Manara alimvaa Makonda mwaka 2022 katika sakata la GSM

Manara alimvaa Makonda mwaka 2022 katika sakata la GSM

Tukianza kumjadili Manara kwa mitazamo na hulka zake tutakuwa hatuna tofauti na wasengenyaji kitaa kwakuwa haathiri jumuiya kwa maneno yake.

Tumakimike tusije tukaangukia kwenye ule usemi usemao small minds discuss people

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni ajabu. Huyu mwanzisha thread ni kati ya hawa chawa wanaoishi kwa kulamba vidonda vya muuaji Makonda pengine. Makonda karma yake iko njiani na nina uhakika hao watu aliotesa na wengine kuua kuna siku yatamkuta. Anadhani Samia ndiyo Mungu?
 
Screenshot_20190703-134214_WhatsApp.jpg
 
SoMo: usimshambulie, kumtukana mwanasiasa hata Kama katumbuliwa, huwa wanarudi, utakosa pa kuficha sura yako, wengine Wana visasi, kuna watu baada ya kumsikia makonda karudi matumbo ya kuhara yamewabana.

Walioandika kitabu cha kumtukana JPM, sijui wana hali gani
 
Ni kumbukumbu ya kilichotokea mwaka 2022 baada ya sakata la Makonda na GSM.

Ajabu ni pale ambapo Haji Manara bila kueleweka alikotokea, aliamua kuingilia ugomvi usio muhusu. Alimuanika Makonda mchana kweupe na kumdhalilisha vibaya mno...
Kwenye haya maisha nimejifunza somo moja kubwa sana.

Kwamba adui yako au mtu yeyote yule ambaye unamchukia eidha alikudhulumu ama alikufanyia mabaya basi akianguka usije ukamaliza maneno yako yote,maana Mungu huwainua tena watu hawa kwa kishindo.

Hata k
ama umekosana na mtu qeka akiba ya maneno,Mungu hanaga gerentii,anaweza akamuinua unayemchukia alafu kwa kuwa haukumaliza maneno(uliweka akiba)akaja kukusave.

Kuna jamaa mmoja alinichunia hataki kunilipa senti yangu ya muda mrefu sana,nikawaza nikamtemee mbovu nimzingue ila nikakausha.

Siku moja nilipatwa na bonge la janga likanitia adabu sana sina njia,nikarudi kwa yule yule ambaye ana senti yangu,nikamuambia nna shida fanya mpango nipate japo nusu ya ile pesa nayokudai jamaa aliona aibu.

Jamaa alielewa na akanisave nusu ya ile pesa nikaenda kitatua shida yangu,ningemtolea mbovu nisingemfata hata kama namdai.

So tuweke tu akiba ya maneno hatujui mbele yetu
 
Nahisi kuna haja ya kutolewa elimu juu hasa ya kazi/nguvu ya Katibu Itikadi na Uenezi wa chama.

Nahisi kwa mahaba makubwa waliyonayo baadhi ya watu kwa Makonda wanahisi amepewa cheo kikubwa cha kuweza kufanya mabadiliko ama athari yeyote kubwa ikiwemo kulipiza kisasi kwa wale wanaohisiwa kumkosea alipokuwa nje ya ulingo wa siasa.

Kama Makonda ni muelewa nahisi kukaa kwake bench kwa muda ilipaswa iwe kama uamsho wake wa kutafakari kiburi chake ikizingatiwa leo hii aliewahi kumdhalilisha (Chongolo) ni Boss wake.
Ila akitaka kuvumbisha misuli tena aelewe hatofika mbali.
 
Kwenye haya maisha nimejifunza somo moja kubwa sana.

Kwamba adui yako au mtu yeyote yule ambaye unamchukia eidha alikudhulumu ama alikufanyia mabaya basi akianguka usije ukamaliza maneno yako yote,maana Mungu huwainua tena watu hawa kwa kishindo...
Umeongea vizuri ila hapo unavyoona umesaidiwa na jamaa wakati ni hela yako ulikuwa unamdai nimeshangaa... jaribu kutoa mfano mwingine hio mfano hapo ni wa kinyonge sana aisee.
 
Nahisi kuna haja ya kutolewa elimu juu hasa ya kazi/nguvu ya Katibu Itikadi na Uenezi wa chama...
Wewe umeongea vyema. Hicho cheo ni kama mtego... akizingua watamzingua vibaya sana. Mwenezi hana nguvu kubwa. Labda angekuwa mwenezi huku mwenyekiti akiwa JPM.

Pata picha KM chongolo na Makamu Kinana, ambao hao wote alishawanyea sana. Awe makini. Mama hana hizo ishu za ubabe ubabe.
 
Umeongea vizuri ila hapo unavyoona umesaidiwa na jamaa wakati ni hela yako ulikuwa unamdai nimeshangaa... jaribu kutoa mfano mwingine hio mfano hapo ni wa kinyonge sana aisee.
Hayo ni maisha ambayo nimeamua kuishi kaka,na hiyo ndio msimamo wangu,sipigishani kelele na watu kwa mambo ya kawaida.

