Kuna timu itawashangaza wengi sana msimu huu kwenye Champions League.
Hamjaizungumzia sana hapa na wengi wanaipuuza. Team hii iangalieni sana kwa makini, wanaweza kutufanyia suprise ambayo hatukutarajia.
Ingaliwe Liverpool kwa jicho la pili. Tuweke ushabiki pembeni, naamini Liverpool kwa sasa wana uwezo wa kuifunga team yoyote kwenye uso wa dunia. Sio Madrid, Barca, PSG, Bayern achilia Man City ambaye mara nyingi ni kibonde wa Liverpool.
Mark my words. Tutegemee suprise kutoka kwa hawa jamaa. Nimekaa nikawaangalia tokea msimu unaanza.
Pale nyuma beki ilikua mbovu Matip na Lovren hawakuweza kutengeneza combination nzuri, wote wawili ni error prone. Usajili wa VVD umestabilize defense ya Liverpool. Hakuna tena yale makosa kama tulivyozoea kuona. Liverpool sahivi wana uwezo kidogo wa ku 'protect the lead'
Kiungo kati achana napo ila tuje kule mbele, false nine Firmino yule jamaa ni mtu mmoja fundi sana, style yake ya ku drop deep na ku hold play ku create pockets of space for Salah na Mane ndio inayoifanya Liverpool saivi inatakata.
Pia ndio beki wa kwanza wa team, jamaa anakaba mwanzo mwisho. Hivyo Liverpool hata wacheze na team gani ni rahisi sana kupata magoli sio chini ya mawili. Ibaki tu kwenye kuzuia.
Kwa hayo basi jamani nawaarifu kuwa hii team tuiangalie kwa jicho la tatu.
Mimi sio mliverpool ila ni mpenzi mmoja wa soka ambae sinaga ushabiki kwenye facts.