Katika shabikia shabikia yangu sikuwahi kuona vipigo mfululizonkama hivi.

Kwa vipigo hivi Tenhag huko alipo anatakiwa anyongwe.

Aliwauza Fred,Mactonomy,Olanga, hawa hawakuwa wakuwauza
Ni zamu yenu sasa mmefikiwa,hela zote mlizonazo zinashindwa kuwasaidia.

Timu mnazoweza kuzifunga hazipo top 10,timu ikiwa top 10 hapo mnaacha points.
 
Kazi ipo wallahi hii timu inahitaji maamuzi magumu mno ambayo kwa ninavyoona INOS hawako tayari kuyafanya maana wameanza kulia lia.
Maamuzi magumu yalikua ni kumuachia timu Mwarabu, unaambiwa Sheikh Jassim bin Hamad al Thani ni shabiki lialia wa Man Utd tokea ana miaka miwili.
Mwamba ana mavisima ya mafuta ya kutosha, lengo lake alikua anataka kuitoa Man Utd kwenye mfumo wa kibiashara iwe ni timu ya burudani ndio maana alikua anataka umiliki wa 100%
Hawa watoto wa marehemu pamoja na huyo tajiri mwembamba wote akili zao zinawaza gawio la faida inayopatikana kuliko maendeleo ya timu.
 
Niliwahi kusema humu kuhusu utapeli wa ETH ,Jamaa alipopewa umeneja manjesta,akasajili kampuni lake la uwakala ,ndio likawa linaleta wachezaji linapiga pesa ndefu, wachezaji wengi wakidach au wale aliowataka ETH walipitia kwenye hili kampuni lake ambalo mwanae alikuwa mfanyakazi humo ndani,

Mimi ningekuwa ETH ,sitaki na ukocha Tena naenda zangu visiwa vya Hawaii huko kula Bata tu ,

Jamaa alianza kuwatapeli manjesta kwenye sajili kama za Anthony Santos,kwenye loan fee za matapeli kama Weghorst ,Malacia, n.k

Sitashangaa na Amorini akitafuta kampuni hewa nalo lilete wachezaji wake kwa Bei za kutupa


MANJESTA IMEKUWA SHAMBA LA BIBI
 
Amorini anaonekana hana muda wakubadilisha formation hata atumie 4-2-3-1,4-4-2,4-3-3 yeye inaonesha kakalili 3-4-3

Hiyo formation imewakataa wachezaji karibu wote wa manjesta,imewakubali hasa Mazarawi,Amadi ,Ugale

ila wengi imewakataa ,mtu kama Kobelo Maino anaonekana fala tu sasa hivi,

Bruno anaonekana kama Okajefa ,

Kocha mwingine haraka sana angetafuta formation inayoendana na hao wachezaji

RVN ana coaching nzuri ,alipotumia 4-2-3-1 nilijua tu angeokota alama nyingi

Sasa huyo Amorini anakwambia atasimama na 3-4-3 Hadi afukuzwe

Na Mimi kama mhafidhina nasema hivi aendelee hivo hivo

Conte ni master wa 3-4-3 lakini pale Napoli anacheza 4-2-3-1 au 4-3-3 ,unadhani kwanini?

Huyu Amorin alijua EPL sawa na ligi za wakulima ,

Subiri sasa atachezea vipigo vya kutosha

Wewe formation imewakubali wachezaji hawazidi watano Bado unalazimisha tu

Kobelo Maino ndio namsikitikia sana
 
Kwa maslahi mapana ya afya ya Soka inabidi manjesta washuke daraja

Hii timu iliwahi kucheza OT zaidi ya miaka 10 hakuna penalty inayotolewa

Hii timu imedhulumu sana watu wakimtumia Howard Webb

Mimi naona hapa Bado inabidi mshuke daraja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…