Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
Ujinga ni nini mpendwa?Lakini wakristo wengi ni wajinga kuliko waislam.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ujinga ni nini mpendwa?Lakini wakristo wengi ni wajinga kuliko waislam.
SahihiKweli mkuu,
Mimi toka nikiwa mdogo nilikua na kipaji cha kuona mambo nikisema jambo huwa linakuwa.
Ndoto pia, nikiota , Inakuja hivyo hivyo.
Ila sijawahi jiita mtabiri wala nabii.
But nikikwambia jambo huwa ndio lenyewe ni karama tu Mungu anatugawia lakini hatupaswi kujivunia na kuanza kuvimba nazo.
Inapaswa kumpa Mungu utukufu yeye pekee.
Hakika, ujinga ni kutokataa kujifunza Kwa kulifanya akili kuwa huru kupokea maarifa mapya badala ya kushupaa na kitu kilekile " rigidity"Acha kupotosha watu...Umeamua kuwa mjinga baki nao mwenyewe
Ww unaelewaje hilo neno!?Ujinga ni nini mpendwa?
Mkuu endelea kujifunza lakini kikubwa ruhusu kuwa na akili huru unaweza ukahisi unaona kumbe unaonwa.Muathirika wa mafundisho potofu huyu hapa.
Hata biblia hujui mnabugizwa matango pori tu.
Kuna tofauti kubwa ya mtu kuitwa nabii na unabii.
1. Unaweza kutoa unabii na usiwe nabii.
Rejea Sauli alipotoka kupakwa mafuta na Samweli, alipofika njiani, alikutana na wana wa manabii...akatabiri lakini hakuwa nabii.
2. Kibiblia ili uitwe nabii sio mafundisho, sio kutabiri wala sio kuponya bali ni suala la muda...utabiri mambo na yatokee..
MALISA WAKO ametabiri nini kimkoa, kitaifa au kijamii kikatukia?
3. Kuna kitu kinaitwa neno la maarifa, kinaweza kufanana na unabii lkn sio.
Hii ikoje?
Inatokea unapokuwa unahubiri au kuombea...utahisi hali ya mtu mwenye tatizo...mfano kuumwa kichwa sana upande mmoja.
Ndio maana kanisanisani utasikia mchungaji anasema...kuna mtu anaumwa na kichwa upande wa kushoto na kweli anatokea.
Huu sio unabii bali neno la maarifa.
Huwezi kunielewa ewe kipofu wa rohoni.
Mtatumikishwa na manabii fake hadi mchakae.
Note: utajiri haupatikani kwa maombi wala unabii...ingekuwa hivyo tungekuwa na mabilionea Tanzania.
binti kiziwi
Be blessedHao manabii waafrika wameifanya waafrika kuanza kukubalika Marekani,Ulaya na Asia kuwafundisha.Wamekubali kuwa waafrika tunajua na tunaweza
Manabii wanaokubalika sana nje ya nchi ni huyo Ulbert Angel,Nabii Lovy Elias Nabii Passion Java wanazunguka mabara yote wanaokubalika na kujaza watu wazungu,Wahindi nk wanapokelewa vizuri
Wawe wa kweli au la ninachokiona ni kuwa waafrika tumeanza kukubalika kwenye hayo mabara ni dalili nzuri yaweza kuwa Mungu anataka kufungua milango ya waafrika kuanza kupeleka Injili kwenye Mabara yote na kukubalika huko.Naona mwelekeo mzuri
Wajinga ndio mtaji wa manabiii wa hovyoNapenda sana kufuatilia habari za kiroho hususani misimbo ya kinabii "prophetic codes". Kuna mengi tumejifunza kuwa ni magumu ila kupitia misimbo mambo huwa bayana.
Bila kuzungusha sana maelezo kilichofanyika usiku wa tarehe 8/12/2023 kwa jina "usiku wa maajabu" ni tukio la kuondoa mazoea na kuonesha uwezekano mpya wa unabii nchini "prophetic paradigm shift". Ni kama Tanzania ilikuwa inahamishwa kwenye mazowea.
Tanzania imekuwa ikisukumwa mara kadhaa kutoka kwenye mazowea na manabii wakubwa ndani ya mwaka 2023. Mwaka huu umefungwa katika namba saba (7) yaani 2+0+2+3=7 ikimaanisha pumziko, mfano ujio wa nabii Uebert Angel nchini ukiwa na mwaliko na Mtumishi Tony Kapola ulikuwa ni kiashiria cha uelekeo wa kinabii nchini.
