JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Bao la kusawazisha la Cristiano Ronaldo limeipa Manchester United pointi moja katika mchezo wa Premier League dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Old Trafford, usiku wa Aprili 28, 2022.
Chelsea walianza kupata bao kupitia kwa Marcos Alonso katika dakika ya 60 lakini United walisawazisha dakika mbili baadaye.
Kwa Matokeo hayo United imebaki nafasi ya sita kwa kuwa na pointi 55, Chelsea imesalia nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 66.