote kwa yote tuachie uhuru vyombo vya Dola na vya kisheria vifanye kazi zao kwenye hili bila uoga au kupendelea pande zozote ili haki ya Kila mmoja ipatikane baada ya mchakato kukamilika. Tofauti na hapo tutakuwa tunahukumu kwa midomo au kutokuhakikisha haki ya kijana inapatikana kama kweli alitendewa jambo hilo la kikatili na la kinyama lakini kama ni tofauti na upande mwingine update haki yake