Manara inawezekana ana chembe za usimba lakini sidhani kama Yanga inahujumiwa
Yanga bado Ina tatizo la forward,ndiyo maana hata mechi zilizopita ni ngumu kushinda zaidi ya goli mbili
Nadhani mechi tuliyoshinda goli nyingi ni dhidi ya Dodoma jiji ile round ya Kwanza.
Na magoli mengi yanapatikana kwenye mazingira magumu yaani ni Kama kubahatisha.
Fiston Mayele ni bonge la striker sema tu yupo peke yake na kila timu anayokutana nayo wachezaji wanambana mwanzo mwisho
Kuhusu ukuta Sina tatizo nao, ndiyo maana hata sare zinazotokea hazina magoli,
Nahitimisha kwa kusema hakuna anaye ihujumu Yanga.