Manara adai hakuna wa kumuua Makonda labda afe kwa 'stress' zake mwenyewe. Amtaka awaombe msamaha watanzania kwa dhulma

Manara adai hakuna wa kumuua Makonda labda afe kwa 'stress' zake mwenyewe. Amtaka awaombe msamaha watanzania kwa dhulma

Haki ya Mungu wallah, Manara ni kijana hatari. Sio kwa majibu haya

Manara hajatumia hekima! Siku zote ni vizuri kuacha akiba ya maneno! Watu husema hujafa hujaumbika!! Huwezi kujua ya kesho!! Na huwezi kujua unawakera wangapi ambao Makonda ana connection Nao!! Huwezi kujua kesho Makonda atakuwa nani kwenye Nchi hii! Manara asidhani kuwa hapo kwa GSM ndo kafika na atafia hapo!! Busara inataka ustaarabu na diplomasia!! Kikwete ni mfano mzuri wa ustaarabu na Diplomasia!! Alikuwa anatukanwa akiwa madarakani, aliitwa dhaifu wakati ni jemadari mkuu wa majeshi yetu yote!! Manara jifunze kwa Kikwete!! Vinginevyo usike ukaja hapa siku moja ukiwa unalia na kutafuta huruma za watu mitandaoni!! Mwombe radhi Makonda!!
 
Kwa hiyo tumeshajivika vyeo vya kuhukumu?... Nadhani busara ni kukaa kimya na kujifunza kwa Makonda.

Tomorrow is unpredictable.
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
 
Haji Manara ameendelea kumnanga rafiki yake wa zamani, Paul Makonda ambaye kwasasa yupo kwenye mgogoro mzito na boss wake wa sasa, Gharib Mohammed(GSM). Manara amedai watu wengi wamekimbia nchi kwasababu ya uonevu wa Paul Makonda.

Manara amemtaka Makonda kuacha kutafuta huruma mitandaoni na sasa wanaongozwa kwa utaratibu badala ya ubabe. Pia Manara amehoji nani wa kumuua Makonda zaidi ya 'Stress' na kumtaka arudi Kolomije kwani sasa hana cheo.

Mwisho Manara amemaliza kwa kusema Makonda alilazimisha kuingia chumbani kwake kwasababu choo cha public sio hadhi yake.

Anyways huyu ndugu akiondoka sehemu au hamsini zenu zikiisha hana kifua, atayasema kwa mabaya yote mliyofanya kwa siri na dhahiri, hata GSM ajiandae siku wakienda sideways. Kwa Makonda pole sana, kuna muhenga alisema cheo ni kama koti la kuazima.

Pia, soma=> Paul Makonda: Kuna makundi matano yanataka kuniua, likiwemo wanaotafuta kulipa kisasi kwa Wasaidizi wa Magufuli

=> Haji Manara: Paul Makonda ulinilaza Korokoroni, acha dunia izunguke kwenye Mhimili wake

.....Umenena vyema Manara....Siku ukija huku kijijini kwetu nitakuzawadia JOGOO
 
Sasa kwa waraka huo wa Manara nini tofauti yake na yule Makonda aliyekuwa na kiburi kipindi cha hatamu yake?

Vyovyote itakavyokuwa iwe fundisho tu kwa wengine, natamani wawakate kidole kimoja kimoja, na ikiwezekana wasagwe na bulldozer wote waliokuwa mafedhuli, ili liwe somo kwa wengine
 
Yaani kwa posts hizi dhidi ya Makonda, nimeamini kweli Paul Christian Makonda ni MWAMBA hasa! Hakuna cha kujadili bajeti, wala uzinduzi anaofanya Mama wa SGR ya JPM, wala upandaji wa being wa mafuta. Ni Makonda tu! Kweli wewe ni MWAMBA!
kweli we mwanauchi
 
Hata iblisi hujadiliwa kila cku
Yaani kwa posts hizi dhidi ya Makonda, nimeamini kweli Paul Christian Makonda ni MWAMBA hasa! Hakuna cha kujadili bajeti, wala uzinduzi anaofanya Mama wa SGR ya JPM, wala upandaji wa being wa mafuta. Ni Makonda tu! Kweli wewe ni MWAMBA!
 
Back
Top Bottom