Ujio wa manabii hawa, Passion Java na Dr. Lovy Elias Longomba ni mwendelezo wa kusafisha njia iliyokuwa na vizuizi vingi sana. Unabii ni moja ya huduma inayokutana na ukinzani mkubwa sana nchini Tanzania. Kwa utafiti mdogo tu nilioufanya katika madhehebu makubwa ya kiroho nchini, unabii haupewi nafasi yake na unaonekana kama huduma inayopoka nafasi na maslahi ya wachungaji. Kwa hifupi manabii huonekana kama wanaingilia huduma tu.
Manabii wanapitia njia ngumu ya kutoaminika na kuchafuliwa zaidi na Watumishi wenzao wa Mungu kuliko waumini wa kawaida. Kuwa na karma ya unabii inayofanya kazi katika makanisa mengi ya kiroho nchini Tanzania ni jambo linaloweza kumfanya mtu kutengwa kabisa na Uongozi wa kanisa.
Waumini wengi leo wanapingwa mambo mengi kutokana na namna walivyofundishwa neno la Mungu na wachungaji wao ila sivyo walivyojifunza au kuelewa neno la Mungu kama lilivyo Kwa kuongozwa na roho Mtakatifu. Chochote kidichowiana na walivyofundudhwa ni upotofu.
Siyo ajabu kuwakuta waumini wengi wakijadili dread locks za Passion Java na Lovy Elias kuliko kile walichojifunza na kupokea kwenye ujio huo. Suala la kujadili Kwa kina ni lengo la usiku wa maajabu ni nini? ila kutokana na kuwa wagumu "rigid" kujifunza tunaishia kukejeli badala ya kuangalia tukio lililopo mbele yetu.
Ujinga kama maarifa ni suala la kukubali tu,Mtaji viongozi wa dini yetu ya kikristo ni ujinga tulionao waamini , michango michango, matoleo sijui mavuno sijui Nini , mbona waislamu viongozi wao ni wakawaida tu hatusikii malalamiko ya michango Wala maigizo ya kuponyana na kufufuana. Ukitaka kubatiza mtoto v8z8ngiti kibao. Ukitaka kuoa vizingiti , kuachana napo tabu.
mweeeeee kwale mayito kwenoko ,kulagha nenga
Wajinga ni akina nani? Wana sifa zipi? Unatumia kipimo gani kupima ujinga au uhovyo wa nabii?..Wajinga ndio mtaji wa manabiii wa hovyo
Sina mdogo katika ukoo aliyewahi kufanya hivyo, huenda unachanganyaNyie kina Mlaki mnakuwaga na matatizo tu karibia wote kwenye ukoo wenu. Yule mdogo wenu alienda kugombea ubunge nilijua ndo popoma kuliko wote ila sasa nimekuona wewe na mawazo yako nime change mtazamo kwa kweli.
Hao wanaitwa manabii wa uongo wamekuja kuliamsha kanisa liwe na uamsho sababu wanaojazana huko wanatoka kwenye hayo Makanisa makubwaWajinga ndio mtaji wa manabiii wa hovyo
Wachaga mmevurugwa sanq na ushirikina pamoja na maombezi fake, mna tamaa mno endelea kucheza kanariMkuu endelea kujifunza lakini kikubwa ruhusu kuwa na akili huru unaweza ukahisi unaona kumbe unaonwa.
Mkuu Glenn ruhusu akili yako kujifunza kwanzaWachaga mmevurugwa sanq na ushirikina pamoja na maombezi fake, mna tamaa mno endelea kucheza kanari
Unaweza kuniambia hapa Kanisa linanisaidia vipi leo nikilala njaa?kodi yangu ya nyumba ikiisha Kanisa litanisaidiaje?Hao wanaitwa manabii wa uongo wamekuja kuliamsha kanisa liwe na uamsho sababu wanaojazana huko wanatoka kwenye hayo Makanisa makubwa
Ni kuwa hayo makubwa hayana majibu Kwa shida za waumini wao wako nazo .Waamke wawe na majibu Kwa shida za waumini wao sio tu kukusanya sadaka