Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Napenda sana kufuatilia habari za kiroho hususani misimbo ya kinabii "prophetic codes". Kuna mengi tumejifunza kuwa ni magumu ila kupitia misimbo mambo huwa bayana.
Bila kuzungusha sana maelezo kilichofanyika usiku wa tarehe 8/12/2023 kwa jina "usiku wa maajabu" ni tukio la kuondoa mazoea na kuonesha uwezekano mpya wa unabii nchini "prophetic paradigm shift". Ni kama Tanzania ilikuwa inahamishwa kwenye mazowea.
Tanzania imekuwa ikisukumwa mara kadhaa kutoka kwenye mazowea na manabii wakubwa ndani ya mwaka 2023. Mwaka huu umefungwa katika namba saba (7) yaani 2+0+2+3=7 ikimaanisha pumziko, mfano ujio wa nabii Uebert Angel nchini ukiwa na mwaliko na Mtumishi Tony Kapola ulikuwa ni kiashiria cha uelekeo wa kinabii nchini.
Ujio wa manabii hawa, Passion Java na Dr. Lovy Elias Longomba ni mwendelezo wa kusafisha njia iliyokuwa na vizuizi vingi sana. Unabii ni moja ya huduma inayokutana na ukinzani mkubwa sana nchini Tanzania. Kwa utafiti mdogo tu nilioufanya katika madhehebu makubwa ya kiroho nchini, unabii haupewi nafasi yake na unaonekana kama huduma inayopoka nafasi na maslahi ya wachungaji. Kwa hifupi manabii huonekana kama wanaingilia huduma tu.
Manabii wanapitia njia ngumu ya kutoaminika na kuchafuliwa zaidi na Watumishi wenzao wa Mungu kuliko waumini wa kawaida. Kuwa na karma ya unabii inayofanya kazi katika makanisa mengi ya kiroho nchini Tanzania ni jambo linaloweza kumfanya mtu kutengwa kabisa na Uongozi wa kanisa.
Waumini wengi leo wanapingwa mambo mengi kutokana na namna walivyofundishwa neno la Mungu na wachungaji wao ila sivyo walivyojifunza au kuelewa neno la Mungu kama lilivyo Kwa kuongozwa na roho Mtakatifu. Chochote kidichowiana na walivyofundudhwa ni upotofu.
Siyo ajabu kuwakuta waumini wengi wakijadili dread locks za Passion Java na Lovy Elias kuliko kile walichojifunza na kupokea kwenye ujio huo. Suala la kujadili Kwa kina ni lengo la usiku wa maajabu ni nini? ila kutokana na kuwa wagumu "rigid" kujifunza tunaishia kukejeli badala ya kuangalia tukio lililopo mbele yetu.