Manara amtaka Waziri Mchengerwa asimamie haki ya kiapo chake cha Katiba

Manara amtaka Waziri Mchengerwa asimamie haki ya kiapo chake cha Katiba

nyehura

Member
Joined
Jun 4, 2022
Posts
6
Reaction score
15
Msemaji wa Yanga Haji Manara ameongea na waandishi wa habari kuelezea sakata lake la kufungiwa kujihusisha na masuala ya michezo ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 2 pamoja na faini ya shilingi milioni 20.

Manara amemtaka Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa kwenda kusimamia haki ya kiapo chake cha Katiba kwa kuhakikisha kanuni zilizotumika kumfungia zinakuwa ni kanuni halali ambazo zimesajiliwa.

“Kwa minajili hiyo mimi na Mchengerwa wote Wandengereko na naamini wandengereko wote tunasimama na haki, Waziri wangu Mchengerwa kasimamie haki ya kiapo chako cha katiba kwamba huwezi kuruhusu kama ulivyosema siku ile kwa mbwembwe kwamba niadhibiwe basi nenda kwa mbwembwe hizohizo kasimamie utekelezaji wa kwamba kanuni lazima zisajiliwe.” Amesema Manara.

Aidha Manara amesema yeye bado ni msemaji halali wa Yanga kwani hajapewa nakala ya hukumu yake ambayo ndiyo inampatia haki ya kukata rufaa.

Akiongea kuhusu sakata la kumtukana Rais wa TFF Wallace Karia amesisitiza kuwa hajafanya kosa kama hilo na hajamtukana Rais Karia zaidi yeye ndiye aliyekosewa na imekuwa ni muendelezo wa kupewa kauli chafu na za kiudhalilishaji kutoka kwa Rais huyo wa TFF.
 
Sema huyu ualbino ndo unamlinda tofauti na hapo kwa namna ya anapoelekea korokoroni pangemuhusu.
 
TFF takadini amearahisishia kazi pigeni ban ya kudumu huyu chizi mvua nguo anayetuharibia mchezo wetu pendwa
Screenshot_20220725-162904.jpg
 
Hapa sasa kajilengesha fresh,anamtuhu waziri kuwa ndiye aliyeshinikiza adhabu ile. Halafu kuna wapumbavu wanataka kwenda kwa Rais kwa ajili ya huyu zeruzeru mvuta bangi.
Unapomgusa Mchengerwa maana yake ni umegusa familia ta SHH directly(ni mkwe wake), sasa sijui anadhani kauli yake juu ya mchengerwa itakuwa na impact gani.
 
Mchengerwa atajua hajui....aliondolewa wizara ya kueleweka kwa kugusa wasiogusika, sasa na huku atapndolewa hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom