Manara kabadilika sana

Anamuheshimu mwajiri wake wa zamani kwa sababu, bakuri la zamani uwezi ukalihita kibakuri
 
Manara wa Simba alikuwa kwenye timu yenye mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi.
Utachangamka vipi kwenye timu inayojipanga kwa Kombe la mapinduzi, wakati umeondoka kwenye timu yenye hadhi sawa na timu kama Al Ahly, Raja Casablanca, Wyadad, Etoile du Sahal, TP Mazembe nk.
Manara wa Yanga ingawa anapata mshahara mzuri lakini anafanya kazi kwenye mazingira magumu, maana timu yake haina cha kujivunia ndani wala nje ya nchi.
 
Ni kweli Manara huyu sio yule wa Simba.
Kiukweli kabisa Simba ajawai kushindwa vita.
Kimsingi inaonyesha kapigwa pin na wenye Yanga.

Kila taarifa saivi inatolewa na yule zuzu Bumbuli.

Manara amebaki kupost mitandaoni km mtu binafsi.

Manara hawezi kuaminika pale Utopoloni. Ikumbukwe ana ugomvi na Mo na CEO wengine wote yuko nao vizuri. Anaweza kutumika na anatumika na Simba. Manara hajawahi kuwa Yanga ni maslahi yamempeleka pale.
 
Hivi,huwa Mnakosa vya kujadili.Huyu bwana mumuambie ashughulike kuikuza Yanga ambayo imedumaa kama kitoto kilichokosa lishe bora kwa miaka mitano.Asipambane na Simba kwa kujidai ni utani.Dunia inazunguka kama arita iliyokauka.He must be very much sensible!
 
Niliwahi kuwaambia watu fulani kuwa Siku Mo akiacha udhamini Simba akaja mwingine na Babra nae akaondoka, watu wasishangae kuona Manara anarudi Simba. Kwanza fikiria Manara japokuwa yupo Yanga kwa sasa lakini Post zake ni kuhusu Simba tu. Tofauti na alivyokuwa Simba, kuna wakati alikuwa anazungumzia ya Simba tu bila kutaja Yanga
 
Nafasi aliokuwa nayo Simba pale Yanga anayo mtu mwengine (Bumbuli). Press zote zinazohusu mechi na matukio muhimu anafanya Bumbuli. Manara ni kama Mzaramo au Bi Hindu wa simba.
[emoji16]
 
manara hana nguvu ile aliyokuwa nayo simba ni suala la muda tu kabla hajapotea
 
Ni kwa sababu unafiki unamshinda!! unajua manara ni simba dam dam ila tumbo nalo linataka na haliwezi kushiba upenzi wa timu!! hadi leo yanga ikifungwa manara anafurahi sana inabidi atafute mahali kama vile chooni afurahie kama akiona hawezi tena kuchekea tumboni. Simba wakifungwa anaugulia tumboni lakini inabidi usoni na mdomoni amfurahishe mwajiri wake mpya ili mkono uende kinywani!! Manara ana kazi kubwa na ngumu sana!!Ila mpaka sasa amejitahidi sana kubalance!! hiyo si kazi ya kitoto!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…