Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Februari 25, 2025 Mwanachama wa JamiiForums.com alidai Mji wa Nachingwea una changamoto ya huduma ya maji kwa zaidi ya miezi minne, hali ambayo imekuwa kero kwa Wananchi wengi, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi – Nachingwea (MANAWASA) imetoa ufafanuzi:
Kusoma alichoandika Mwanachama huyo bofya hapa ~ Kuna shida ya Maji wilaya ya Nachingwea mwezi wa nne sasa
HALI YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI KATIKA MJI WA NACHINGWEA
MANAWASA inakiri kuwa mji wa Nachingwea umekuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kutokana na sababu mbalimbali zinazoendelea kushughulikiwa kama zifuatazo;
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA) hadi sasa imechukua hatua mbalimbali ya kuhakikisha hali ya uzalishaji wa maji inatengemaa kama ifuatavyo:
Mamlaka inakusududia kutekeleza mradi wa Shilingi bilioni 2.9 ambao utakuwa na kazi ya kubadilisha bomba kubwa ambalo limekua likipasuka mara kwa mara lenye kipenyo cha milimita 250 umbali wa kilometa 5 kutoka Chiliogoli kwenye tanki la Usambazji maji. Hatua za awali za manunuzi zimeshakamilika na tayari makabrasha ya manunuzi yamewasilishwa kwa katibu mkuu Wizara ya maji kwa ajli ya kuomba fedha za utekelezaji wa mradi.
Mamlaka kwa kushrikiana na Wataalam wa bonde la maji ya Mto Ruvuma na Pwani ya kusini umefanyika utafiti wa vyanzo vipya vya maji chini ya ardhi kwenye maneneo 16 (kumi na sita) ya Nachingwea. Maeneo hayo ni Ruponda sehemu 4, Mkumba shamba 6, Nangoe 2 na Nammanga 4. Visima vitakapokamilika kwa makadilio vitakuwa na uwezo wa kuzalisha maji ya lita 2,000,000 kwa saa.
MANAWASA inaendelea na kutoa maji kwa wateja wake kwa njia ya mgao ili kuhakikisha wateja wanaendelea kupata huduma bila kujali changamoto zote zilizopo.
Ninaomba kuwasilisha.

- Uzalishaji wa maji kuwa mdogo ukilinganisha mahitaji halisi ya maji.
- Mahitaji ya maji ya mji ni lita 6,000,000 kwa siku mbapo uzalishaji kwa siku ni lita 3,000,000 hivyo kuna upungufu wa lita 3,000,000 za maji ili kuweza kutosheleza mahitaji halisi ya mji.
- Kupasuka mara kwa mara kwa bomba kubwa linaloleta maji katika Mji wa Nachingwea kutokea kwenye tanki la usambazaji maji Chiliogoli kumesababisha kupunguza uzalishaji maji.
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA) hadi sasa imechukua hatua mbalimbali ya kuhakikisha hali ya uzalishaji wa maji inatengemaa kama ifuatavyo:
Mamlaka inakusududia kutekeleza mradi wa Shilingi bilioni 2.9 ambao utakuwa na kazi ya kubadilisha bomba kubwa ambalo limekua likipasuka mara kwa mara lenye kipenyo cha milimita 250 umbali wa kilometa 5 kutoka Chiliogoli kwenye tanki la Usambazji maji. Hatua za awali za manunuzi zimeshakamilika na tayari makabrasha ya manunuzi yamewasilishwa kwa katibu mkuu Wizara ya maji kwa ajli ya kuomba fedha za utekelezaji wa mradi.
Mamlaka kwa kushrikiana na Wataalam wa bonde la maji ya Mto Ruvuma na Pwani ya kusini umefanyika utafiti wa vyanzo vipya vya maji chini ya ardhi kwenye maneneo 16 (kumi na sita) ya Nachingwea. Maeneo hayo ni Ruponda sehemu 4, Mkumba shamba 6, Nangoe 2 na Nammanga 4. Visima vitakapokamilika kwa makadilio vitakuwa na uwezo wa kuzalisha maji ya lita 2,000,000 kwa saa.
MANAWASA inaendelea na kutoa maji kwa wateja wake kwa njia ya mgao ili kuhakikisha wateja wanaendelea kupata huduma bila kujali changamoto zote zilizopo.
Ninaomba kuwasilisha.
KIULA MAKALLA KINGU
MKURUGENZI MTENDAJI - MANAWASA
MKURUGENZI MTENDAJI - MANAWASA