Shusha link mzee wa phase 5.
Wahuni wamezima saa 1 kamili
ebwana nilikua sipo online ruka na hii
 
Kwa huu mpira hata kama ni kocha wa mpito unashindwa kujua hawa wachezaji wa United wanashindwaje kufanya vitu basic kabisa uwanja wakiwa na mpira na bila mpira!
 
Nimeangalia msimamo wa ligi baada ya mechi, naweza kubashiri kwa 99.9% kwamba zile timu zote zilizoko top 10 hakuna ambayo tutaishusha/kuifunga comfortably.

Amorin and kazi ya kufanya sio ya kitoto.
 
Huyu Ugarte kuna wasiwasi leo atakula umeme. Yellow card ya pili inamnyemelea.
Baada ya njano amejitahidi sana kucheza kwa umakini, ni mchezaji mzuri sana, sijui ni kwanini yule mjinga alikuwa anamuweka bench.

Garnacho anatakiwa afundishwe kufanya maamuzi uwanjani, ana ubinafsi wa kijinga sana.

Zirkizee sioni kama ana nafasi EPL.
 
Kule mbele kumtegemea Rashy na Zirkzee watupatie uhakika wa goli hata 10 tu kwa msimu ni ndoto. At least Hojlund anasumbuka sema tu upishi nao ni wa kuokoteza.
 
Nimeangalia msimamo wa ligi baada ya mechi, naweza kubashiri kwa 99.9% kwamba zile timu zote zilizoko top 10 hakuna ambayo tutaishusha/kuifunga comfortably.

Amorin and kazi ya kufanya sio ya kitoto.
Wachezaji wa utd ni kama hawajiamini kila wakishika mpira ni kama wanatetemeka na hawajui wapi pakupeleka wanahitaji mwanasaikolojia. Embu angalia jinsi Garnacho alivyopoteza nafasi leo unamlaumuje kocha. Hamad anapaswa kupewa nafasi angalau anaweza kudribble, kufinya, na kutoa pass.
 
Wachezaji wa utd ni kama hawajiamini kila wakishika mpira ni kama wanatetemeka na hawajui wapi pakupeleka wanahitaji mwanasaikolojia. Embu angalia jinsi Garnacho alivyopoteza nafasi leo unamlaumu kocha.
Nikifiria kocha mpya anakuja kufundisha hawa washambuliaji nakata tamaa
 
Siku Rashford akiondolewa United, nitafurahi sana kwa kweli.
Amorin akiwa anampanga regularly, nitajua naye hatakuwa na jipya kama akina EtH tu.
Eneo pekee ambalo naweza kusema tupo vizuri kwa kuangalia ubora na ufundi kwa mchezaji mmoja mmoja ni eneo la ulinzi.

Onana, mazroui, dalot, de ligt, maguire, martinez.

Wote hao wana uwezo wa kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kwa timu nyenginezo.

Shaw, lindelof ni wachezaji wa kuuzwa kama uongozi upo makini.

Kuanzia namba 6 kwenda juu ndipo chaos inapoanzia, ni vurugu, vurugu na vurugu kila siku.

Kuanzia namba 6 panahitaji kusafishwa bila ya huruma na bila ya kurejea makosa ya kiusajili yaliozoeleka kufanywa.

Ni aibu kuwa mpaka leo hii wachezaji wa maana tuliowasajili ni mazroui na martinez.

Aibu kwa fedha iliotumika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…