Haya maisha yanahitaji uvumilivu,na uimara wa moyo.

Kwangu mimi kusamehe pesa ni uvumilivu kuliko kumpiga na kumtukana ninayemdaia huku asinilipe.

Na hii imekuwa inafanya kazi sana kwangu mkuu,so kinachonipa matokeo chanya nakifanya na huwa naishi nacho.
😃😃.
 
Hakuna aliyemsafi,ila kuwa kiongozi bongo raha sana,hata ufanye kosa gani,ukisemwa kuna watakao kuwa wanaumia kwa kusema kwako,mean kila kitu ni usimba na yanga,na viongozi endeleeni tu mijitu yenyewe hii ni coconut head
 
Hayo ni maisha ambayo nimeamua kuishi kaka,na hiyo ndio msimamo wangu,sipigishani kelele na watu kwa mambo ya kawaida.

Haya maisha yanahitaji uvumilivu,na uimara wa moyo.

Kwangu mimi kusamehe pesa ni uvumilivu kuliko kumpiga na kumtukana ninayemdaia huku asinilipe.

Na hii imekuwa inafanya kazi sana kwangu mkuu,so kinachonipa matokeo chanya nakifanya na huwa naishi nacho.
😃😃.
Ndugu uko vizuri sana. Washindi wote huwa wana moyo wa kusamehe. Kwenye hii dunia usipoweza kusamehe hutaishi kwa amani. Ila kwenye baadhi ya mambo usionyeshe unyonge maana watakuonea. Kwa mfano huyo jamaa unayemdai alikuwa ni mtu wa kupelekewa tu moto sio hadi aone aibu ndo akupe nusu ya hela yako.
 
Paul Makonda kajua kuwakomesha watu, tuliwaambia huyo mtu hagusiki bakizeni maneno msije mkaumbuka, sasa kiko wapiiiiiii,

Baba Keagan kanyaga twende, tumechelewa sanaaaaaaaaaa
...Hata wewe ni CHAWA wake ? Sad [emoji45]...
 
Paul Makonda kajua kuwakomesha watu, tuliwaambia huyo mtu hagusiki bakizeni maneno msije mkaumbuka, sasa kiko wapiiiiiii,

Baba Keagan kanyaga twende, tumechelewa sanaaaaaaaaaa
Baba kegan alipotezewa mpaka na wale waliokuwa wanasema mlezi wao wale wachafu, sijui wataanza kujirudisha urafiki Ila kapata funzo la kujua watu wanakupenda ukiwa kwenye nafasi, mungu kamtoa aibu.
 
Paul Makonda kajua kuwakomesha watu, tuliwaambia huyo mtu hagusiki bakizeni maneno msije mkaumbuka, sasa kiko wapiiiiiii,

Baba Keagan kanyaga twende, tumechelewa sanaaaaaaaaaa
Kwani atawafanya nini?

Kumbuka ameteuliwa kwenye chama chake.... Na kikatiba hana mamlaka ya kuamuru kukamatwa mtu...labda atumie njia haramu au magenge
 
Kwani atawafanya nini?

Kumbuka ameteuliwa kwenye chama chake.... Na kikatiba hana mamlaka ya kuamuru kukamatwa mtu...labda atumie njia haramu au magenge
Wapi nimesema anatakiwa amkamate mtu? Hapa tunaonesha kua Mungu akikuandikia NDIO ni ndio tu, hakuna wakusema Hapana.
 
Baba kegan alipotezewa mpaka na wale waliokuwa wanasema mlezi wao wale wachafu, sijui wataanza kujirudisha urafiki Ila kapata funzo la kujua watu wanakupenda ukiwa kwenye nafasi, mungu kamtoa aibu.
Watajirudisha wale hawana aibu, lakini na yeye atakaa kimachale hawezi kujiachia kama mwanzo
 
Wabongo wanafki ukiwa nacho,ukiwa kwenye nafasi utapata marafiki wengi
Kila mtu anasema anakujuwa
Ngoja wale machawa sasa waanze kumsogelea

Ova
 
Ndugu uko vizuri sana. Washindi wote huwa wana moyo wa kusamehe. Kwenye hii dunia usipoweza kusamehe hutaishi kwa amani. Ila kwenye baadhi ya mambo usionyeshe unyonge maana watakuonea. Kwa mfano huyo jamaa unayemdai alikuwa ni mtu wa kupelekewa tu moto sio hadi aone aibu ndo akupe nusu ya hela yako.
Hapana mkuu,kupelekea moto watu sio njia ambazo nazikubali katika kutatua matatizo yangu.

Kuna mambo mengi ya kuangalia kabla ya kufanya maamuzi magumu.

Kuna kanuni zangu mwenyewe naziishi naona zinanipa matokeo chanya kuliko haya mambo ya kupelekea watu moto.

Kama kuna ambao njia hizo huwasaidia waendelee kuzitumia maana siku zote kinachofanya kazi kwangu huwenda kwa mwingine kisifanye kazi
 
Back
Top Bottom