Kufanya hivyo ni kumpa kiki. Kama anayoyasema ni kweli, mbona asianzie mahakamani kisha aje na uthibitisho wa mahakama kuwakuta simba na hatia? Kuanza kumkimbiza mwehu aliyenyakua nguo zako ukiwa unaoga angali uko uchi na yeye amevaa nguo, ni kuuambia umma unaokutazama kwamba nawe umeingia kwenye kundi la vichaa. Kujibu tuhuma za manara ambazo hazipo kisheria ni kuzidi kumpandisha zaidi kwasababu atazidi kupata jina. Kumpuuza ni akili kubwa sana jambo ambalo hata manara mwenyewe linamuumiza, anatamani wamjibu ili apate wakumfuatilia zaidi.
Sent from my SM-J530F using
JamiiForums mobile app